Uhalisia wa Fursa (Opportunities)

Sci-Fi

Member
Jan 30, 2016
71
266
Salam wakuu.

Moja ya watu ninaoa farijika sana kuishi nao katika zama hizi na kushare nao hili anga na hii Oxygen ya bure kutoka kwa Muumba ni huyu Mr Elon Musk. Shule ni kitu muhimu sana endapo inachangia positive katika either kukufanya uwe bora katika jamii kwa kutatua baadhi ya changamoto ambazo yamkini usingali kwenda shule ingelikua vigumu kuzitatua.

Huyu jamaa kazaliwa June 28th, 1971 hapa hapa Africa kwa Mzee Mandela hapo, South Africa. Mwaka 1988 akiwa na miaka 17, Musk alihamia Canada ambako alifanikiwa kupiga undergraduate and he earned a degree in Physics and Business kutoka Chuo kikuu cha Pennsylvania. Mwaka 1995 huyu jamaa aliamua kudrop Chuo Kikuu cha Stanford ili aingie mtaani kuanzisha kampuni yake ya kwanza.

Moja ya vitu vilivyo nifanya nikaamua kumfungulia huu uzi ni pamoja na jinsi alivyo/anavyo zifanya FURSA 'CHANGAMOTO' mbali mbali alizo kutana nazo na zile zinazoikabili dunia.

Elon Musk alihitaji njia mpya itakayo muwezesha kufanya payments kwa wepesi online (kwenye mtandao wa internet). Jamaa huyu akaona isiwe shida, akatumia Elimu yake ya Fizikia kudesign mfumo mpya ambao mpaka sasa tuna utumia kufanya malipo na hata kupokea pesa kwa jina PayPal. Ingawa huu mfumo wake ulikuja boreshwa zaidi na vijana wa Kiisrael kutoka katika kampuni ya 'Fraud Science'. Kampuni hii pia ilikuja nunuliwa na PayPal kwa pesa ndefu sana hapo baadae.
ATTACH]

Elon Musk alihitaji kuendesha gari za umeme. Nadhani alichoshwa na hizi issue za Waarabu kupandisha bei ya mafuta wanapojiskia. Jamaa akaona isiwe tabu, 'I can design whatever the f**k I want'. Akaanzisha kampuni kwa jina Tesla Motors. Hii company lengo lake ni supply gari za kuchaji ka simu au niseme gari zinazotumia umeme, 'Electric Cars'. Nimebahatika kupanda na kuendesha hizi gari. Tulikua tunapigia mzigo asubuhi hadi jioni, usiku gari tunailaza kwenye umeme. Kesho kazini kama kawa. Ila nadhani kwa umeme wa Tanesco Tz tutasubiri sana.
ATTACH]

Elon Musk anahitaji kwenda kwenye Space kwa haraka na gharama nafuu. Akaamua kuja na SpaceX. Hii ni basically a Space Exploraring Company. Moja ya vitu vitakavyo pelekea pia mawasiliano ya Simu na matumizi ya data yawe kwa gharama nafuu kabisa ni pamoja na yatakayokuja mafanikio ya SpaceX chini ya Elon Musk.

Huyu jamaa pia, alihitaji usafiri wa haraka zaidi. Basi akamua kuja na Hyperloop. Hizi kitu unaambiwa speed yake ni kubwa mno.

Inakadiriwa kuwa hizi hyperloop train zitakua na uwezo wa kusafiri kwa only 30mins kutoka Los Angeles to San Francisco. Distance from Los Angeles to San Francisco.
ATTACH]

Distance from Los Angeles to San Francisco is 559 kilometers. This air travel distance is equal to 347 miles. Hapa kwa ndege ya moja kwa moja (non - stop) muda wa kawaida huwa ni saa moja na Dakika 30, kwa maana hiyo train za Bwana Elon Musk zitakua zimesave saa moja kwenye usafiri.

ATTACH]

Hapa Duniani kila mmoja kaletwa kwa kusudi maalum. Na yamkini 'changamoto' unayopitia ndio mlango wako wa kutokea endapo utaamua kuifanya 'fursa'. Ieleweke kuwa, kila mmoja anayo njia bora zaidi ya kutatua changamoto inayo mkabili. Elon Musk anaamini katika kufikria jambo flani linalo kutatiza mpaka ulipatie jibu. Si lazima majibu yatoke kwako, ila you must act kwa kile kinachokusumbua.

