IHOLOMELA
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,807
- 1,677
Utumika kama kitambulisho tena chenye kuaminika sana kwenye taasisi nyingi tu za huduma.Sema wwe utembei,ukiwa na vitambulisho vyote ukavitoa sehemu husika wakitaka kimoja paspot ndo itakuwa chaguo La kwanza kabla ya vingine.
Mkuu unanifahamu hadi useme mie sitembei? Hahahaaa duh! Kinachosumbua watu wengi humu ni kutokuelewa Pasipoti ni kitu gani. Toka mwanzo nimesema kuwa ili upate pasipoti lazima uwe na dhamira ya safari, pasipoti hutolewa kwa kuangalia hizo dhamira ambazo huletwa kwa maandishi (viambato) mfano unaenda India kutibiwa, lazima uje na barua toka wizara ya Afya yenye kuthibitisha hilo.
Sasa ukienda Uhamiaji kuomba pasipoti ili utumie kama kitambulisho kuwa ww ni raia wa Tanzania watakuelekeza nenda NIDA. Sijakataa kuwa pasipoti inaweza kutumika kufanya usajili wa akaunti ya Benki sawa na kadi ya mpiga kura inavyotumika lakini hilo sio lengo lake. Lengo la kuwa na pasipoti ni kusafiri nje ya nchi, full stop.