Uhamiaji wamezuia passport yangu!

Uhamiaji wamezuia passport yangu!

Walikuuliza ya nini?
Je ulienda na docoment zipi
Maana nami nahitaji passport ila mizinguo balaa
Nilienda na cheti cha kuzaliwa na lessening ya kuendeshea gari, Mimi nilitaka ya kikazi niakaambiwa nionyeshe barua ya mwajiri wangu nikajiongeza nikawaambia Mimi nafanya kazi za kujitegemea kwenda nje wakaniuliza kama zipi nikajieleza wakaridhika, barua ya kiapo mahakamani ni 5,000/= ila kwa faster ni 10,000/= kwa wanasheria wa mtaani, kwa hiyo bado hujajaza chochote?
 
Kwani unapoenda bank kufungua account hawaipokei passport kuthibitisha identity yako? Mkuu naomba nikuulize kama umebahatika kusafiri nje ya Tanzania.
Nilimsikia waziri ingawa simkumbuki ni wa wizara gani akikemea passport kutumika kama kitambulisho ndani ya nchi,kuhusu kusafiri nje ya nchi yes nimeshasafiri mara mbili
 
Nilienda na cheti cha kuzaliwa na lessening ya kuendeshea gari, Mimi nilitaka ya kikazi niakaambiwa nionyeshe barua ya mwajiri wangu nikajiongeza nikawaambia Mimi nafanya kazi za kujitegemea kwenda nje wakaniuliza kama zipi nikajieleza wakaridhika, barua ya kiapo mahakamani ni 5,000/= ila kwa faster ni 10,000/= kwa wanasheria wa mtaani, kwa hiyo bado hujajaza chochote?
Nimekutumia pm mkuu nijibu kule
 
Siku zote mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni watuhumiwa.

Sijapenda uweke dhana kwamba kupata pasi ya kusafiria mpaka utoe rushwa?

Mimi mwenyewe nilishapoteza pasi ya kusafiria. na kwa uhakika nilifuata utaratibu walionielekeza pasipo kutoa hata RUSHWA.

Endelea na dhana ya kutoa rushwa utakuja kutoa rushwa hata kwenye kuandikisha mwanao chekechea maana umeshazoea kutoa rushwa.

Napinga kabisa hakuna rushwa ukiwa umekamilisha mahitaji ya ofisi husika.

Hakuna rushwa Uhamiaji ni dhana potofu mnazozijenga kwa wananchi. hebu fikiria kwa mtu ambaye hata kwa mara ya kwanza hajawahi kumiliki pasi ya kusafiria naye atakuwa anawaza tu rushwa itakapofika wakati wa kufuatilia pasi.

Usipende kuhukumu maana hata wewe utahukumiwa kwa kuhukumu. tusipende maneno ambayo leo ukiambiwa tupe uhakika wa jambo kwa evidence utajikuta hauna hata kidogo.
Rushwa adui wa haki, ukiwa na mkono mfupi utasugua bechi sana tu. ila kama huna haraka utasubiri sana,ila kama una haraka jiongezeee tu hakuna namna[emoji3]
 
Mie niligoma kutoa rushwa usawa huu mgumu, ila mwezi wa tatu huu bado naisubiri naambiwa makaratasi yameisha!!!
Bila chochote utasubili sana ila kama huna haraka subilia tu mkuu watakupa
 
U
Kwanini Tanzania suala la passport linakua kero sana? Mimi nilidhani passport ni haki yangu na pia ni njia rahisi ya kutumika kama kitambulisho. Kuwa na passport si lazima nisafiri. Sijui lini hii idara itskua na watu wrnye weledi kuiboresha same kwa jeshi la polisi. Pale jeshi litakapotambua kuwa wao si maagent wa serikali na chama tawala bali wapo kwaajili kulinda usalama ws kila mtanzania na mtu yeyote aliyepo nchini awe kihalali ama kimagumashi. Haki inatakiwa kutendwa kwa yeyote yule
Unaelewa maana ya PASSPORT?
Ungekuwa unaelewa maana yake usingelalama
Vp utumie passport kama kirambulisho wakati passport maana yake ni hati ya kusafiria nje ya mipaka
 
