Uhalali wa ukahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhalali wa ukahaba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Darwin, Sep 16, 2008.

 1. D

  Darwin JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwanza sikujua kwamba hii thread niiweka wapi, watakaokereka wanisamehe  ataka ukahaba uhalalishwe

  Diwani wa Kata ya Makuburi jijini Dar es Salaam, Busee Gabbas, ameitaka Serikali na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kuhalalisha biashara ya ukahaba ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi pamoja na kuongeza mapato la taifa.

  Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akitoa mchango wake kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Wilaya ya Kinondoni, lililokutana kwa lengo la kuangalia matatizo na mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Alisema kinachotakiwa kwa serikali ni kuhahalalisha biashara hiyo na kutenga maeneo maalumu ambayo makahaba watakuwa wakiyatumia kwa biashara zao kwa uhakika.

  Alisema pia kutengwa kwa maeneo ya kufanyia biashara hiyo,
  kutawawezesha wateja kujua sehemu ya kupata huduma hiyo bila kificho, tofauti na ilivyo sasa.

  Alisema kitendo cha kuzuia biashara hiyo, kunaigharimu serikali fedha nyingi kufanya misako kwa watu wanaojihusisha na biashara hiyo na kusababisha ongezeko la maambukizi ya ukimwi.

  “Ni wakati muafaka kwa halmashauri yetu na Serikali kuhalalisha ukahaba ili tuweze kujiongezea mapato lakini pia kutasaidia kupunguza maambukizi ya ukimwi,” alisema Gabbas.

  Alisema kuruhusu ukahaba si jambo geni kwani mataifa yaliyoendelea, yanafanya hivyo kwa kuitambua na kutenga maeneo maalum lakini pia hujipatia kipato kutokana na kukusanya kodi kutoka kwa makahaba.

  Alisema halmashauri inapaswa iwape leseni ya kufanya biashara watu wenye nia ya kufanya biashara hiyo na yenyewe ijuhusishe katika kukusanya mapato.

  Alisema askari au mgambo wanapofanya msako wa makahaba
  wanatumia fedha nyingi za walipa kodi ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo kama biashara hiyo itaruhusiwa.

  “Si siri kuwa tunapoteza fedha nyingi katika misako ya makahaba ila hali tungeruhusu tungepata fedha badala ya kutoa,” alisema Gabbas.
   
 2. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri lakini liangaliwe pande mbili. Moja maadili na pili hali halisi ya ufahamu wa wadanganyika.
  Je watu wataelewa hili? Je wanatambua kweli kuwa serikali inapoteza mabilioni ya pesa kwa ajili ya kupambana na UKIMWI tu!!

  Panahitajika debate hapa na hoja mbalimbali ili tuweze kuona kama itafaa(kwenye kupunguza gharama) ili tusijute baadae.
   
 3. M

  Magehema JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siamini kama hilo ni wazo zuri kwasababu mamlaka husika inataka kudeal na matokeo ya tatizo na sio tatizo lenyewe. Nadhani hao wafanyao umalaya hawafanyi kwa kupenda ni ugumu na maisha. Ni jukumu la mamlaka husika kuangalia chanzo cha tatizo na sio kukimbilia kushughulikia matokeo ya tatizo. Kwa mwendo huu anaweza akatokea Mheshimiwa akapropose vibaka nao wasajiliwe na walipe kodi!!! Teh tehe teheeee!
   
 4. D

  Darwin JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Au pengine hao wanaofanya ukahaba wawe pia wanapata kuchekiwa na madokta kila baada ya muda.
  kwa maana hio wawe na afya nzuri, wateja wasalimike LOL

  Ila itakua aibu kama sisi ambao tunavizia sehemu za mitaa fulani, ukienda tu huko unaambiwa kaenda kwa makahaba.
   
 5. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  PROSTITUSION IS THE 1ST AND OLDEST PROFESSION.
  Other professions zilifuata baadaye.
   
