Uhaini wa Mtwara ulipangwa

Uhaini wa Mtwara ulipangwa

Mkuu unachosema ni kweli haya ni mandalizi ya kitambo yenye malengo maalumu,watu walishasema nchi isitawalike vitu kama hivi tuvitarajie tu kwa watu wapumbavu wenye nia mbaya na taifa letu ila kamwe hawatafanikiwa na mwisho wao waja.
 
Ikiwa nitajibiwa kwa facts nitaridhika na kuona kuwa sasa JF inao washiriki ambao ni great thinkers haswa sio wale wa matusi na posho. JF hii inapaswa kuwa bora kuliko ilivyo sasa, na inaweza kuwa hivyo tu ikiwa watu wake wanafanya na kusema yale ambayo great thinkers wanatakiwa kuyasema na kuyafanya.
Tatizo lenu wana ccm mmesahau kuwa ukicheka na nyani unavuna mabua.

Wenzenu wanacheza rafu zote ili kuweza kuwatoa madarakani nyie bado mnakenua meno,watu kama kina lema,mwisiga etc wanachochea vurugu serikali inawakamata kwa mda na kuwaacha huku wakipelekwa mahakamani kama geresha tu,mnategemea nini wakati serikali inawakamata wachochezi leo,kesho wanatolewa hukt wakibebwa jujuu na vijana kama mashujaa.ITAKULA KWENU NAWAMBIENI.
 
Mkuu unachosema ni kweli haya ni mandalizi ya kitambo yenye malengo maalumu,watu walishasema nchi isitawalike vitu kama hivi tuvitarajie tu kwa watu wapumbavu wenye nia mbaya na taifa letu ila kamwe hawatafanikiwa na mwisho wao waja.

Kibwete = Kikwete ??
 
Ikiwa nitajibiwa kwa facts nitaridhika na kuona kuwa sasa JF inao washiriki ambao ni great thinkers haswa sio wale wa matusi na posho. JF hii inapaswa kuwa bora kuliko ilivyo sasa, na inaweza kuwa hivyo tu ikiwa watu wake wanafanya na kusema yale ambayo great thinkers wanatakiwa kuyasema na kuyafanya.

Sasa mkuu TandaleOne ngoja nikujibu walau mambo machache ambayo yana facts kwa kadri ntakavyoweza ila nakuomba usikimbie.

  • Kwanza unaposema kwa sasa Jf ina members wa matusi na posho unakosea maana na wewe uko humu.Au unataka utuambie nawe ni mdau wa matusi na posho! hapana bwaana wewe na watu wengine ni miongoni mwa great thinkers!au unasema je?


  • Pili; nikubaliane na wewe kwamba kinachotokea Mtwara ni zaidi ya gesi.Gesi imekuja kuwa ni kichocheo tu cha fujo ila nyuma yake kuna mambo kibao.Tunatakiwa tufahamu kwamba migogoro mingi huwa inakuwa na chokochoko za muda mrefu za chini kwa chini lakini ili kufikia hatua ya mapambano kuna jambo moja tu ambalo ndilo husababisha (Wataalam wa masuala ya usuluhishi wa migogoro wanajua sana hili).Mf. Rejea vita ya kwanza na ya pili ya dunia.


  • Mkuu TandaleOne ; yatupasa tufahamu kwamba watu wa mtwara wanalalamika toka siku nyingi kwamba wao wameachwa nyuma kimaendeleo ukilinganisha na kanda nyengine (Na hili liko wazi sidhani kama linahitaji mjadala).Hali hii imesababisha wawe wanajisikia wanyonge, waliotengwa, wanaonyonywa, wanaodharauliwa, wanaopuuzwa kwa kiwango cha juu kabisa lakini wakiwa hawana la kufanya.Kwa kipindi chote wamekuwa wakidhani tatizo ni unyonge wao .(ki uhalisia inaweza kuwa kweli au laaa; ila huo ni mjadala mwengine).Hali hiyo imekuwa ikiwajengea hasira; hasira ambazo zimekuwa zikijilimbikiza.


