Fikra yangu sio dini yangu

fakhbros

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
338
550
Katika maisha ya kawaida jamii inakuwa na watu wa kila tabia na tabia ndio zinazoweza kuitambulisha jamii husika

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alianzisha kampeni yake yakupambana na wamiliki wa Madangulo katika viunga vya jiji la Dar

Kwa hulka za waungwana ni kweli ukahaba sio jambo jema kimaadili kutokana na mila na desturi zetu kama watanzania na sio jambo jema katika ustaraabu wa Dini zote zenye heshima juu ya Mungu

Lakini kwa nini vita hii ya kuondoa madangulo iwaumize makahaba wa hali ya chini nakuwaacha makahaba walio starabika kueendelea na biashara yao pasina kuguswa na mamlaka

Nimejaribu kutafakari mbona ukahaba limekuwa ni jambo ambalo linatugusa wote kama watanzania?

Kuna ukahaba unaofanyika kwenye majengo yanayo uza vilevi kama mabar au grocery huku wahudumu wa hizo sehemu wanajiuza wazi wazi na hawaguswi na mamlaka

Kuna ukahaba kwenye taasisi za uma kama mahosptalini, Mashuleni, vituo vya police, Magereza, na hata kwenye halmashauri zetu wapo makahaba walio staarabika lakini kwenye vyama vya siasa kuna makahaba lukuki walio valia uniform za vyama na bado utawakuta Bungeni kama watunga Sheria

Tafakari yangu inanihofisha nakunihuzunisha ikiwa ndani ya nchi yetu wapo watu walio someshwa na mama wanaojiuza katika madanguro au mabar na wanafanya vyema kwenye jamii kwanini mkuu wa mkoa alie teuliwa na mamlaka ya juu aidharau nakunyanyasa watu wanaofanya biashara ya ukahaba?

Makahaba wapo wakike na wakiume na wote wanaishi kwa kutegemeana katika vitabu vya dini vinamtaja Nabii wa Mungu Sellemani kuwa alikuwa na wake 700 na michepuko 900 hivyo Sellemani aliweza kutoka na wanawake 1600 hii ni ishara ya wazi kuwa mwanaume hawezi kuishi kwa kutegemea mwanamke mmoja au wawili au wanne bali hao wachache wanaweza kuishi kwa kumtegemea mwanaume mmoja na bado maisha yakaendelea sasa jamii ikiondokewa na hawa watu wanao pingwa na mkuu wa mkoa heshima ya mwanaume itapatikana wapi au Serikali imejipangaje kukabiliana na migogoro ya ndoa?

Mambo ambayo ndoa nyingi zimepelekea kuvunjika sio kwamba wanaume walishindwa kuwahudumia wake zao bali ndoa nyingi zimekufa kutokana na wanawake wengi kushindwa kuwatimizia tendo la ndoa wenza wao wa kiume na sio rahisi mwanaume kumvumilia mwanamke ambae hampatii tendo la ndoa bali anaweza kumvumilia endapo huyo mwanaume atakuwa na sehemu anayo pata utulivu huo anao ukosa kwa mkewe

Kuondoa jamii ya wahudumu wa madanguro ni kutaka kuruhusu migongano ndani ya jamii

Wahudumu wa Madanguro wanapanda daladala, wananua nyama buchani, wanamiliki simu nakununua vocha, wakiugua wanatibiwa kwa kulipa pesa wanalipa kodi za nyumba wanako ishi na wanalipia vyumba maeneo wanakofanyia biashara zao sasa Serikali inapo chukua jukumu lakuwaondoa mzunguko wa pesa kwenye maeneo yao hamuoni kama unakwenda kupotea kwanini Serikali isingelifnya tafiti kabla yakuanza kuwadharilisha mama zetu ambao wametusomesha kupitia hiyo biashara

Tafakuri yangu ni kwamba sioni ushindi kwa Serikali juu ya biashara ya Ngono kama Serikali inaweza kushinda.

52F1FC40-7BF5-491B-B2B4-692E607E9CD2.jpeg
 
Back
Top Bottom