Uhamiaji wamezuia passport yangu!

Uhamiaji wamezuia passport yangu!

Natumai wote muwazima, na pia familia zenu, na marafiki wanaendelea vyema.

Mimi nina swali linanitatiza juu ya uhamiaji, nimeomba passport baada ya kupotea mbaya zaidi wameizuia kwa muda wa miezi 6 yaani mpaka mwezi wa 5 mwakani, ila nasikia mara nyingi inaashiria inahitajika rushwa ili kuipata kwa haraka na mapema tofauti na muda tajwa.

Tafadhalini nisahihisheni kama nimekosea.

Ahsanteni,
Wako sahihi kabisa. Kanuni zinaeleza kwamba mtu akipoteza au kuibiwa passport kabla hajapewa pasi ingine lazima atoe taarifa polisi na kupewa Loss Report Form halafu atangaze gazetini, baada ya siku 180 ndio apewe passport ingine. Hivyo kuwa mpole tu
 
Kijana naomba uwe makini na taarifa unayotoa kuhusu UHAMIAJI.

Uhamiaji sio idara ya kufanya mambo kwa kukurupuka. wanafanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu.

Kwanza umesema umepoteza? hapo kuna changamoto na lazima uchunguzi ufanyike wa kina tofauti na hapo wao wanaweza kuwa hatiani.

Je utajuaje pasi yako inatumiwa na mtu mwingine kimakosa?

Na ddiyo maana sheria inasema untakiwa utangaze kwenye gazeti ya serikali ukiwa na RB, kisha ukae mda sio chini ya miezi 3 au 6 kubaini pengine imeokotwa.

Baada ya hapo utaandika Barua kwa mkono wako kwa kuomba Mkurugenzi wa Uhamiaji namna pasi yako ilivyopoatea na hatua ulizochukua pia pasipo kusahau kueleza sababu ya kuomba ya pili?

Kisha uwape uhamiaji mda wa kufanya uchunguzi wao wa kina.

Hivyo basi nikusihi uwe mvumilivu usipende kusema kuna Rushwa labda wewe ndio uhojiwe kwa nini utake kutoa rushwa, pengine unajua pasi yako ilipo.

Akhsante.
Safi sana. Na kingine ajue kuwa ni kosa kutumia pasport mbili zilizo valid kwa wakati mmoja, akipewa pasi ndani ya wiki halafu ile ingine ikapatikana anaweza asiipeleke uhamiaji akaamua kukaa nayo hivyo tayar anakuwa anatenda makosa
 
Kwanini Tanzania suala la passport linakua kero sana? Mimi nilidhani passport ni haki yangu na pia ni njia rahisi ya kutumika kama kitambulisho. Kuwa na passport si lazima nisafiri. Sijui lini hii idara itskua na watu wrnye weledi kuiboresha same kwa jeshi la polisi. Pale jeshi litakapotambua kuwa wao si maagent wa serikali na chama tawala bali wapo kwaajili kulinda usalama ws kila mtanzania na mtu yeyote aliyepo nchini awe kihalali ama kimagumashi. Haki inatakiwa kutendwa kwa yeyote yule
Pasipoti sio kitambulisho ukae nayo tu bila kusafiria. Ni hati ya kusafiri nje ya nchi, sasa kama huna safari waachie wenye safar wapewe
 
Kijana naomba uwe makini na taarifa unayotoa kuhusu UHAMIAJI.

Uhamiaji sio idara ya kufanya mambo kwa kukurupuka. wanafanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu.

Kwanza umesema umepoteza? hapo kuna changamoto na lazima uchunguzi ufanyike wa kina tofauti na hapo wao wanaweza kuwa hatiani.

Je utajuaje pasi yako inatumiwa na mtu mwingine kimakosa?

Na ddiyo maana sheria inasema untakiwa utangaze kwenye gazeti ya serikali ukiwa na RB, kisha ukae mda sio chini ya miezi 3 au 6 kubaini pengine imeokotwa.

Baada ya hapo utaandika Barua kwa mkono wako kwa kuomba Mkurugenzi wa Uhamiaji namna pasi yako ilivyopoatea na hatua ulizochukua pia pasipo kusahau kueleza sababu ya kuomba ya pili?

Kisha uwape uhamiaji mda wa kufanya uchunguzi wao wa kina.

