Uharibifu wa mali na mazao unaosababishwa na mifugo; nani aadhibiwe, mfugo au mchungaji (mchungi)

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,213
2,812
Samahani wataalamu wa lugha kama nimevuruga hapo juu

Tuingie kwenye mada...
1.Kuna baadhi ya watu akiona mifugo mathalani ng'ombe au mbuzi wanaleta uharibifu kwake basi anachukua silaha na kuwaadhibu kanakwamba mifugo hao watamuelewa na wasirudie kitendo hicho tena

2.Wengine huchukua hatua ya kumtoa kafara mnyama mmoja au wawiliwatatu na kujipatia kitoweo cha dharula basi anakuwa anajihisi amejilipa kwa hasara aliyoingizwa na wanyama hao (japo kuna jamii hii kitu mtu hajaribu akihofia kuvimba tumbo, kufa au kutoa sauti ya (kulia kama) mnyama huyo)

3.Kuna ambao wao huzuia mfugo mmoja au mifugo kadhaa kuwakilisha mingine au mifugo yote na kumngojea mwenye mifugo waje wahesabu mguu kwa mguu kwato kwa kwato wapigiane tathmini ya uharibifu

4.Wengine nao hutega sumu (kabla mifugo kuingia) na kuua wanyama kikatili wote watakaohusika kuleta uharibifu (hii inaitwa tukose wote)

5.Wengine humkamata mchungi na kumuadhibu heavily iwe fundisho kwa wachungi wengine

6.Wengine nao wanaona isiwe tabu basi wanaamua kurudisha mashambulizi (ya uharibifu) kivingine

Mambo hayo yana changamoto zake na mafanikio yake kwani wengine hufika mbali sana kwa maswala ya uharibifu wa mifugo. Kupitia mambo hayo watu wanaingia uhasama wa kudumu, vita na wengine wanapata vilema, kesi kubwakubwa, maradhi ya hatari na hata vifo.

Hayo na mengine yote yanayofanywa kwajili ya kesi za uharibifu wa mifugo yanaangukia sehemu mbili... kwanza ni adhabu kwa mfugo na/au pili ni adhabu kwa mwenye mfugo. Sasa ipi ni sahihi? Nadhani swali langu limeeleweka

Msimamo wangu:
Ni bora yule anayemkamata mchungi na kumcharaza henzilani hadharani kuliko kuua wanyama pasipo hatia halafu hata hakuna hasara yoyote unayokuwa umefidia. Ni angalau kwa mbali pia yule anayejipongeza kwa kitoweo kwasababu itamfanya mhusika awe na machungu na azidishe umakini zaidi juu ya mifugo yake.

Tusiadhibu mifugo kwani haijui chochote na ni ukatili uliopitiliza!
 
Tuliochunga tunajua mifugo inavyotamani mazao shambani kwa mtu,unakuta shamba halina uzio imara mifugo inavamia shamba kwa kasi, au umetorokwa na mifugo na imepotea na kuibukia shambani kwa mtu.

Kupona labda mwenye shamba awe hayupo hapo,ukiiona ipo shambani kwa mtu unaitoa fasta,vinginevyo utaadhbiwa vikali na kesi ya fidia italipwa.Wenye mashamba wengine ni jeuri wanaacha mifugo iharibu zaidi ili kupata fidia kubwa.

Wafugaji wengine nao ni jeuri,wanaingiza mifugo shambani kibabe mifugo yao ile mazao ishibe vizuri ikatoe maziwa mengi na kuzaliana kwa wingi.Mkulima ukileta za kuleta unaulizwa ulipwe fidia ng'ombe wangapi?,msipoelewana ugomvi unatokea.

Utatetewa na wakulima wenzako na wafugaji nao wanamtemtea mwenzao,ni ugomvi kati ya wakulima na wafugaji mpaka polisi waje kutuliza fujo
 
Back
Top Bottom