  • Kwa nini mgogoro uibuke sasa; Kugundulika kwa gesi na kutangazwa kujengwa kwa bomba kwenda dar bila maelezo ya kutosha, kueleweka, kushirikishana na wananchi wa kusini kutoandaliwa kisaikolojia kuupokea mradi; imekuwa ni sababu za wao kuutua mzigo wa hasira walizokuwa nazo dahari na dahari.


  • Pia ifahamike kwamba maadui wa nje nao wanapoona mahali kuna rasilimali; hutafuta sehemu yenye mwanya wanauongezea ili wanyonye rasilimali pale wanapotaka kufanya hivyo.kwa hiyo mgogoro huu kwa sasa pia utakuwa unachagizwa kutoka nje.


  • Je! kuharibu mali kunasaidia nini!; Kitaalam hakusaidii kitu, ila kisaikolojia inafahamika kuwa mtu mwenye hasira kali huwa mara nyingi hafanyi uamuzi yasiyo "Rational" Hata Mh.Jakaya Kikwete Alishawahi kusema wakati fulani anapata hasira na kutoa maamuzi ya ajabu ila washauri wake humshauri "Mzee; hebu pumzika kwanza kidogo halafu ndoo utoe maamuzi" naye akishapumzika hasira zikishuka basi hutoa maamuzi tofauti kabisa.Hili ni suala la kimaumbile (kibinadamu).Sasa unatakiwa ujue kuwa watu wa mtwara wana hasira na negative feelings halafu hawana washauri na hawana uelewa wa kutosha juu ya mambo kama ilivyo kwa Jk, na hawashirikishwi vya kutosha kwenye mradi unaoleta matatizo.


  • Kwa nini wanashambuliwa wana CCM na ofisi za CCM; Ni kwa sababu wao ndio wanaounda serikali na wanamtwara wanahisi serikali ndio adui yao.


  • Ni nini cha kufanya; Hali ikishatulia, ni suala sasa la kutafuta maridhiano kwanza kutoka kwa pande zinazozozana , kila upande utoe hoja na kusikilizwa na ujisikie umesikilizwa na kushirikishwa vya kutosha na kisha hoja zenye nguvu ndio zifanyiwe kazi.Kabla ya utekelezaji; ni lazma ajenda za maridhiano zifikishwe kwenye jamii nzima ya wana kusini na kuhakikisha kwamba walio wengi wamezielewa.


  • Mambo haya yalitakiwa yawe yashafanyika hata kabla ya mgogogoro, lakini kwa kuwa ndo sasa hayajafanyika, mimi nadhani tusilaumiane badala yake tufanye sasa.


  • Nakushauri haya uwafikishie na wenzako yatasaidia.
 
Haya maneno ni mazito sana na yana reflect the ongoing situation,''Gesi kwanza,maisha baadae",kimsingi si maneno ya kupuuza.
 
Leo asubuhi ya saa mbili na dakika 56 (08:56:16am) nimepokea ujumbe wa simu kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, ambae kwa cheo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Ujumbe wenyewe ni huu ufuatao:


Ujumbe huu uliniongezea simanzi na majonzi niliyonayo juu ya maafa mbalimbali yaliyojitokeza katika vurugu za Mtwara jana. Simanzi hii ilitokana na kuona hali ya unyonge, woga na wasiwasi mkubwa walionao viongozi wenzangu wa Chama, wasiwasi huo hautokani na woga wa kitoto bali kutokana na hatari wanayoiona mbele yao ya kuwindwa, kushambuliwa na kufanyiwa hujuma na matendo mengine ya kudhuru mwili.

Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo.

Maana ya maneno mawili ya mwanzo ya yaani hujuma na uhaini yanafuatana kwa maana hujuma inaweza kutumika kama mkakati wa uhaini. Uhaini ni tendo la kusaliti nchi, serikali au mfadhili; uasi. Hujuma ni shambulio ama vamio: fisidi, kuvuruga ama kuharibu.

