Uhamiaji: Wallace Karia ni Mtanzania

Uhamiaji: Wallace Karia ni Mtanzania

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096


Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika August 12 mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi habari makao makuu ya Idara hiyo, Msemaji Mkuu wa Uhamiaji, Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake Wallace Karia kuwa si raia wa Tanzania hali ambayo inafanya akose sifa ya kuwa mgombea wa kiti hicho.

"Wallace Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357(Rejeo la 2002) na kanuni zake, wakati huo huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi".

Mtanga amesisitiza utambuzi wa uraia upo kisheria sura ya 357 (rejeo la 2002} uraia hauangaliwi Rangi, kabila wala dini.

Idara hiyo imevitaka vilabu vyote na taasisi za michezo kuhakikisha wafanyakazi wote na wachezaji ambao raia wa kigeni wanatimiza taratibu zote za kisheria za kukaa nchini bila kufanya hivyo sheria itashika mkondo wake .
 
FB_IMG_1501824264007.jpg
Idara ya Uhamiaji imesema Makamu rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tnzania, (TFF) , WALES KARIA ni raia halali wa Tanzania. WALES alifanyiwa figisufigisu na wagombea wenzake kuwa siyo rais baada ya kuonekana kuwa tishio kwenye uchaguzi wa kumpata rais mpya wa kuiongoza TFF unaotarajia kufanyika jumamosi ijayo

Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema , Wales Karia ndiye mwenye uwezo wa kuiongoza TFF kwa sasa ukilinganisha na wagombea wengine. KARIA anaelezewa kuwa mtu anayependa kufanyakazi kwa kushirikisha viongozi wenzake, siyo mla rushwa na ni mpiganiaji mzuri wa haki za viongozi na wachezaji. Walio karibu na TFF wanasema KARIA Wakati akiwa chini ya Jamal Malinzi alikuwa ànaibua mbinu mbalimbali za namna ya kuinua kiwango cha Soka nchini lakini Bosi wake (JMAL MALINZI) akawa anatumia ubunifu wake kujipatia pesa kwa ajili ya mambo yake binafsi.
Wagombea wengine katika nafasi hiyo ya rais wa TFF ni pamoja na Imani Mdega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayai Tembele, Shija Richard na Emmanuel Kimbe
 
Hilo nilo nilijua siku nyingi watagonga ukuta tu kwa sisi tuliobahatika kuishi kunani palee tunamfahamu huyo ni hana tatizo la uraia hata rage anamfahamu!
 
Kumbe nini kwani utasomaje bila cheti cha kuzaliwa we vepeeeeee? !
Nilidhani nawasiliana na mtu mzima kumbe mtoto anaeleta jokes...huyo jamaa amezaliwa kitambo namna hiyo na kigezo cha kuingia shuleni ilikuwa ni kushika sikio la kushoto kwa mkono wa kulia unaupitishia kichwani...hayo mambo ya vyeti ya kuzaliwa yameanza kwa kizazi kilichozaliwa 1987 yaani walioanza shule ya msingi miaka ya 90 tena mwishoni kabisa au 2000 kabisa na wengine wamekutana na issue ya vyeti chuo
 
Huu ushenzi ulioanza siku za karibuni za kusingizia watu sio raia, hii nchi yetu haina watu wa kusema ndio original wa hapa karibu makabila yote ni wa kuja tu..ina maana akitokea mwarabu wa shinyanga, tabora au singida akataka kuongoza hoja ya sio raia italetwa.? Huko Tanga haswa Muheza kuna watanzania wenye asili ya Somalia wa kumwaga na somalia hawajahi kanyaga wala kuishi.hii nchi ni yetu wote ..mie nilijua tu huyu jamaa ni mbongo ila fitna tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa kwa hii kauli yake ya kuchanganya mambo ya siasa kwenye mpira, amesababisha watanzania wapenda soka na tusiofungamana na chama chochote kile cha siasa tumuone ni kilaza wa mwisho na mtu mwenye akili ndogo sana aliyekabidhiwa majukumu makubwa asiyostahili.

Binafsi, nimemdharau sana! Mfano wake wa kumlinganisha hasimu wake Michael Wambura na mh.Tundu Lissu ulikua totally irrelevant! Siasa na mpira wapi na wapi! Alitakiwa afiche ujinga/mahaba yake maana anafahamika fika ni kada wa chama tawala.
 
Back
Top Bottom