Uhalali wa Tanzania kuwa mpatanishi wa Mgogoro wa Burundi uko wapi?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,786
Nimetafakari kuona uhalai na ujasiri wa Tanzania walionao kushiriki katika vikao adilifu vya upatanishi kuhusu mgogoro wa Burundi, nimeshindwa kuuona.

Iweje leo umuone mtu aje akifoka na kughani tenzi za kubembeleza amani wakati kisogoni kwake ndugu zake wanaishi kwa hofu na jinamizi zisiokwisha?

Iweje leo Tanzania ilalamikie uchafu kwenye paa la nyumba jirani yake wakati kizingiti cha nyumba yake kimekithiri uchafu unaonuka? utapata wapi ujasiri wa kukemea na kumkaripia yule aliotenda kosa?

Hivi leo Burundi kukataa kuhudhuria kikao hicho cha upatanishi mjin Arusha, ataonekana mtukutu na jeuri, huku akijua fika kuwa hakuna mufaka wa maana uatakaopatikana? Ni uamuzi wa busara!

Wasuluhishi wenyewe kwao mitafaruku mitupu na wanashindwa hata kuteguwa kitendawili kilicho wazi na chepesi .Sembuse hiki kinachohitaji mtu kupewa mji!

TANZANIA SHUGHULIKIA TATIZO LA ZANZIBAR KWANZA KABLA YA KUJIVIKA KILEMBA CHA MIBA UKAFIKIRIA NI UKOKA
 
acha nione muv la Tanganyika vs Zanzibar litaishia wapi....utam kolea..asante mtoa post
 
Yaani hawaoni hata aibu! Wanaacha mambo ya zanzibar hapa wanakimbilia Burundi, tofauti ni nini sasa?
 
Back
Top Bottom