Uhalifu wa chuki za kisiasa waongezeka Nchini Ujerumani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Takwimu rasmi kuhusu uhalifu unaotokana na siasa nchini Ujerumani zinaonesha kuwa ghasia na uhalifu wa kibaguzi vimeongezeka nchini humu. Waziri wa Mambo ya ndani wa Ujerumani. Horst Seehofer leo amewasilisha takwimu za uhalifu uliotokana na siasa uliofanyika mwaka 2020.

Seehofer ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa matukio ya uhalifu yanayochochewa kisiasa, hasa yale yanayofanywa na watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia, kama vile mauaji ya vijana 11 wenye asili ya uhamiaji kwenye mji wa Hanau Februari mwaka uliopita.

Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Ujerumani amesema uhalifu unaochochewa kisiasa uliongezeka kwa kasi na kwamba asilimia 8.5 ya visa vinavyotokana na uhalifu huo vilirekodiwa mwaka 2020 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Aidha, Seehofer amesema ongezeko la asilimia 11 la uhalifu ulifanywa na wafuasi wenye siasa kali za mrengo wa kushoto.
 
Back
Top Bottom