Uhuni huu wa TBC kuchomoa Signal Cable wakati Bunge Limetota haukubaliki.

Narejea maneno na wosia wa baba yangu ya kwamba '''MTU MPUMBAVU NA MJINGA AKIAMBIWA UKWELI YEYE HUFIKRI ANATUKANWA AMA HAPENDWI''' sasa naanza kuamini kwa hayo yanyotokea kwa tbc-ccm kwa kuamua kukata mawasiliano, lakini pia wakumbuke kwamba '''UKITAKA UBONDIA USIOGOPE NGUMI ZA USO''' bila shaka waliyakubali mageuzi ya vyama vingi kwa kutegemea vitu kama hivi vya kukosolewa sasa kama wao walitegemea kwamba siku zote wapinani wangekuwa watumwa wao na vibaraka wao wametepeta kwa mategemeo yao kudoda.....hahahahahaaaaaaaaaa na bado!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nilifikilia labda mi kadish kamecheze lkn nlvyocheki strength iko 38 wakati hata 18 huwa clear.Lakn siwalaumu ndio matumz kichwa,kwan c unamwona naibu sub ufa hana nywele kabisaaa.....!Mhando ndio ulfundshwa hvo chuo eeh!Hongereni sana Tbc kwa kutumika ila kumbuka 2016 mtakuwa bado hapo?Ni mtazamo tu......!
 
Kilichofanywa leo na TBC bungeni ni aibu ya mwaka. Hakika enzi za chama maarufu zipo ukingoni.
 
TBC wameona naibu spika kabanwa mbavu na mbatia, tundu lisu,manchali sasa wamekata mawasiliaono watanzania tusione kinachoendelea au kujua ni maamzi gani naibu spika ametoa,wabunge hao wlikuwa wanambana mbavu naibu spika kwa kanuni no.77 wakiomba bunge kuahirishwa kwani hawfiki nusu ya wabunge ili wasitahili kuamua kupitisha bajeti ya wizara ya kilimo na ushirika.

Kama ni kweli hawafiki idadi inayotakiwa kwa kanuni mboni ni wazi kanuni itasema nini kinachofuata?
 
Nasikia kabla hata kimemo hakijafika kwenye chumba cha kurushia matangazo pale Bungeni jamaa wa Usalama wa Taifa alichomoa Signal Cable!

Usalama wa Taifa wanatafuta nini TBC inaweza kuwa ni kiongozi wao TBC ni vema tuhuma ziwe na ukweli kuepusha kupandikiza chuki
 
Hii habari sijaielewa kabisa ningeomba muanzisha thread atoe ufafanuzi wa kina kilichojiri huo mjengoni.Walioelewa ni wale wanatazama TBC1 muda huu wengine tunapiga mzigo.

Nami sijaelewa ingawa wengine wanajadili bila kutoa ufafanuzi.
 
Bunge lilikuwa kwenye hatari ya kupitisha bajeti ya Wizara likiwa na wabunge 110 tu wakati kanuni za bunge (kwa idadi ya wabunge waliopo) walipaswa kuwa zaidi ya 172. Wabunge Tungu Lissu, James Mbatia, Moses machali wote wakaomba mwongozo wa Spika. Yeye Mbatia alitoa hoja kutaka wahesabiwe kama wanafikia idadi inayotakiwa.. Naibu spika akaona jaribio lake hapo limefeli baada ya kukuta wapo chini ya namba akasema kengele igongwe wabunge watoro waingie. Bunge likakaa kimya huku wengine wakionekana kuongea. Mhe.Tundu Lissu akasimama. Kabla hajaongea Naibu Spika akasimama.. Akiwa anaongea kwa kusitasita huku akinong'onezana na mhudumu wa Bunge Signal Cable ikachomolewa. (Tunaotumia Satelite cable ikichomolewa inaonyesha)

Tupe habari zaidi basi nini kinaendelea kama bado unaona
 
Wazalendo wote tuwe na faraja kwa kukumbuka usemi huu, 'Siku ya kifo cha nyani, miti yote huteleza'. kifo cha ccm kimewadia sasa.
 
TBC wanaendeshwa kwa remote - robot design. Yaani mtu yeyote wa Ikulu anaweza kuwapigia simu na kusema ''hebu ondokeni hewani until further notice, hii ni amri ya mkuu'' na wao wanakurupuka kutenda kama walivyoagizwa. Ni aibu sana


MMMh chumvi nyingine kali?????
 
bunge lilikuwa kwenye hatari ya kupitisha bajeti ya wizara likiwa na wabunge 110 tu wakati kanuni za bunge (kwa idadi ya wabunge waliopo) walipaswa kuwa zaidi ya 172. Wabunge tungu lissu, james mbatia, moses machali wote wakaomba mwongozo wa spika. Yeye mbatia alitoa hoja kutaka wahesabiwe kama wanafikia idadi inayotakiwa.. Naibu spika akaona jaribio lake hapo limefeli baada ya kukuta wapo chini ya namba akasema kengele igongwe wabunge watoro waingie. Bunge likakaa kimya huku wengine wakionekana kuongea. Mhe.tundu lissu akasimama. Kabla hajaongea naibu spika akasimama.. Akiwa anaongea kwa kusitasita huku akinong'onezana na mhudumu wa bunge signal cable ikachomolewa. (tunaotumia satelite cable ikichomolewa inaonyesha)
kwa yoyote mwenye kipande cha malumbano ndugai alivyobanwa mbavu tafadhali weka
 
Tuwe na subira hata kama kweli kuna madai ya kukata matangazo kwa makusudi tuangalie mwisho wake
 
Tupe habari zaidi basi nini kinaendelea kama bado unaona

wewe mwanamama una matatizo kweli.. Fuatilia majibu yangu hoko juu na kuna Taarifa nyingine nimeandika. Tatizo lako wewe ni mvivu kusoma.. Hapo juu kuna majibu ya maswali yako yote unayouliza hapa
 
Nasikia kabla hata kimemo hakijafika kwenye chumba cha kurushia matangazo pale Bungeni jamaa wa Usalama wa Taifa alichomoa Signal Cable!

Hebu nijuze mkuu kwani hao usalama wa taifa wanafanya kazi bungeni au ndiyo wanasimamia sound system bungeni?
 
Hii ni aibu ya watawala kwa watawaliwa. Mwisho wake ni kukimbia kabisa...
 
Aisee nilijisikia kichefu chefu sana ile huwezi sema kulikuwa na tatizo la mitambo ni uhuni tu ulifanyika ili tusione kilichoendelea. Mimi nilianza kuwa na mashaka nao tangu jumapili iliyopita katika kipindi cha kapu la tbc tulitegemea watupe matukio muhimu kama taarifa za mtu aliyekamatwa na kwa kumteka dokta ulimboka kama walivyo fanya kwa tukio la serengeti lkn badala yake wakatuletea matukio yasiyo na mvuto. lkn kilichonisikitisha nilisikia neno wewe mnyatulu kaachini wakati tunafuatilia na mnyatulu matangazo gafla yakakatika. ovyoooo
 
Hawafai hata kidogo yaani TBC inachefua ni kichefuchefu tu. Hivi tuambizane fedha za kuondeshea hiyo TBC zinatoka CCM?
Signal Cable ya TBC kutoka Bungeni imechomolewa wakati Naibu spika akitota na Bunge lake baada ya kushindwa kupindisha kanuni za bunge!.. Hata hivyo Mhe.Tundu Lissu alisimama akatukanwa na Mbunge mmoja wa CCM!.. TBC hapa mnapofikia sasa mtachomewa hilo jengo!
 
Back
Top Bottom