Uharamia bei za vifurushi una baraka za Nape na Serikali kwa kuihofia Mitandao!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Serikali inaogopa unganiko la watanzania kupitia mitandao ya kijamii!

Serikali haipendezwi na ukosoaji mkubwa inaoupata kupitia Mitandao ya kijamii!

Je, "Internet"nayo inaagizwa kutoka Ukraine?

Iweje Serikali kukaa Kimya huku kampuni za simu zikituibia mchana kweupe?

Bundle ina Expire huku zikiwa bado MB's na GB's zikiwa zinasoma kwenye salio!
Je! Hizo huwa zinapelekwa wapi?

Kwanini mteja asiunganishiwe salio lake la Internet kwenye Bundle lake jipya?

Lakini pia kuna sababu gani kuweka ukomo wa Bundle wakati,tayari limekwisha lipiwa na mteja husika?

Kwa nini serikali kupitia "TCRA"haiwajibiki ipasavyo kwa kutuwekea
"Internet Bundle Usage reading Meters"
kama kigezo cha lazima kwenye matumizi ya Internet sambamba na ilivyo kwenye muda wa Maongezi.

Kwa nini tupewe taarifa ya matumizi ya dakika na sekunde,kwenye maongezi ya simu,na hatupewi taarifa kama hizo,kwenye matumizi ya Internet?
Wakati kampuni na system inayomiliki vyote hivyo ni hiyohiyo?

Kwa kitendo cha Nape kukaa kimya!
Huenda na yeye ana maslahi binafsi kutoka kwenye hayo mapunjo tunayopunjwa.
Na huenda amewekwa kwenye "Paylist"zao

Kwa kitendo cha serikali ya CCM kukaa kimya juu ya hili.
Ina maanisha kuwa ni njia ya kupunguza nguvu ya ukosoaji toka kwa jamii,kupitia Mitandao ya kijamii.

Jumapili Njema.

Alamsikhi!
 
Bila Samia kuwaondoa Nape ,awesona mwigulu ahesabu ameumia

USSR
Uko sahihi wala hilo halihitaji degree kuliona mkuu USSR !

Nchi hii,watakaofanikiwa kufika nayo,watafika wakiwa wanatembelea magiti.
 
Hamna, hawaogopi maoni ya watu kiasi hicho

Yule mwendawazimu mnayemuabudu yeye alikuwa akikakamta, kuteka alipoona vyote vimeshindwa kunyamazisha aliizima kabisa

Ila hata alipozimà spana zikaendelea hadi zikamsababishia matatizo ya moyo

Alitamka angetamani malaika washuke waizime
 
Namna wanavyotukandamiza utadhani wataishi milele kwenye hayo ma V8.

Time will come.
 
Mitandao karibu yote ya simu inamilikiwa.na wanasiasa mafisadi wa CCM, wengine wako madarakani. Hakuna nchi iloyowahi kuendelea chini uongozi wa genge la mafisadi
 
Vyama vya kadhaa vya siasa vikeshajipambanua kulamba asali ndo maana wapo bize na kudandia ziara za chama twawala badala ya kusimamia misingi ya kuwapazia wananchi sauti.
Dawa ya CCM ni 2024 na 2025 iwapo wenye nia ovu na nchi hii wataacha kukibeba
 
Hamna, hawaogopi maoni ya watu kiasi hicho

Yule mwendawazimu mnayemuabudu yeye alikuwa akikakamta, kuteka alipoona vyote vimeshindwa kunyamazisha aliizima kabisa

Ila hata alipozimà spana zikaendelea hadi zikamsababishia matatizo ya moyo

Alitamka angetamani malaika washuke waizime
Kwa hiyo Muuaji wenu Dakataa! Janabaa! alisukumwa na nguvu za mtandao akafanya alivyoagizwa?
 
Namna wanavyotukandamiza utadhani wataishi milele kwenye hayo ma V8.

Time will come.
Tatizo utawala huleta upofu,utawala humfanya mtu kuishi kama mateka!
Utawala humuondolea mtu marafiki wa kweli.
Utawala humfanya mtu kupoteza hofu ya Mungu na kukimbatia hofu ya Umaskini.
 
Hamna, hawaogopi maoni ya watu kiasi hicho

Yule mwendawazimu mnayemuabudu yeye alikuwa akikakamta, kuteka alipoona vyote vimeshindwa kunyamazisha aliizima kabisa

Ila hata alipozimà spana zikaendelea hadi zikamsababishia matatizo ya moyo

Alitamka angetamani malaika washuke waizime
Huyo hayupo tena. Hizi gharama zinabaraka kutoka juu, mawaziri ni watekelezaji tu.
 
Back
Top Bottom