 6. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  .......Muhimu huduma...wanaosema acha waseme!!
   
 7. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama kuna DEMAND na SUPPLY ipo then there is a need 4 us kufikiria hili suala sisi sote kama jamii ni kwa jinsi gani tutaweza kutrade hii PRODUCT.

  Kuibuliwa kwa sector hii itasaidia sana kupunguza makali ya ongezeko la mara kwa mara la kodi kwenye mafuta ya taa na vinywaji baridi na other consumables

  Serikali itakuwa IMEIBUA ajira mpya na lile lengo la ajira milioni moja WILL BE EXCEEDED BEYOND EXPECTATIONS.

  TALKING ABOUT BROADENING TAX BASE ,THIS IS IT.
   
 8. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona mumekuwa wepesi wakusahau kwani si kulikuwapo na jengo la MARGOT pale hata mawaziri hufika kwamapumziko ya muda mfupi kwa wakati ule au naweza kusema kukosha rungu wala hayati mwalimu hakuwahi hata siku moja kukema au kusema pafungwe .
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Zamani pale karibu na Dar Tech kulikuwa na vibanda vya Wahaya, wanafunzi tulikuwa tunaenda kupata huduma hapo ya bei rahisi.

  Ni ngumu kuua biashara ambayo ina wateja wengi.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hilo la kwanza kuhusu maadili haliwezi kujadilika, kwa sababu tayari maadili kwenye jamii yetu yako lowest, hayawezi kwenda low zaidi ya yalipo sasa. Ukahaba wa sasa uko-wazi ingawa hauko legal, ni vizuri kama ukawa legal lakini si kweli kuwa kulegalize kutapunguza maambukizi. Kwa sababu waambukizaji wakubwa sio wao, kuna utafiti mmoja mdogo ulifanyika ukagundua kuwa, wanafunza wa shule fulani fulani za sekondari ndio wako infected zaidi na wako vulnerable zaidi kuliko makahaba.
  La pili kuhusu maadili ya kuufanya ukahaba uwe chanzo cha mapato, sioni kama kunapingana na maadili yoyote, mbona sasa hivi ufisadi ni chanzo kikubwa cha mapato kwa baadhi ya watu? mbona hilo halikemewi ipasavyo? Hata hivyo ni kiasi gani ambacho serikali inapata kutokana na soko la ukahaba. Hatuna makahaba wa kutosha kuweza kuwa na ukahaba industry ya kuifanya iwe sehemu ya source ya income hata ukusanyaji wake wa kodi utakuwa mgumu sana. Unless kuwe na madanguro ambayo hata hivyo watanzania mafuska hawatakubali kwenda.
  Hii issue ni debateable sana, kama ni kuishughulikia tuanze kwanza na majumbani, kusiwe na watoto bastards kwanza na familia lazima zichukue wajibu wao wa kuhakikisha hazi-produce watu wa design hii.
   
 11. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naona diwani ametoa wazo huru (objective). Ni wazo realistic kabisa. Hii habari ya kuficha the obvious ni baya. Haina tofauti na kuwahubiria watu kuwa wasitumie condom bali wawe waseja wakati inajulikana kuwa wahubiriwa ni wazinzi na hawataacha hiyo tabia! Let's face it. Ingawa mimi binafsi kwa misingi ya kimaadili na kidini silipendi hili wazo! Silipingi lakini silipendi!
   
 12. D

  Darwin JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Umeshindwa kuelewa tofauti ya kibaka na kahaba.

  Kibaka anachukua bila idhini ya mhusika.

  Kahaba wanafanya makubaliano kati ya watu wazima, kwahio haitakoea hata siku moja mheshimiwa akapropose vibaka wasajiliwe na kulipa kodi.

  Mwisho

  Hata huyo kahaba kama umembaka bila idhini yake basi utapelekwa Segerea
   
 13. D

  Darwin JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hahahaaaa, kukosha rungu.
   
