Biashara ya ukahaba ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo, like it or not, legal or illegal- its there to stay! Asilimia kubwa ya wanaokamatwa katika kupiga vita hii biashara ni makahaba wenyewe lakini 'wateja' na 'mapimps' amabao ndio wadau wakubwa kwenye hii biashara wanaendelea kupeta tu. Isitoshe kuna wanawake hii ndio njia pekee ya kujipatia kipato chao na hawafanyi hivyo kwa kuwa wanapenda, ni kwa kuwa tu hawana namna nyingine ya kujiingizia kipato!
Hebu mfikirie mwanadada mdogo hapo bongo aliyepata mimba na kuzaa baada ya kubakwa na baba yake wa kambo, as a result she had to flee home kwa kuwa mama yake alikuwa hamuelewi na anaamini kile anachoambiwa na mumuwe, hana msaada wowote toka serekalini au kwa ndugu au marafiki, ukahaba ndio njia pekee inayomuwezesha kumlea mtoto wake. Wakati akijiuza huko mtaani kuna anakuatana kila aina ya abuse and harassment kwa wateja na hata wale wasiokuwa wateja! Kuna wanaompiga, kuna wanaomtukana, kuna 'wanaomchapa' na kukimbia, kuna wanaomlazimisha wapige kavukavu, wengine wanataka tigo, etc. Kajikuta ameingia katika matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na kazi na mazingira ambayo anafanya kazi yake. Surely someone out there somehow can do something to protect this girl and many others.
Nakubaliana na Muheshimiwa Diwani- we need to legalise it and tax it lakini kwa kuwa hela itakayoingia serekalini itakuwa machoni kwa wengi ni 'chafu' basi hela hiyo hiyo itumike kuanzisha miradi ambayo itawatoa wasichana wanaojiuza kwenye biashara hiyo na kufanya shughuli nyingine ili kujipatia kipato. Kuhalilisha biashara hii pia kutawaondoa machangudoa barabarani na kutupunguzia kero sisi tusiokuwa wateja! tutakuwa tumetunza mazingira pia kwa kuwa condom zilizotumika hazitakuwa zikionekana zimezagaa mitaa (kinondoni makaburini ni mfano hai). Na kubwa zaidi dada zetu hawa watakuwa at less risk ya abuse na harassment. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa pia yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa, kama ilivyo kwenye nchi ambazo hii biashara ni legal, wasichana wanaojiuza hufanyiwa regular mandatory health checks. Hata self esteem yao pia itakuwa iko juu, tofauti ni kubwa sana kwa wanaojiuzia makaburini na wale wanaojiuzia ndani ya nyumba zao.
Nimeshasema hapa kuwa maendeleo sio ujenzi wa barabara, shule na zahanati tu, lets think about the well being of watu kama hawa machanguduo na namna ambavyo tunaweza kuboresha maisha yao, I truly believe kwamba kuhalilisha hii biashara yao itakuwa ni huge step towards that.