Maana ya kipengele cha tatu ambacho kimebeba maneno mawili harakati na siasa, ama siasa ina maana ni mfumo wa mawazo yaongozayo utawala wa serikali ya nchi tafsir nyingine ni utaratibu wa utekelezaji au uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo linalotarajiwa.,na maana ya neno la mwisho yaani harakati ni juhudi zinazoafanywa na watu kwa ajili ya kufikia lengo fulani, bidii, jitihada.

Katika tafsir hizo tatu, kinachoendelea mtwara hivi sasa tunakitoa kabisa katika maana halisi ya harakati za kisiasa, kwa kuwa maana ya harakati za kisiasa ni juhudi za kupanga utaratibu wa mfumo wa mawazo yaongozayo (ama yanayolenga kuongoza) utawala wa serikali ya nchi.

Kwa maana ya Hujuma kuwa ni shambulio, kuvuruga ama kuharibu ni sahihi kwa upande mmoja kuwa hiki ndicho kinachoendelea mtwara lakini kwa tafsir ya uhaini ndiyo hasa inayoelezea kinachoendelea Mtwara.

Ndio ni uhaini uliopangwa na kutekelezwa na watu wenye nia mbaya na nchi hii, wasio wazalendo na waliokosa utaifa. Wanaoendesha mkakati wa nchi kutotawalika, kwa kuibua hujuma mbalimbali dhidi ya serikali na chama kiendeshacho serikali hiyo yaani CCM.

Sio ajenda na hoja ya gesi, bali hoja hii imetumika kimbinu kuendesha mkakati huu wa kihaini ambao unawawinda wanaCCM, ofisi zao, mali zao pamoja na serikali yao. CCM ni chama cha siasa kinafanya siasa ya kuendesha nchi hii, vipo vyama vya upinzani navyo vinalenga kuelekea katika mlengwa huu wa kisiasa, lakini wakati mwingine vinapotoka na kuacha Siasa ama harakati za kisiasa na kujikuta wakifanya hujuma na vitendo vingine vya kihaini. Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?



WHEN THE RICH AND CCM ROB THE POOR IT'S CALLED BUSINESS,

WHEN THE POOR FIGHT BACK IT'S CALLED VIOLENCE & UHAINI??

FACE IT...!


Pia nenda kamwambie na boss wako nape sisi tunaskia furaha sana kuwaona mnalia na kusaga meno kias hiki,mambo haya ambayo mmeshindwa kuyatekeleza yalikuwa kwenye ilani yenu wakati mnaomba kura,sasa mmebakiza mwaka mmoja muondoke madarakani bado mnaendelea kuja na kutupa maneno ya kwenye vitabu na ahadi za kusadikika,hilo hatutalivumilia na tumeghair moja kwa moja,na kazi ndio kwanza imeanza....
 
  • Thanks
Reactions: awp
Kwa nini hawa watu wanalenga nyumba za ccm na wanaccm hapa hutakiwi kutumia akil nyingi kupata majibu huu ni mpango wa siasa lakini watu si wajinga na hili litakoma tu.
 
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .

Mheshimiwa Spika, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba chama lege lege huzaa serikali legelege; udhaifu huu wa wizara unaweza kutafsiriwa kwamba unachangiwa na ushiriki wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupewa na kukubali hisa toka kwa moja ya makampuni yanayojihusisha na utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini, kampuni ya Ophir energy. Kwa mujibu wa taarifa rasmi za Bunge za tarehe 08.11.2012 ni kuwa wakati CCM ikipewa hisa wapo pia baadhi ya watanzania ambao waligawiwa sehemu ya hisa hizo kwa ajili ya CCM

Aidha,Katibu Mkuu wa CCM Abdurahaman Kinana anatajwa na vyanzo mbalimbali kwamba amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Artumas ambayo iliingia mkataba na Serikali wa kuzalisha Mega Watt- 300 za umeme Mtwara eneo la Mnazi Bay. Mkataba huo ulikuwa wa misingi ya mabadilishano ya gesi kwa nishati ya umeme (gas for power). Kwamba Artumas ingechimba na kuuza gesi asilia na kuilipa serikali kwa pamoja na mambo mengine kuizalishia umeme wa 300MW. Baadae mwaka 2010 Artumas baada ya kufaidika vya kutosha kutokana na uvunaji na uuzaji iliacha kuendeleza mradi huo kwa kisingizio cha madai ya mdororo wa Uchumi mwaka 2009 na kuuza hisa zake kwa kampuni ya Wentworth ya Ufaransa.