Siku hizi nami nashughurikia scholarship ya kwenda kusoma ughaibhuni, lkn katika harakati ya kujaza zile form online ili uwe eligible na kuwa admitted kwenye chuo husika wanataka Passport ya kusafria.
Naombe msaada ni taratibu zipi nizifuate ili niweze kupata kwa muda na ni hela kiasi gani natakiwa kuanda ambazo zipo kisheria kwa ajili ya hiyo passport?
 
Kwa Tanzania labda ukienda nchi za wastaarabu passport driving licence vinatumika kama vitambulisho. Halafu ikitokea leo mgonjwa na unatakiwa kupelekwa nje kwa matibabu huoni kama kuwa na passport mkononi kutakusaidia badala ya kuanza process chovu kuipata?. Passport ni kama leseni ya gari mbona watu wanapewa bila kuwa na gari.

Mawazo kama watu kama ninyi yanafanya mambo madogo kama haya na haki za watu yawe magumu. Nikihitaji passport siyo kazi ya serikali kujua lini nitasafiri hii ni karne ya 21 kila mtu ana haki ya kuwa nayo mradi tu ni raia halalif.
an official document issued by a government, certifying the holder's identity and citizenship and entitling them to travel under its protection to and from foreign countries. Hii ni maana ya passport inathibitisha utambulisho na uraia wa mmiliki. Ndiyo maana ni moja ya vitambulisho muhimu

Ni kweli Tanzania pasipoti haitolewi kwa mtu bila ya kuwa na safari eti akae nayo ndani kama kitambulisho, na ni kweli pasipoti ni haki ya kila raia mwenye dhamira ya kusafiri nje ya nchi. Vitambulisho vya Uraia vipo vinatolewa na NIDA, hio ndio haki ya kila raia kuwa na kitambulisho cha Utaifa. Pasipoti utaitumia kama kitambusho ukiwa nje ya nchi yako ili utambulike wewe ni raia wa nchi gani.
 
U

Unaelewa maana ya PASSPORT?
Ungekuwa unaelewa maana yake usingelalama
Vp utumie passport kama kirambulisho wakati passport maana yake ni hati ya kusafiria nje ya mipaka
Jamaa anafosi vitu ambavyo haviwezekani. Kama anataka kutambulika kuwa ni raia wa Tanzania kuna Vitambulisho vya Utaifa vinatolewa NIDA hio ni haki yake pasipoti ni haki ya raia anayetaka kuvuka mipaka ya nchi.
 
Siku hizi nami nashughurikia scholarship ya kwenda kusoma ughaibhuni, lkn katika harakati ya kujaza zile form online ili uwe eligible na kuwa admitted kwenye chuo husika wanataka Passport ya kusafria.
Naombe msaada ni taratibu zipi nizifuate ili niweze kupata kwa muda na ni hela kiasi gani natakiwa kuanda ambazo zipo kisheria kwa ajili ya hiyo passport?

Screenshot hio page ya kujaza namba za pasipoti iprint attach kwenye maombi yako, wanakusaidia bila shida. kama hujaelewa nifuate PM
 
Mi pale dirishani nimeambiwa nipeleke vitu vingi kweli halaf wananiambia wana mwanasheria pale anatoa affidavit kwa 30000 wakati mi najua affidavit ni elfu kumi tu,nikajiuliza hawaogopi kurekodiwa
Halaf ina maana kupata passport mpaka uwe na vielelezo vingi barua ya mwaliko ,copy ya passport ya anaekualika,,sijui niniiii
Ina hawawezi kukupa passport tu mpaka yote hayo,,au sio haki ya mtanzania kupata pass?