Elon Alipoacha na PayPal alikua na mtaji wa almost $180M. Ili kutimiza malengo yake na kuyapatia majibu matatizo mbali mbali aliyohitaji kusolve, Elon Musk aliwekeza $100M kwenye Mradi wake wa SpaceX, $70M kwenye mradi wa Tesla Motors na $10M kwenye SolarCity. Halafu akafulia, pesa ya pango akenda kukopa.

Hitimisho.

Kitu cha pekee kabisa nilichotaka tujifunze hapa ni kwamba, Elon Musk hakua na muda kawaelezea watu how bad the world is, ila alikua na yuko busy katika kuifanya dunia iwe better place kwa kuanza na alicho nacho, 'shida zake'. Kila mmoja ana package yake kwa ajili ya huu ulimwengu that's why uumbaji wake ulikua muhimu. Yaani kuna kitu I believe Mungu aliona kina kosekana Duniani that's why akaamua kukuleta na kila mmoja yuko full equipped ili ku_manifest why s/he is here.
ATTACH]

Tusiache kuzisoma alama za nyakati na kutumia changamoto zinazotukabili kama fursa. Naamini kuna mengi sana hayajafanyika.

(Mods naomba msibadili chochote kwenye uzi huu)
 
Attachments

  • b3db176652007efc3d5578ebab0acda1.jpg
    b3db176652007efc3d5578ebab0acda1.jpg
    15.6 KB · Views: 24
  • dfa559fc092edb401197fe0714044de8.jpg
    dfa559fc092edb401197fe0714044de8.jpg
    42.5 KB · Views: 20
  • e0062625f396a5c96554ae661a001e86.jpg
    e0062625f396a5c96554ae661a001e86.jpg
    24 KB · Views: 22
Vipaji ni Mali. Tanzania kipaji ni mwanzo wa misukosuko yako na vyombo vya dola, rejea aliyetengeneza helikopta Tunduma
Kuna watu hua wamebarikiwa sanaa kila wanachogusa imooooo!!!! Ila kuna kina sisi sasa mpaka ufeli mara 50 kwanza hhahhaa
 
Kama Tanzania ingekuwa na inawaendeleza watu wenye vipaji tungekuwa mbali sana, rejea jamaa wa Tunduma aliyetengeneza helicopter, kuna wanatengeneza magobole na mabomu mwisho wa siku huishia kufungwa badala ya kuwachukua na kuwapeleka kwenye karakana za keshi wakatapewa vifaa watengeze silaha na mabomu ya kisasa.

Mara nyingi wazungu wakijua kuna mtu kutoka Africa kafanya maajabu ya tekenolijia wanamchukua na kumpeleka kwao mwisho wa siku tunauziwa bidhaa zilizotengenezwa na Mwenyezi aliyechukuliwa na wazungu.

Kuna rafiki yangu aliwahi kutengeneza kijenereta kidogo kinatumia maji, kilikuwa na uwezo wa kuwasha taa ndogo za pikipiki au gari lakini leo hii ni fundi simu.

Tanzania kuna watu wenye vipaji amabo wakiwezeshwa tutafika mbali na Tz yetu ya VIWANDA.

NAKUPENDA TANZANIA.
 
Hii ishu ya mtu kutengeneza kitu fulani alaf watu kutaka kitumike kiholela holela sio sawa. Kila kitu kina utaratibu, hata ulaya ugunduzi ukifanyika hauendelezwi kiholela holela tu eti kisa ni ugunduzi, kuna sheria na taratibu za kufuata ili kuendeleza ugunduzi huo. Vitu hivyo vina effect kwenye maisha ya binadam kwaiyo lazima vikidhi standards fulani, mfano huyo alietengeneza sijui ndege, angeachwa hiv hiv leo hii angeanza kupakia watu kwenye chombo hicho ambacho pengine hakijakidhi standards za safety, huyo wa generator nae siku ilo generator lake likileta madhara hiyo hiyo serekali ingelaumiwa.sikatai ugunduzi, ila kuna mamlaka na taratibu za kufuata kuendeleza ugunduzi sio kufanya vitu kienyeji.
 