Hivyo basi nikusihi uwe mvumilivu usipende kusema kuna Rushwa labda wewe ndio uhojiwe kwa nini utake kutoa rushwa, pengine unajua pasi yako ilipo.

Akhsante.
unaakili kinoma safiii
 
Pasipoti sio kitambulisho ukae nayo tu bila kusafiria. Ni hati ya kusafiri nje ya nchi, sasa kama huna safari waachie wenye safar wapewe
Kwa Tanzania labda ukienda nchi za wastaarabu passport driving licence vinatumika kama vitambulisho. Halafu ikitokea leo mgonjwa na unatakiwa kupelekwa nje kwa matibabu huoni kama kuwa na passport mkononi kutakusaidia badala ya kuanza process chovu kuipata?. Passport ni kama leseni ya gari mbona watu wanapewa bila kuwa na gari.

Mawazo kama watu kama ninyi yanafanya mambo madogo kama haya na haki za watu yawe magumu. Nikihitaji passport siyo kazi ya serikali kujua lini nitasafiri hii ni karne ya 21 kila mtu ana haki ya kuwa nayo mradi tu ni raia halalif.
an official document issued by a government, certifying the holder's identity and citizenship and entitling them to travel under its protection to and from foreign countries. Hii ni maana ya passport inathibitisha utambulisho na uraia wa mmiliki. Ndiyo maana ni moja ya vitambulisho muhimu
 
Pasipoti sio kitambulisho ukae nayo tu bila kusafiria. Ni hati ya kusafiri nje ya nchi, sasa kama huna safari waachie wenye safar wapewe
Ukute una degree na unajiona msomi. Mawazo ya kama yako ndio chanzo cha nchi hii kutokuendelea
 
Hapana,passport haitakiwi kutumika kama kitambulisho ndani ya nchi.
Kwani unapoenda bank kufungua account hawaipokei passport kuthibitisha identity yako? Mkuu naomba nikuulize kama umebahatika kusafiri nje ya Tanzania.
 
Ukute una degree na unajiona msomi. Mawazo ya kama yako ndio chanzo cha nchi hii kutokuendelea
Ni wakuwaonea huruma mkuu labda hawajui hata maana ya passport ni nini. Labda hata hawajaiona lakini wanataka kuonekana wanachangia hoja.
 
Siku zote mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni watuhumiwa.

Sijapenda uweke dhana kwamba kupata pasi ya kusafiria mpaka utoe rushwa?

Mimi mwenyewe nilishapoteza pasi ya kusafiria. na kwa uhakika nilifuata utaratibu walionielekeza pasipo kutoa hata RUSHWA.

Endelea na dhana ya kutoa rushwa utakuja kutoa rushwa hata kwenye kuandikisha mwanao chekechea maana umeshazoea kutoa rushwa.

Napinga kabisa hakuna rushwa ukiwa umekamilisha mahitaji ya ofisi husika.

Hakuna rushwa Uhamiaji ni dhana potofu mnazozijenga kwa wananchi. hebu fikiria kwa mtu ambaye hata kwa mara ya kwanza hajawahi kumiliki pasi ya kusafiria naye atakuwa anawaza tu rushwa itakapofika wakati wa kufuatilia pasi.

Usipende kuhukumu maana hata wewe utahukumiwa kwa kuhukumu. tusipende maneno ambayo leo ukiambiwa tupe uhakika wa jambo kwa evidence utajikuta hauna hata kidogo.
Rushwa ipo sana Mkuu Tena Sana nishaona kwa mzee wangu elfu 50 inamtoka .. labda imeisha kwa baba Jesca ila ipo sana yaan polizi wakasome kabisa
 
Pasipoti sio kitambulisho ukae nayo tu bila kusafiria. Ni hati ya kusafiri nje ya nchi, sasa kama huna safari waachie wenye safar wapewe
What is considered a valid form of ID?What are considered valid forms of ID? ... ( Social Security Card, from the USA Social Security Administration, with your signature AND Photo Identification with your signature ie: unexpired driver's license, government issued identification card, military identification or passport).
Angalia mnawaiga kuvaa milegeezo na kutoboa masikio lakini ya maana mnayaacha.
 