Ombi lako ndio linalopelekea viambato gani vinahitajika, mfano; Umealikwa na ndugu yako yupo Marekani kama ni raia wa Tanzania basi aandike barua ya mwaliko, nakala ya pasipoti yake na Residency permit inayomuweka Marekani, kama ni Mmarekani basi barua ya mwaliko, pasipoti yake na kitambulisho cha kazi.

Kingine ni kuwa, pasipoti sio sawa na leseni ya udereva, Inahitaji docs za kutosha ili kujiridhisha kuwa anayepewa pasipoti ni raia wa Tanzania. Ukikurupuka kutoa pasipoti kumbe mtu sio raia basi utakuwa umempa uraia kwa elfu 50 badala ya US$5000.

Kumbuka, Hakuna Pasipoti bila Dhamira (kusudi) ya Safari
 
What is considered a valid form of ID?What are considered valid forms of ID? ... ( Social Security Card, from the USA Social Security Administration, with your signature AND Photo Identification with your signature ie: unexpired driver's license, government issued identification card, military identification or passport).
Angalia mnawaiga kuvaa milegeezo na kutoboa masikio lakini ya maana mnayaacha.

Hii ni Tanzania na hio ni Marekani, ushoga kwao halali kwetu haramu. Uganda Konyagi Mwitu aka Gongo ni halali Tanzania ni jinai. Kwahiyo usitupangie.

Pasipoti inatengenezwa kwa gharama kubwa na ina security features kibao, zenye kuonekana kwa macho (watermark) na zilizofichwa (UV-Light) zenye kuonekana kwa mionzi ya UV.
Kwa Tanzania labda ukienda nchi za wastaarabu passport driving licence vinatumika kama vitambulisho. Halafu ikitokea leo mgonjwa na unatakiwa kupelekwa nje kwa matibabu huoni kama kuwa na passport mkononi kutakusaidia badala ya kuanza process chovu kuipata?. Passport ni kama leseni ya gari mbona watu wanapewa bila kuwa na gari.

Mawazo kama watu kama ninyi yanafanya mambo madogo kama haya na haki za watu yawe magumu. Nikihitaji passport siyo kazi ya serikali kujua lini nitasafiri hii ni karne ya 21 kila mtu ana haki ya kuwa nayo mradi tu ni raia halalif.
an official document issued by a government, certifying the holder's identity and citizenship and entitling them to travel under its protection to and from foreign countries. Hii ni maana ya passport inathibitisha utambulisho na uraia wa mmiliki. Ndiyo maana ni moja ya vitambulisho muhimu
Ni kwa mtazamo wako ila kanuni na sheria ya Passport & Travel Documents Act ya Mwaka 2007 inasema pasipoti ni kwa raia mwenye dhamira ya kwenda nje ya nchi.

Pitia hapa pia pia wanasema "An ordinary passport may be issued to any citizen of the United Republic of Tanzania for the purpose of travelling outside the United Republic of Tanzania" kwenye nyekundu hapo ndio lengo kuu la kupewa pasipoti, otherwise endelea kulalamika tu.

Passports and Travel Documents
 
Kijana naomba uwe makini na taarifa unayotoa kuhusu UHAMIAJI.

Uhamiaji sio idara ya kufanya mambo kwa kukurupuka. wanafanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu.

Kwanza umesema umepoteza? hapo kuna changamoto na lazima uchunguzi ufanyike wa kina tofauti na hapo wao wanaweza kuwa hatiani.

Je utajuaje pasi yako inatumiwa na mtu mwingine kimakosa?

Na ddiyo maana sheria inasema untakiwa utangaze kwenye gazeti ya serikali ukiwa na RB, kisha ukae mda sio chini ya miezi 3 au 6 kubaini pengine imeokotwa.

Baada ya hapo utaandika Barua kwa mkono wako kwa kuomba Mkurugenzi wa Uhamiaji namna pasi yako ilivyopoatea na hatua ulizochukua pia pasipo kusahau kueleza sababu ya kuomba ya pili?

Kisha uwape uhamiaji mda wa kufanya uchunguzi wao wa kina.

