Mto Ndumbwi huingia Bahari ya Hindi sehemu za Mbezi Beach. Mto huu una mikoko mingi sehemu hiyo na kama inavyofahamika miti hii ndio mazalia ya samaki hivyo ni muhimu kuhifadhiwa. Huko nyuma kama miaka miwili iliyopita marehemu mama Lwakatare[ R.I.P] alijenga nyumba yake ya kifahali pembeni ya mto huo na sio mbali na ufukwe wa bahari.
Kitendo hicho cha ujenzi ule kulileta malalamiko mengi kwa wana mazingira kwani kilikuwa kinakiuka sheria inayolinda fukwe za bahari. lakini hata hivyo marehemu hakulazimishwa kuvunja jumba lake kama sheria inavyosema kwa kuwa tu alikuwa Mbunge na hivyo kutumia influence yake.
Kwa bahati mbaya sana hapo hapo karibu na nyumba ya marehemu kuna sehemu ya wazi ambayo mara nyingi wavamizi wa viwanja wamejaribu kujenga nyumba sambamba kabisa na mto; huko nyuma juhudi zao zilishindwa kwani Manispaa ya Kinondoni ilikuwa inabomoa majengo na kuta zilizokuwwa zinasimamishwa kinyume na sheria.
Kitu cha kushangaza hivi sasa kuna mtu anazungusha ukuta na kuanza kujenga kwenye hiyo open space ambayo huko nyuma ilikatazwa kwa sababu za kulinda mikoko na mazingira ya sehemu mto unapoingia baharini! Nadhani kwavile bunge li karibu kuvunjwa wavamizi hawa wa viwanja na wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni wasio waaminifu, wanataka kutumia mwanya huo wakidhania kuwa hakutakuwa na viongozi wa serikali watakaokuwa makini na ulinzi wa mazingira ya mto sehemu hii.
Ningewasihi wahusika katika wizara ya mazingira kufanya haraka na kutembelea sehemu hii na kuona uharibifu unaofanywa na watu wasiojali athari wanazozifanya kwa jamii. Ni muhimu kusimamisha ujenzi unaoendelea mapema iwezekanavyo na pia kuvunja kuta za nyumba zilizojengwa karibu na ukingo wa mto. Nategemea Mheshimiwa Azzan Zungu waziri mwenye dhamana ya mazingira atapata taarifa ya malalamiko haya na kuchuka hatua kabla ya Bunge kuvunjwa.