Mtu kazaliwa Tanzania 🇹🇿 halafu leo unataka kumwita Mmarekani kwasababu ya kibali. Watanzania ni wajinga sana wakati mwingine utu wa mtu sio makaratasi yake. Kila Mtanzania anajijua popole alipo mimi nimekaa US miaka 20 lakini mpaka leo wanasema mimi ni Mtanzania hakuna mtu anaweza kunitaja bila kuhusisha na Utanzania wangu maana Utanzania ni utu sio makaratasi siku hizi ndiyo watu wanataka kubadilisha Utanzania kuwa vitabu na vibali.
Mtu kazaliwa Tanzania ni Mtanzania awe na passport ni mambo ya sheria tu na yanabadilika kila siku lakini Manji ni Mtanzania na hakuna binadamu anaweza kubadilisha hilo passsport unapewa na watu lakini utaifa unapewa na Mungu.
Hapana.
Wewe huwa ninakupinga sana juu ya hili, na unaelewa kwa nini, kwa sababu ya historia yako.
Sasa kuwa mTanzania kuishie kwenye utu?
Hakuna anayetumia uTanzania kwa fursa tu, bila hata ya kuujali huo uTanzania wa makaratasi?
UTanzania ni zaidi ya kuwa na makaratasi, ambayo wakati wowote mtu anaweza kuyatupilia mbali na hata kulihujumu taifa lake hilo la makaratasi, huo ndio tuuite utu?
Kuvaa uraia wa nchi kama nguo inayovuliwa wakati wowote, huo siyo uraia.
Inafahamika, sasa hivi watu wanachukua, si uraia wa nchi moja, mbili au hata tatu, mradi tu wafanye mambo yao.
Lakini naomba nirudi nyuma kwenye andiko lako, hasa hapo unapozungumzia uraia wa kuzaliwa.
Ndiyo, inafahamika kuna baadhi ya kundi hili wanaoweza kulisaliti taifa lao la kuzaliwa kwa maslahi yao binafsi au hata ya nchi yao mpya, lakini kawaida ya wengi ni kwamba nchi ya kuzaliwa mara nyingi ndiyo huwa inachukua nafasi kubwa zaidi bila kujali uraia wa nchi nyingine ya kujiandikisha kwa ajili ya maslahi.
Kwa mfano, itakuwa ni vigumu sana kwa mtu aliyezaliwa Tanzania, halafu ahamie na kuchukuwa uraia wa Kenya. Mtu huyu, mara nyingi itakuwa vigumu kwake kuondoa uTanzania ndani yake. Hali ni hivyo hivyo na kwa mtu toka Kenya aje achukue uraia Tanzania, ukenya wake huwezi ukauondoa.
Nimalizie kwa kusema kuweka msemo huu maarufu wa viongozi wetu wa zama hizi:
Wakati huu tulionao sasa hivi ni kutekeleza ile dhana mashuhuri ya
"Kula na wewe ukubali Kuliwa" Hii ndiyo phylosophy inayotawala kwa sasa hivi. Sahau yote ya
"Uraia na Utu"
You ain't seen nothing yet!