kkarumekenge
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 1,708
- 1,028
Upo ukweli kwamba kuna wafanyakazi wengi wa serikali wana kumbukumbu za uongo juu ya umri wao, wamedanganya wakionyesha umri wao ni mdogo ili wachelewe kustaafu.
Lakini tunasahau kwamba kwa kufanya hivyo wazee hao huziba nafasi za wahitimu kutoka vyuo mbalimbali nchini na inawezekana tatizo la ajira rasmi nchini linaweza likawa sivyo lilivyo sasa.
Wahitimu hawa wapya watapataje ajira huku nafasi zinaendelea kushikiliwa na wanaopaswa kustaafu, wengine hata miaka mitano hadi kumi nyuma?
Rais Magufuli, kama alivyofanya uhakiki katika maeneo mengine hili alipitie atagundua madudu mengi ya vyeti feki vya kuzaliwa kutoka RITA wakati huo ikiitwa Vizazi na Vifo.