Hivyo basi nikusihi uwe mvumilivu usipende kusema kuna Rushwa labda wewe ndio uhojiwe kwa nini utake kutoa rushwa, pengine unajua pasi yako ilipo.

Akhsante.
Majibu maridhawa yenye weledi ndani yake....safi.
 
Bora hii mada inayojadiliwa inekuwa hivi- KWA NINI NSSF HAWATOI MAFAO YA WATU WALIOFUKUZWA KAZI BILA YA WAO KUJIFUKUZISHA KAZI KWA KUANDIKA BARUA YA KUOMBA KAZI.

je hamjaona wengi wanavyoteseka NSSF kudai hela ambazo ndio haki yao utafikiri walizikopesha?
Hiyo ungeifungulia thread yake ingependeza....ila kutaka hii isiwepo ili iwepo hiyo yako humu ni vurugu kama vurugu zingine.
 
Nilimsikia waziri ingawa simkumbuki ni wa wizara gani akikemea passport kutumika kama kitambulisho ndani ya nchi,kuhusu kusafiri nje ya nchi yes nimeshasafiri mara mbili
Ndiyo kina Nkamia hao mkuu. Kuna wenye matatizo. Hivi ukienda Kenya kuthibitisha wewe ni nani utaonyesha nini? Passport ni moja ya form of ID. Inakubalika popote pale duniani. Pia Driving licence ni kitambulisho pia.
 
Hujanielewa mkuu..mm nilimaanisha kwamba ndani ya Tanzania hutakiwi kutumua passport kama kitambulisho,na siyo nje ya Tanzania.
 
Hii ni Tanzania na hio ni Marekani, ushoga kwao halali kwetu haramu. Uganda Konyagi Mwitu aka Gongo ni halali Tanzania ni jinai. Kwahiyo usitupangie.

Pasipoti inatengenezwa kwa gharama kubwa na ina security features kibao, zenye kuonekana kwa macho (watermark) na zilizofichwa (UV-Light) zenye kuonekana kwa mionzi ya UV.

Ni kwa mtazamo wako ila kanuni na sheria ya Passport & Travel Documents Act ya Mwaka 2007 inasema pasipoti ni kwa raia mwenye dhamira ya kwenda nje ya nchi.

Pitia hapa pia pia wanasema "An ordinary passport may be issued to any citizen of the United Republic of Tanzania for the purpose of travelling outside the United Republic of Tanzania" kwenye nyekundu hapo ndio lengo kuu la kupewa pasipoti, otherwise endelea kulalamika tu.

Passports and Travel Documents
Mimi niliuliza kwanini Tanzania passport siyo haki ya msingi wewe ukasema passport siyo kitambulisho. Ninajua kabisa kuhusu hiyo sheria iliyopitwa na wakati ila wewe hukujua namna ya kuijibu hoja yangu. Maana kila nchi niliyoenda nimetumia passport yangu kama kitambulisho na ndilo swali langu ambalo labda hukulielewa ukaamua kulijibu juu juu

SOMA HAPA CHINI NIAMBIE WAPI NILIPOSEMA HICHO ULICHONIJIBU.

Ni kweli rushwa ipo sana, nilishuhudia mama mmoja tarehe 12 February akihitaji passport ya kwenda matibabu nje alizungushwa sana mara aambiwe apeleke vielelezo mara vitambulisho, tukamshauri aombe kuonana na Mkurugenzi wa Uhamiaji, baada ya wale wahudumu kugundua kuwa yule mama yupo kwenye hiyo process ya kwenda kwa Mkurugenzi, wakampa pass in less than one hour kitu kilichoashiria kuwa walikuwa wameprint tayari isipokuwa hawakutaka kumpa, mwingine alikuwa anasafiriri kwenda Nordic countries, tena huyu alikuwa anarenew naye wakamwambia ataiapta kesho yake, alipokwenda kwa boss wao akaambiwa asubiri passport apewe siku hiyohoyo na akapewa.