Mheshimiwa Spika, Ushiriki huu wa viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi na chama hicho kwenye shughuli ambazo zinaitia hasara serikali unazua mazingira ya kwamba CCM inasababisha unyonywaji wa Taifa na wananchi, na hivyo ni dhahiri si mwafaka kuendelea kuongoza nchi hii. CCM na baadhi ya viongozi wake wamekuwa wakifaidika kutokana na ombwe la kisera na kisheria katika sekta hii na nyingine muhimu. Katika hali kama hii, maneno ya Mwalimu Nyerere yanapaswa kuongezewa nukuu mpya kwamba “chama cha mafisadi huzaa serikali ya mafisadi”.
Mheshimiwa Spika, Kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni, utekelezaji kivitendo wa dhana ya mali ya umma wakati wote wa uhuru umekuwa ni kuwanyang'anya wananchi rasilimali asilia zilizoko kwenye maeneo yao na kuzimilikisha mamlaka za Serikali (wakati wa miaka ya uchumi-dola), au kuzimilikisha kwa wawekezaji wa kigeni katika zama hizi za soko holela kwa kisingizio cha huria.

Mheshimiwa Spika, Matokeo ya mfumo huu ni kwamba milki na mamlaka ya maamuzi juu ya matumizi ya rasilimali asilia yameondolewa mikononi mwa wananchi na kuhamishiwa kwenye mikono ya warasimu wa Serikali. Sio hio tu, wananchi wamejikuta wakiondolewa kwa nguvu kutoka kwenye maeneo yao ili kuwapisha wamiliki wapya wa rasilimali hizo, yaani wawekezaji wa kigeni au wa ndani. Kwa sababu hiyo, uchumi wa wananchi umeanguka, umaskini umeongezeka na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yameongezeka.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madini imeonyesha udhaifu wa kumnyima hata Mkuguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhakikia mikataba ambayo Serikali imefunga na wachimbaji ili “kubainisha taratibu ambazo zinafuatwa na Wizara katika kutekeleza matakwa ya sheria hii kwa vile mikataba hii ya Uchimbaji ni ya watu binafsi na ni siri kwa watu wengine wasiokuwa sehemu ya mikataba hiyo. Kutokana na usiri huo, sikupewa haki ya kuipitia mikataba hiyo na hivyo kuzuia wigo wa ukaguzi wangu”[4].
 
Tatizo lenu wana ccm mmesahau kuwa ukicheka na nyani unavuna mabua.

Wenzenu wanacheza rafu zote ili kuweza kuwatoa madarakani nyie bado mnakenua meno,watu kama kina lema,mwisiga etc wanachochea vurugu serikali inawakamata kwa mda na kuwaacha huku wakipelekwa mahakamani kama geresha tu,mnategemea nini wakati serikali inawakamata wachochezi leo,kesho wanatolewa hukt wakibebwa jujuu na vijana kama mashujaa.ITAKULA KWENU NAWAMBIENI.

kama huelewi kitu bora ukae kimya.!
 
WHEN THE RICH AND CCM ROB THE POOR IT'S CALLED BUSINESS,

WHEN THE POOR FIGHT BACK IT'S CALLED VIOLENCE & UHAINI??

FACE IT...!


