Uhalali wa cheti kutoka Marriage Conciliation Board ni upi?

Wakuu habari,

Inatambulika kuwa inapotokea shida ya kutoelewana kwa wanandoa wawili na kutaka kusuluhisha migogoro yao, hushauriwa kuendea mabaraza ya usuluhishi ya ndoa;

BAKWATA (kwa ndoa iliyofungwa kwa sheria za kiislamu) na Taasisi za kikristo au kanisani ( kwa ndoa iliyofungwa kwa sheria za kikristo)

Sasa je, ni upi uhalali wa cheti kutoka hayo mabaraza ya usuluhushi kwa ajili ya kupeleka mahakamani inapotokea kushindwa kusulihisha mgogoro kwa wanandoa kwa ndoa yenye viashiria ya kuvunjika?

Je, barua kutoka hayo mabaraza inaweza kutambulika kama ushahidi/ cheti kwa mahakama?

Je, ni nani anatakiwa kusaini hivyo vyeti?

Je, ni taratibu zipi za kufuatwa kisheria kwa uhalali wa cheti kutoka mabaraza ya usuluhushi ya ndoa?
Husainiwa na watu wawili ambao ni
1. Mwenyeki wa baraza hilo(Chairperson or chairman)
2. Katibu wa baraza( Secretary).

Kwa sasa sheria anamtaka muomba talaka aambatanishe nakala ya cheti wakati wa kufungua maombi ya talaka halafu ile original certificate itolewe wakati wa kusikilizwa hayo maombi ya talaka. Lengo ni kwamba inabidi mahakama ijiridhishe kwamba hiyo certificate imepatikana kihalali na sheria zote zimefuatwa.

Zamani watu walikuwa wanagushi sana hizo certificate na kuzipeleka mahakamani ambapo sasa mahakama zilikuwa hazichukui muda kufanya utafiti kwamba hii certificate imepatikana kihalali au lah!
 
Back
Top Bottom