Nashukuru Mimi nimechukua yangu leo japo kuna mazingira ya kutengeneza rushwa ila nashukuru sijatumia zaidi ya (80,000/= ) 10,000/= ya kujaza form online, 20,000/= ya wakili kwa ajili ya kiapo cha changu na cha mzazi na 50,000/= ya Ada, nilijiandikisha tarehe 18/10/2017 imetoka 19/12/2017 japo nishaenda pale zaidi ya mara tatu kuangalia, Leo ndiyo nimefanikiwa kuikabidhiwa
Hapo bado imekaa muda mi yangu niliipata kwa wiki mbili ni kwa sababu ya kufahaminazesheni hata hivyo nililiwa 40000 plus 50000 ikawa 90000 rushwa iko sana pale
 
Hapo bado imekaa muda mi yangu niliipata kwa wiki mbili ni kwa sababu ya kufahaminazesheni hata hivyo nililiwa 40000 plus 50000 ikawa 90000 rushwa iko sana pale
Mie niligoma kutoa rushwa usawa huu mgumu, ila mwezi wa tatu huu bado naisubiri naambiwa makaratasi yameisha!!!
 
Kule +254 niliona wana apply kwenye simu wiki mbili tu passport unayo mkononi.
 
Pasipoti sio kitambulisho ukae nayo tu bila kusafiria. Ni hati ya kusafiri nje ya nchi, sasa kama huna safari waachie wenye safar wapewe
Utumika kama kitambulisho tena chenye kuaminika sana kwenye taasisi nyingi tu za huduma.Sema wwe utembei,ukiwa na vitambulisho vyote ukavitoa sehemu husika wakitaka kimoja paspot ndo itakuwa chaguo La kwanza kabla ya vingine.
 
Hawa watu hawajasafiri hawajui kabisa umuhimu wa passport. Wangejiuliza inakuwaje upatikanaji wake unakubidi uonyeshe cheti cha kuzaliwa ama utie affidavit basi wangejua umuhimu wa hiki kitambulisho.
 
Kule +254 niliona wana apply kwenye simu wiki mbili tu passport unayo mkononi.
Hiyo lazima itakua ku renew kwa mara ya kwanza kwa miaka hii huwezi apply online na ukapewa lazima uthibitisho maana ni miaka ya biometric
 
Ni kweli rushwa ipo sana, nilishuhudia mama mmoja tarehe 12 February akihitaji passport ya kwenda matibabu nje alizungushwa sana mara aambiwe apeleke vielelezo mara vitambulisho, tukamshauri aombe kuonana na Mkurugenzi wa Uhamiaji, baada ya wale wahudumu kugundua kuwa yule mama yupo kwenye hiyo process ya kwenda kwa Mkurugenzi, wakampa pass in less than one hour kitu kilichoashiria kuwa walikuwa wameprint tayari isipokuwa hawakutaka kumpa, mwingine alikuwa anasafiriri kwenda Nordic countries, tena huyu alikuwa anarenew naye wakamwambia ataiapta kesho yake, alipokwenda kwa boss wao akaambiwa asubiri passport apewe siku hiyohoyo na akapewa.

Mchezo wa rushwa unachezwa na wale maofisa waliopo kwenye yale madirisha siyo viongozi, nilichojifunza ni kuwa ukipata nafasi ya kuonana na viongozi ukawaambia shida yako wakakuelewa basi hutoi hata senti moja
Mi pale dirishani nimeambiwa nipeleke vitu vingi kweli halaf wananiambia wana mwanasheria pale anatoa affidavit kwa 30000 wakati mi najua affidavit ni elfu kumi tu,nikajiuliza hawaogopi kurekodiwa
Halaf ina maana kupata passport mpaka uwe na vielelezo vingi barua ya mwaliko ,copy ya passport ya anaekualika,,sijui niniiii
Ina hawawezi kukupa passport tu mpaka yote hayo,,au sio haki ya mtanzania kupata pass?
 
Nashukuru Mimi nimechukua yangu leo japo kuna mazingira ya kutengeneza rushwa ila nashukuru sijatumia zaidi ya (80,000/= ) 10,000/= ya kujaza form online, 20,000/= ya wakili kwa ajili ya kiapo cha changu na cha mzazi na 50,000/= ya Ada, nilijiandikisha tarehe 18/10/2017 imetoka 19/12/2017 japo nishaenda pale zaidi ya mara tatu kuangalia, Leo ndiyo nimefanikiwa kuikabidhiwa
Walikuuliza ya nini?
Je ulienda na docoment zipi
Maana nami nahitaji passport ila mizinguo balaa
 
Back
Top Bottom