Duh! Ngoja niache ubishi wa kuung'ang'ania huu mtandao. Pole sana. Hivi ingekuwa namba ya mkeo halafu inapokea njemba ya kiume tena choli choli kuch kuch hotae si ingekuwa balaa!
Toka huko baba, unasubiri mpaka yakupate.
Pole sana. Mimi pia walinifanyia hivyo, ilikuwamajira ya saa nane mchana mwaka jana simu iliandikia insert sim card nilidhani labda ni tatizo la simu kushindwa kusoma card nikatoa line na kuirudisha na kuwasha lakini haikuonyesha kama kuna mtandao, kuangalia za wenzangu mtandao upo, bahati nzuri nilkuwa na line ya voda watu wakaanza kuniambia mbona simu yangu ya tigo anapokea mtu mwingine tena yuko lindi? nilivyojaribu kupiga kweli akasema ni namba yake ameinunua ofisi za tigo kama mimi nilivyoinunua tena pale jirani na makao yao makuu, niliwapigia tigo nikawaeleza wakajibu niifuatilie ofisini kwao na nikaenda lakini wakaniambia watanipa namba nyingine kwani ile hawawezi kuirudisha, walisema kuna mfanyakazi ambaye sio mwaminifu anauza namba za watu baada ya kupewa fedha kwa kuzifunga kisha anaihamishia kwa huyo anayeihitaji. hadi leo ile namba ukiipiga inapatikana hewani. tigo ni wahuniMie natumia Mtandao wa TIGO Leo majira ya saa kumi jioni simu yangu ilipoteza network ghafla baada ya kuongea tu na baadhi ya simu. Imekua ni kama desturi toka niingie Jiji la Mwanza wiki iliyopita tigo wamekua na matatizo ya network.
Nilichukulia suala hilo kama la kawaida lakini nikawa najiuliza mbona wengine wanapata network? Nikaamua kutulia nyumbani nikiwa na mawazo ya kwenda Tigo shop siku ya kesho yaani Tarehe 16 november 2011. Mara bimkubwa aliporudi akaniuliza wewe simu yako umempa nani mbona nikipiga anapokea mtu mwingine? nikamwanbia itakua network sababu hata simu yangu haionyeshi network.
Nikachukua simu yake nikapiga akapokea Muhindi nikamuuliza inakuaje namba yangu unapokea ww kila inapopigwa? Umeanza kutumia lini hiyo namba? akajibu wiki hii hapo akili ikanijia Teyari namba yangu ilisha uzwa.
Nimempigia tena sahizi kapokea akaniambia yeye katengenezewa kama special number, nikamjibu isiwe tabu keho nitaenda kufuatilia TIGO.
Mpaka sasa sielewi hiyo namba yangu imechakachuliwa kwa mpango upi na kawa authority gani NAOMBA USHAURI wenu WANAJAMVI NICHUKUE HATUA GANI? sababu nimeitumia namba kwa miaka mingi sana.
Ikiwa namba ni yako na ile fomu ya usajili unayo,nenda kawafungulie tigo mashtaka na uwadai fidia ya tshs 200 miliöni kwa kuingilia uhuru wako wakupata mawasiliano nakuvuruga shugulizako zote kibiasha, kimaisha,pia unaweza kutafta wanasheria ukafungua kesi na utalipwa fidia kubwa.