Uhalali wa Baraza la Mawaziri baada ya Bunge kuvunjwa ukoje?

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,127
Reaction score
1,634
Naombeni kujua mwenye ufahamu atufahamishe inakuwaje hawa mawaziri wa Rais Samia mpaka sasa wako Ofisini wakati Bunge limeshavunjwa. Inavyoeleweka kikatiba Waziri hutokana na Mbunge, Mbunge anapo poteza haki ya kuwa Mbunge automatically anapoteza hadhi ya kuwa Waziri. Na iko wazi ki Katiba tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Rais atavunja Bunge na Baraza la Mawaziri, na Wizara zitakuwa chini ya Watendaji Wakuu wa Wizara husika ambao kimfumo tulionao ni Makatibu Wakuu wa Wizara mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo Rais aliyseshinda atateua baraza lake la Mawaziri kutoka miongoni wa wabunge wake walioshinda Uchaguzi au atakaowateua. Sasa Mawaziri hawa wa sasa hivi kila siku wako ofisini na barabarani na wakitoa maelekezo kila siku wakati kisheria hawana haki hizo. Nashawika kuwa na mashaka na hawa Mawaziri wasije wakafanya mambo yasiyokuwa na maslahi kwa Nchi ikiwemo kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa Nchi na utakapompeleka Mahakamani watashinda kwani wanaweza kabisa kusema yeye hakuwa Waziri. Ni sheria ikampa ushindi. Awamu Hii tunashuhudia uvunjwaji wa sheria na kanuni ambazo ni za hatari sana. Aliye karibu na Mama amwambie hao watu wapishe ofisi za Umma; Makatibu Wakuu waendelee na Majukumu yao. Over
 
Kama makatibu wakuu wa wizara wapo haina maana mawaziri kuendelea kuhudumu kwani ubunge wao umekoma baada ya bunge kuvunjwa
 
Hili suala hata mimi nimekuwa najiuliza pia.Kisheria mawaziri wanapaswa kuwa wabunge sasa hawa waliopo wapo wapo je????? Na kwa Katiba ipi labda.Wataalamu wa Katiba tupeni uelewa tafadhali.
 
Naombeni kujua mwenye ufahamu atufahamishe inakuwaje hawa mawaziri wa Rais Samia mpaka sasa wako Ofisini wakati Bunge limeshavunjwa. Inavyoeleweka kikatiba Waziri hutokana na Mbunge, Mbunge anapo poteza haki ya kuwa Mbunge automatically anapoteza hadhi ya kuwa Waziri. Na iko wazi ki Katiba tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Rais atavunja Bunge na Baraza la Mawaziri, na Wizara zitakuwa chini ya Watendaji Wakuu wa Wizara husika ambao kimfumo tulionao ni Makatibu Wakuu wa Wizara mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo Rais aliyseshinda atateua baraza lake la Mawaziri kutoka miongoni wa wabunge wake walioshinda Uchaguzi au atakaowateua. Sasa Mawaziri hawa wa sasa hivi kila siku wako ofisini na barabarani na wakitoa maelekezo kila siku wakati kisheria hawana haki hizo. Nashawika kuwa na mashaka na hawa Mawaziri wasije wakafanya mambo yasiyokuwa na maslahi kwa Nchi ikiwemo kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa Nchi na utakapompeleka Mahakamani watashinda kwani wanaweza kabisa kusema yeye hakuwa Waziri. Ni sheria ikampa ushindi. Awamu Hii tunashuhudia uvunjwaji wa sheria na kanuni ambazo ni za hatari sana. Aliye karibu na Mama amwambie hao watu wapishe ofisi za Umma; Makatibu Wakuu waendelee na Majukumu yao. Over
Magu ndio alianzisha hiyo takataka, mwenzie kaiga tu.
 
Back
Top Bottom