 14. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  La msingi ni kuhalalisha tu kwani biashara hii imetapakaa kila kona ya nchi hii na nchi zote duniani. Ni muhimu kukubaliana na uhalisia wa mambo, afterall TZ haitakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo:

  Faida ni nyingi kuliko hasa, kwa mfano:

  1. Wanawake na wasichana watapata stahili yao bila kunyonywa na wajanja wenye madanguro yasiyo rasmi
  2.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Sep 16, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  uhalalishwe usihalalishwe....ukweli ni kwamba utaendelea kuwepo....
   
 16. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  La msingi ni kuhalalisha tu kwani biashara hii imetapakaa kila kona ya nchi hii na nchi zote duniani. Ni muhimu kukubaliana na uhalisia wa mambo, afterall TZ haitakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo:

  Faida ni nyingi kuliko hasa, kwa mfano:

  1. Wanawake na wasichana watapata stahili yao bila kunyonywa na wajanja wenye madanguro yasiyo rasmi
  2.Serikali itaongeza chanzo kingine cha uhakika cha kodi
  3. Afya za wanawake na wasichana zitaweza kuwekewa utaratibu mzuri wa kuziangalia, kwani unawezekana wale wote wenye kuendesha biashara hizo wakatakiwa kuwana utaratibu wa kuwachunguza afya zao kwa faida ya hao wanawake pamoja na wateja
  4. Midume dhurumu itakuwa imefunzwa adabu na kuondoa unyanyasaji wa wanawake
  5. Kuthibiti magonjwa ya ngono itakuwa ni rahisi sana
  6. Kuna uwezekano wa kupunguza nyumba ndogo kwa wanaume
  7. Kuna uwezakano wa kupunguza wanaume wabakaji kwani hata wasiyoweza kumwaga sera za kutongoza mwanamke atahitaji kuuliza bei tu na kuchagua kulingana na bei yake
  8. Uwezekano wa kupunguza watoto wa mitaani kwani itabidi pia suala la kutoa mimba liruhusiwe kisheria pia itakuwa rahisi NGO na serikali kutoa mafunzo ya namna ya kupractise control of unplanned pregnancy kwani itakuwa rahisi kuwafikia wanawake na wasichana wengi kwa pamoja kirahisi.
  9. et cetera, et cetera.

  Ni muhimu tujaribu kwenda na mambo ya maisha kihalisia zaidi kuliko kujifanya hatuoni ukweli huku tukijidanganya.

  Ahsanteni,
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Baada ya kuhalalisha UKAHABA hatua ya pili ni kuhalalisha USHOGA...!

  Nao pia watachangia pato la taifa... Maana umaskini wa taifa letu unaweza kukua kwa kuhalalisha mambo haya ya UKAHABA na USHOGA au sio...!?
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ukahaba na ushoga ni vitu viwili tofauti... usipindishe mada
   
 19. D

  Darwin JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama jamaa alivyosema juu, unapindisha mada!

  Ushoga na Ukahaba ni vitu tofauti

  Ukahaba= kufanya kwa ajili yakupata kipato

  Ushoga= hawa wanafanya kwa raha zao tu nisizojua, haya niambie wataliletea vipi taifa mapato?
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hakuna kupindisha mada...! Ushoga na Ukahaba ni vitu pacha. Penye Ukahaba na Ushoga Haukosekani.

  Wakipewa Green light Makahaba na Ukahaba wa jinsia moja pia Utataka kupewa Green light.

  Kwani kuna tofauti gani kati ya vitendo hivi viwili?

  Ukahaba na Ushoga vyote ni Prostitution...! Vitendo vyote hivyo vinaingia kwenye kundi la UASHERATI.

  Ukihalalisha kimoja na Kingine kitadai haki Kwani kama nilivyosema hapo kabla Hawa ni ndugu pacha. Huwezi watenganisha.
   
Loading...