Utafiti mdogo sana Entry Point zote ambazo ni class A na B hakuna Mtu ama mfanya kazi ambaye hana mahusiano na wanao julikana Makamishana wa uhamiaji,Ama ni watoto wao au ndugu zao.Tazama KIA,Namanga,Tunduma,Kasumulo,ZIA,Sirali,Mtukula na mikoa yote ambayo ni active kwa shughuli za Kiuhamiaji lazima kutakuwa na watoto wao ama wandugu zao,Sasa kuna nini huko kama hakuna uharifu unafanyika wa ubadhilifu ndio maaana kila mwenye mtoto ama jamaa hupendelea wakafanye kazi vituo hivyo,Kuna Mikoa kama Singida,Tabora,Mtwara,Rukwa,Ruvuma,Dodoma hii imetengwa kama Mikoa ya adhabu kwa Maafisa uhamiaji pindi wanapo haribu kwenye mikoa mingine,Mfano Maafisa Uhamiaji walio hamishwa Mkoani Arusha mwishoni mwa mwaka jana kwa tuhuma za kutoa vibari feki wote 16 wamesambazwa mikoa ya kusini,Sidhani kama ndio ufumbuzi wa tatizo.Kwa mtazamo wangu nadhani kunatatizo la mfumo hasa ajira na aina ya watu wanaoajiriwa na Idara hii nyeti kwa mustakbali wa Taifa hili.Bilakuwepo juhudi ya ziada kuitazama upya Idara hii kuna hatari ya kuwepo raia wengi wakigeni ambao hawana tija kwa Taifa na kupelekea machafuko ya siyo yalazima kwa kuendekeza Rushwa na kuwalinda watoto ama ndugu zao walio wajaza sehemu zote nyeti ambazo ndio hupatikana makusanyo makubwa kupitia malipo ya Visa ha hati zingine ambazo nyingi hulipwa kwa Dolla.(Tafakali chukua hatua tunaangamia)