Pia nenda kamwambie na boss wako nape sisi tunaskia furaha sana kuwaona mnalia na kusaga meno kias hiki,mambo haya ambayo mmeshindwa kuyatekeleza yalikuwa kwenye ilani yenu wakati mnaomba kura,sasa mmebakiza mwaka mmoja muondoke madarakani bado mnaendelea kuja na kutupa maneno ya kwenye vitabu na ahadi za kusadikika,hilo hatutalivumilia na tumeghair moja kwa moja,na kazi ndio kwanza imeanza....
Wewe unawasema ccm nyie chadema mmetekeleza lipi au haya ya ugaidi na masndamano.
 
Makubaliano ya Pinda na wanamtwara yapo bayana tena yakiwa na viongozi wa kaya, viongozi wa kisiasa na hata wa kidini wa mtwara. Makubaliano hayo yanabainisha faida na mafanikio ambayo mtwara kama mkoa utanufaika nayo kutokana na miradi ya gesi, lakini hmakubaliano hayo hayakuwa yakikataza gesi kutoka mtwara na hata neno lenyewe kutoka linatrumika vibaya kwa maana kiasi cha gesi ambacho kitaendesha shughuli zakiuchumi za mtwara ni kubwa na inayokidhi haja kuliko hata itakayosafirishwa kwa ajili ya kufua umeme kwa ajili ya gridi ya Taifa.

Ni upotoshaji wenye nia ile ile ya kuvuruga nchi ndio hasa unapelekea matukio na kadhia hizi zenye kuchafua taswira ya Taifa. Wananchi wa mtwara wanao wawakilishi wanaowaridhia, lakini si tu kuwa kuna wawakilishi, serikali na chama kimefanya juhudi kubwa ya kukutana na kujadili na wananchi wa kawaida kabisa juu ya manufaa yatakayopatikana mtwara. Hivyo hakuna usahihi wa aina yeyote kudai kuwa hawakuandaliwa kisaikolojia.

ANOTHER BIG MISTAKE! Hakuna makubaliano yaliyofikiwa wakati ya ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati wa safari yake ya takribani wiki nzima hapa Mtwara. Hoja zote zilizotolewa alikwepa ama kuzielezea au kuzijibu hivyo akaacha hali ya sintofahamu.
 
Wewe KIBE! ishu ya kugoma gesi kugomewa na wanamtwara haikuanza jana ni muda wabunge wa upinzani kwa muda mrefu walipigia kelele bungeni kuhusu mgawanyo wa mapato, mwaka jana wananchi wa mtwara waliandamana sana kupinga, hadi baadhi wakaja ikulu ya dar, na kama utakumbuka vizuri kuna BIBI alilaani kwamba wakichimba tu bomba litatowa maji na sio gesi........., akatumwa mn'goa kucha mmoja kwa bibi wananchi wakamshtukia nusura auwawe akakimbia gari lake likachomwa moto. wananchi wa mtwara wakaendelea kuwa na msimamo kwamba gesi haitoki..kwa hiyo yanayofanyika ni ya wanamtwara wenyewe na sio msukumo toka nje.

1. Silaha za wananchi ni mabomu ya uvuvi,mishale na mapanga ambayo yapo kila siku,miaka yote hayajaagizwa kutoka nje ya nchi.

2. Hivi wewe unataka kuniambia mwananchi akidai haki zake eti "katumwa na wachochezi'' kana kwamba yeye hana akili timamu.......unataka kutuambia hata wazee wetu wapigania uhuru waliambiwa na watu wa nje kwamba nchi zetu zilikuwa zinanyonywa na wakoloni.

3. Hata kama makosa yalifanyika nyuma kwa mikoa ya tabora,shy,mza,mara (migodi ya dhahabu na almasi) sio lazima turudie mtwara.

4. Ingekuwa Mza,A-town,Dar,Moshi serikali ya CCM ingekuja na jibu rahisi kwamba CDM inachochea, ingekuwa Zenj CUF wangetuhumiwa, Sasa mtwara tunadanganya ''mkono wa nje"

5. Wewe kama Mtz em pita vijiwe vya watu wa kawaida Kariakoo,manzese,tandale,Tmk,Kndoni,Mza,Arusha,Musoma,Bk jaribu kuuliza au kusikiliza maoni ya wananchi ndio uende kuwaambia wakuu wako pale lumumba.

