Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,042
- 16,872
Assalam aleykum jami'ya,
Tumsifu Yesu kristo.
Dunia nzima kila kiumbe kinahitaji Uhuru, Amani na utulivu.
Lakini kubwa zaidi tuangazie Uhuru.
Uhuru ni nini?
Kwa definition fupi ni kwamba Uhuru ni hali ya kujiamulia na kupanga mambo yako bila kubughudhiwa au kupangiwa na mtu.
Lakini ni Uhuru gani mtu unatakiwa kuwa nao haswa?
Nafikiri ni Uhuru ambao hautawakwaza wengine na kuwaharibia mudi na mambo yao.
Mfano mtu unaweza kutoa hewa chafu (kuja.....a.)mbele za watu,bila Shaka ni starehe yako na Una Uhuru wa kufanya hivyo lakini tayari utawakwaza watu na ni jambo la aibu pia.
Lakini Unaweza kuingia hotelini na kuagiza chakula Kwa Uhuru na starehe zako lakini ulaji wako unaweza kuwakwaza watu mlioshare meza au sehemu nzima.
Hali kadhalika waweza kufanya tendo la ndoa au ngono na mwenza wako mkiwa huru lakini mkawa kero Kwa wengine kulingana na miguno au kelele zenu.
Hii ni mifano midogo sana namna Uhuru wako usipotumia vizuri unaweza kugeuka mwiba au kero Kwa wengine.
Vipo vitu vingi ambavyo vinampa Uhuru mwanadamu ila ni vikwazo Kwa wengine,na mtu huyu anayekwaza watu inawezekana havunji Sheria ,aidha Sheria hazijatungwa au ni jamii inachukulia mambo mengine ni ya kawaida.
Amani na utulivu vipo sehemu nyingi tu jela na mahabusu Amani ipo ila Uhuru hakuna.
Hata hospital Amani na utulivu vipo Sana Kwanza unakirimiwa,unabembelezwa ule,unafarijiwa na kuoneshwa upendo na ndugu ,jamaa na wauguzi wako ila Uhuru hakuna,kwasababu inawezekana unapangiwa vyakula, muda wa kulala na ikiwezekana hutotumia Tablet yako ama simu ,kwani upo kwenye uangalizi wa wataalamu.
Hebu niache porojo hebu tujiulize maswali haya watanzania..
Tangu tarehe 29 October 2025 yametokea mambo mengi ikiwemo kuharibiwa Mali za taasisi pamoja na za watu binafsi lakini pia ,kuwepo na taarifa mchanganyiko juu ya ripoti ya vifo vya kadhaa.
1.Je watanzania tunafanya vitu Kwa kufuata mkumbo,au tunatafuta Uhuru wa kweli?
2.Inawezekana madai yetu yakawa ni mazuri na yenye mashiko,je njia tunayotumia katika kusaka huo UHURU ni sahihi au tunaburuzwa tu?
3.Tanzania siyo ya mtu mmoja ,rasilimali zote zinapaswa zitufaidishe wote kama wengi wanavyosema lakini je,hakuna njia nyingine salama zaidi tunaweza fikisha ujumbe zaidi ya hii tunayopanga?
UHURU ni jambo muhimu Kwa yeyote ,mtu hawezi kuwa huru ikiwa haridhishwi na taratibu fulani badala yake anajikuta ni kama Mtumwa kwenye himaya yake mwenyewe.
Ndiyo maana mwenye nyumba hawezi ishi na mpangaji asiyefuata taratibu,
Boss hawezi dumu na mfanyakazi asiyefuata maadili ya kazi .
Watu wanahitaji UHURU,AMANI na UTULIVU kuna muda unaweza kutengwa kisa umasikini wako kwakuwa hujavaa vizuri ,hunukii kiujumla haupo smart.watu watakukimbia,na utawalaumu bure,utajiuliza nimewakosea nini lakini ukweli ni kwamba watu hawapendi shida.
Assalam aleykum.