JOSEPHAT J BAZA
Member
- May 4, 2013
- 27
- 22
Kwanza Mh. Rais kwa kuondoa watumishi wote waliobainika kughushi vyeti katika utumishi wa umma. Lakini ili zoezi hili liwe na maana zaidi ni vema lingewagusa watu wote kuanzia Ikulu, wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wote. Nasema hivi kwa sababu kwa mujibu wa sheria kughushi cheti ni kosa la jinai bila kujali hadhi au wadhifa alionao mtu. Sasa najiuliza kwanini baadhi ya kundi la watu halikuguswa? je, kuna nini chini ya kapeti? au tuseme ni njia ya kumlinda bashite? Kama kweli Mh. Rais ana nia ya dhati katika suala hili anapaswa kuwaondoa wote wenye vyeti feki bila kujali hadhi au wadhifa wao kwani sifa pekee ya kiongozi bora ni kuwa mfano bora wa kuigwa na walio chini yake. Aidha katika kuwaondoa kwenye orodha ya malipo umakini ufanyike ili wale walio safi wasiathirike. Pia nalishauri baraza la mitihani wanapotoa matokeo ya mithani wawe wanaandika jina kamili la mtu. Hii itasaidia raia wema kutoa taarifa pale unapomkuta mtu alipata daraja o kwa kutumia jina fulani kisha unamkuta ana cheti chenye daraja 1 kwa kutumia jina lingine.