Mchezo wa rushwa unachezwa na wale maofisa waliopo kwenye yale madirisha siyo viongozi, nilichojifunza ni kuwa ukipata nafasi ya kuonana na viongozi ukawaambia shida yako wakakuelewa basi hutoi hata senti moja
Click to expand...

HHILI LILIKUA JIBU LA HUYU JUU NDILO ULILOLIKURUPUKIA NJIANI BILA KUUJUA MWANZO WAKE.

Kwanini Tanzania suala la passport linakua kero sana? Mimi nilidhani passport ni haki yangu na pia ni njia rahisi ya kutumika kama kitambulisho. Kuwa na passport si lazima nisafiri. Sijui lini hii idara itskua na watu wrnye weledi kuiboresha same kwa jeshi la polisi. Pale jeshi litakapotambua kuwa wao si maagent wa serikali na chama tawala bali wapo kwaajili kulinda usalama ws kila mtanzania na mtu yeyote aliyepo nchini awe kihalali ama kimagumashi. Haki inatakiwa kutendwa kwa yeyote yule
 
Hujanielewa mkuu..mm nilimaanisha kwamba ndani ya Tanzania hutakiwi kutumua passport kama kitambulisho,na siyo nje ya Tanzania.
JF-Expert Member
#60
A moment ago

New

Wewe hukunielewa mimi sababu umejibu bila kuangalia chanzo. Mimi niliuliza kwanini kuna mizengwe mingi kupata passport wakati ni haki ya mtu. Maana wengine wakanijibu hutakiwi kuwa nayo kama huna safari.

NHii ndiyo message yangu ya kwanza.

Kwanini Tanzania suala la passport linakua kero sana? Mimi nilidhani passport ni haki yangu na pia ni njia rahisi ya kutumika kama kitambulisho. Kuwa na passport si lazima nisafiri. Sijui lini hii idara itskua na watu wrnye weledi kuiboresha same kwa jeshi la polisi. Pale jeshi litakapotambua kuwa wao si maagent wa serikali na chama tawala bali wapo kwaajili kulinda usalama ws kila mtanzania na mtu yeyote aliyepo nchini awe kihalali ama kimagumashi. Haki inatakiwa kutendwa kwa yeyote yule
 
Mimi niliuliza kwanini Tanzania passport siyo haki ya msingi wewe ukasema passport siyo kitambulisho. Ninajua kabisa kuhusu hiyo sheria iliyopitwa na wakati ila wewe hukujua namna ya kuijibu hoja yangu. Maana kila nchi niliyoenda nimetumia passport yangu kama kitambulisho na ndilo swali langu ambalo labda hukulielewa ukaamua kulijibu juu juu

Kwanini Tanzania suala la passport linakua kero sana? Mimi nilidhani passport ni haki yangu na pia ni njia rahisi ya kutumika kama kitambulisho. Kuwa na passport si lazima nisafiri. Sijui lini hii idara itskua na watu wrnye weledi kuiboresha same kwa jeshi la polisi. Pale jeshi litakapotambua kuwa wao si maagent wa serikali na chama tawala bali wapo kwaajili kulinda usalama ws kila mtanzania na mtu yeyote aliyepo nchini awe kihalali ama kimagumashi. Haki inatakiwa kutendwa kwa yeyote yule

Mkuu naona hata ww hujaelewa nimekujibu kitu gani, nilichokujibu ni HAKI ya kupata Pasipoti na Pasipoti kutumika kama kitambulisho ukiwa ndani ya Tanzania. Sasa kama unaona nimekurupuka, ni mtazamo wako.

Watu kama wewe wakifika Uhamiaji na kueleza dhamira yao kuwa "nataka tu niwe na pasipoti ila sina safari kwa sasa labda ikitokea zali" huwa mnanyimwa na kuanza kulialia baadaye ndio mnatengeneza mazingira ya rushwa. Ukiwa umekamilisha kila kitu na viambato vya dhamira viko sawa huwezi kuhonga wala kusumbuliwa.
 
Back
Top Bottom