Uhamiaji marekani ndo basi tena?

Wale wenzangu na Mimi wa kutafuta green card ndo bas tena baada ya Trump kushinda
Hapana mkuu njia halali ya kwenda Marekani bado ipo na itakuwa wazi.

Wakati wa utawala wa Trump (2016-2020) nilikwenda States mara kadhaa na ni kweli wale maofisa uhamiaji walikuwa "hostile" kwa wageni khasa weusi.

Lakini ukiwa uko sawa hakuna shida kwani hata sasa waweza kuingia na GC yako bila shida ukumbuke tu kuirekebisha kama yakaribia kuisha muda wake (hutakiwi kuwa nje ya Marekani kwa zaidi ya mwaka mmoja).

Trump shida yake amesema wazi ni wahamiaji waso na vibali halali vya ukaazi.

Na amesema atamalizia ule ukuta mrefu kuzuia uingiaji haau nchini humo.
 
Kama namuona RomaMkatoliki na mabegi yake pale Airport Dsm
 
Green card - permanent resident ID, ni kadi inayotolewa kwa watu walioingia kihalali kuja kuishi na kufanya kazi na hatimaye watakaoqualify kuwa raia ndani ya miaka mitano.

Trump yupo busy na illegal immigrants - yani wanaovuka mipaka bila documentation zozote na hasa wa jirani hapa America ya kati, Mexico na ya kusini. So ni nadra sana mtu kama anatoka Africa apite njia yote ndefu hiyo na ya gharama kubwa kuja kuzamia hapa.

Wabongo wanaosema wanawasubiri wenzao warudishwe ni kama ile tu ya malaika alivosema anatamani watu waishi kama mashetani. So sioni kama kuna mtanzania atarudishwa labda waliokuja kwa njia ya shule na wakashindwa kuchange status zao kabisa!
 
Wale wenzangu na Mimi wa kutafuta green card ndo bas tena baada ya Trump kushinda

Hakuna nchi ambayo inakataa raia wa nchi nyingine ,wanachozungumzia ni wahamiaja haramu(illegal immigrants)z,Trump hawezi kuzuia raia wa nchi nyingine wasiingie marekani maana kuna wafanyabiashara wa india ,nigeria ,kuna wawekezaji pia kutoka nchi nyingine ,kuna waislaeri huko etc
 
Wale wenzangu na Mimi wa kutafuta green card ndo bas tena baada ya Trump kushinda
Anachopinga trump ni uhamiaji holela, yani ilifika muda wewe unachotakiwa kufanya ni kufika mexico tu, then unaanza kuitafuta border ushafika. Hili ndo tatizo kuu. Sio wahamiaji waliofata taratibu zilizowekwa kufika huko.

Mambo mengi tu watu wanatafsiri wanavoona wao
 
Hakuna nchi ambayo inakataa raia wa nchi nyingine ,wanachozungumzia ni wahamiaja haramu(illegal immigrants)z,Trump hawezi kuzuia raia wa nchi nyingine wasiingie marekani maana kuna wafanyabiashara wa india ,nigeria ,kuna wawekezaji pia kutoka nchi nyingine ,kuna waislaeri huko etc
Naam hili nililishangaa siku moja crown fm walimualika profesa gani sjui yupo huko karudi likizo, akamponda sana trump kwamba ata yeye hamtaki kitu nilikua naona mbona hii si kweli ntaattach link

Nusu saa la kwanza
View: https://www.youtube.com/live/QpWKxhb-bbs?si=Wy-k12TjxQAZG00P
 
Kwanini watu hasa wa Afrika wana mentality za kumbilia Ulaya ama Marekani badala ya kupambana kurekebisha hali za maisha nchini mwao? Europe is for Europeans and Amerca is for Americans haukuzaliwa hapo ulipo kwa bahati mbaya pambana kubadilisha hali kwa namna yoyote ile sio kukimbia kimbia kwa watu na kwenda kuishi kama mtumwa.
 
Unaweza ukawa upo sahihi Mkuu ila kumbuka kua,hata huko Ulaya na Marekani,nchi zao hazikujengwa na wao wenyewe tu,walichukua watumwa na kwenda kuwatumikisha,au unafikiri hawa Black Americans wametoka wapi na kujikuta wapo huko?
 
Back
Top Bottom