Naona kama hujanielewa,
Hao wagunduzi inabidi waendelezwe siyo kuwaacha mfano aliyetengeneza ndege na jenereta inabidi serikali iwachukue au kuwaletea watu waliobobea kwenye mambo kama yako ili wapate vitu vingi na mwisho wa siku watengeneze kitu kikaguliwe then kitumike.
 
kama COSTECH inashughulika na tafiti za TWAWEZA basi tuna safari ndefu sana.
 
naunga hoja, mimi nafikiri kungekuwepo na NGO'S za uwakala wa vipaji kutoka Afrika kwenda ulaya, amerika na kwingineko ili akipatikana mwenye kipaji anapelekwa huko kwa mafunzo zaidi yenye faida kubwa.

Akifanikiwa katika ugunduzi wake asirudi tena kuishi huku maana watamlazimisha kuwa mwanasiasa halafu wamuharibu akili na kupoteza uwezo wake,

Afrika bado sana.
 
Hii ishu ya mtu kutengeneza kitu fulani alaf watu kutaka kitumike kiholela holela sio sawa. Kila kitu kina utaratibu, hata ulaya ugunduzi ukifanyika hauendelezwi kiholela holela tu eti kisa ni ugunduzi, kuna sheria na taratibu za kufuata ili kuendeleza ugunduzi huo. Vitu hivyo vina effect kwenye maisha ya binadam kwaiyo lazima vikidhi standards fulani, mfano huyo alietengeneza sijui ndege, angeachwa hiv hiv leo hii angeanza kupakia watu kwenye chombo hicho ambacho pengine hakijakidhi standards za safety, huyo wa generator nae siku ilo generator lake likileta madhara hiyo hiyo serekali ingelaumiwa.sikatai ugunduzi, ila kuna mamlaka na taratibu za kufuata kuendeleza ugunduzi sio kufanya vitu kienyeji.
Shida moja wapo ya ofisi nyingi tendaji za serikali wanafanya kazi kumfurahisha mtu na sio kwa manufaa ya umma. Watu badala ya kusupport jitihada binafsi za watz wao wako tayari kuzima jitihada hizo kisa hawaelewi kilichogundukiwa au wanadhani kinaweza kuwa na madhanara.

Nadhani hakuna ugunduzi hatari zaidi kutokea duniani kama ugunduzi wa silaha za moto, like Nuclear weapons, lakini kwakua waliogundua serikali zao ziliwapa support ndio maana leo tunazo Mother of all Bombs.

Kuna raia mmoja wa Israel anaitwa Aggasi, huyu alikuja na idea ya kutengeneza hizi hizi gari za Umeme 2006 kabla kabisa ya Elon Musk. Kwakua alihitaji support ya serikali yake, alikua kumshirikisha Raisi wa kipindi kile bwana Shimon Peres. Huyu mzee anasema japokua alikua haelewi how things will workout, ila alimua serikali yake i take risk into the unknown kumsupport huyu jamaa, Aggasi. Wanasema, "If not for Peres, even Aggasi might not dared to pursue his own idea" Peres alikubali kuwa embarrassed mahali flani kisa kutetea idea ya kijana wa taifa lake which after a lot of hustling Israel was the first country kudevelop hizi electric cars ndo kina Elon Musk wakafuata.

Hatuhitaji siasa kwenye kukuza vipaji vya watz, ila tunahitaji mazingira rafiki, na serikali iliyo tayari kusaidia initiatives za raia wake hasa kwenye nyanja hii ya technology. Waliopewa majukumu ya kuendeleza hizi gunduzi za watz wafanye kazi kwa manufaa ya nchi bila kutafuta credits na waweke wazi utaratibu gani ufuatwe ili kurasimisha gunduzi hizi za wazawa na sio kuja na matamko tu kwenye TV's.

Wote wanao gundua vitu flani hapa tz ni kwakua walipata shida mahali na katika kutafuta solution ndio wakafikia wanapokua wamefikia so juhudi zao ziheshimiwe coz hizo gunduzi ndio zaweza kuwa chanzo (Fursa pekee) za wao kujitoa kimeisha.
 
Back
Top Bottom