6. Tunataka masahihisho yaanzie mtwara, mji ufanane kama miji maarufu ya uchimbaji wa madini kule africa kusini tusirudie makosa ya mwanza,Shy,Tbr,Mara nk.

7. Unaposema mtwara ni mbali, unamaanisha mbali na wapi? kwasababu wanaihitaji gesi watalipia gharama za usafiri kuifuata sababu ni adimu.

8. Eti Mtwara hamna wataalamu ni uongo, Nchi yetu haina wataalamu ndio kwanza wameenda shule.......kama hiyo ni sababu bomba lingejengwa kumwaga gesi urusi ndio kuna wataalam.

9. Wasomi wote wako Dar sababu ya ajira na asilimia zaidi ya 90% si wazawa wa Dar, ni matumaini yangu kwamba hata bomba lingekuwa mtwara bado wasomi wangelifuata mtwara kupata ajira nzuri, mbona migodi ya dhahabu haijahamishwa Tbr,Shy nk lakini vijana wasomi kibao wanakimbilia huko kupata ajira nono.

Kwahiyo ni vema kukaa chini na kuja na suluhisho la juu juu, kwa sasa serikali ya CCM haiwezi kudanganya watu, sababu watu wamekufa kahama,mererani,tarime kwa manufaa ya viongozi walafi pasipo hata manufaa kwa mwananchi. Pia wananchi wakipinga usiuite uhaini, tatizo lako na CCM hamjui kwamba hata Polisi na JWTZ ni watanzania na hawafurahishwi dhuluma kwa wananchi...................

shangazi yangu kipenzi!!! tatizo lako na wewe ni kama vigori wenzako, kazi ni kulalama tuuuuuuuuu,,, jiweke nafasi ya JK na CDM iweke katika nafasi ya CCM kama chama tawala(though it wont happen 4ever),, then bring the solution.. nina hakika huna suluhisho kichwani mwako zaidi ya vile ilivyofanywa, inavyofanywa na itakavyoendelea kufanywa.. acha kulalamika aunt just bring the solution!!!!!
 
Ccm mnapaswa mjue kuwa wenzenu wanafanya haya ili waeze kuwatoa madalakani kama hamlijui hili litambueni.
 
Ninachosikitika ni kuwa wakati tumekubaliana na TandaleOne kwamba tujadili mjadala huu kwa hoja ili kupata kiini hasa cha tatizo; mpasa sasa keshaukimbia mjadala wake aliouanzisha na sijui kama atarudi tena.Akirudi atarudi kama guest.
 
Last edited by a moderator:
Ninachosikitika ni kuwa wakati tumekubaliana na TandaleOne kwamba tujadili mjadala huu kwa hoja ili kupata kiini hasa cha tatizo; mpasa sasa keshaukimbia mjadala wake aliouanzisha na sijui kama atarudi tena.Akirudi atarudi kama guest.

mkuu mimi mwenyewe nilishaanza kuvutiwa na huu mjadala, baada ya TandaleOne kuja na hoja badala ya vioja kama siku zote.

Lakini ndio hivyo tena ameingia mitini.!!
 
Last edited by a moderator:
Unapingana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara "Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa Mkoa"?? Maana yeye kwa kauli yake kasema zile ni vurugu tu ila wewe naona unasema ni Uhaini!!!
 
Tatizo lenu wana ccm mmesahau kuwa ukicheka na nyani unavuna mabua.

Wenzenu wanacheza rafu zote ili kuweza kuwatoa madarakani nyie bado mnakenua meno,watu kama kina lema,mwisiga etc wanachochea vurugu serikali inawakamata kwa mda na kuwaacha huku wakipelekwa mahakamani kama geresha tu,mnategemea nini wakati serikali inawakamata wachochezi leo,kesho wanatolewa hukt wakibebwa jujuu na vijana kama mashujaa.ITAKULA KWENU NAWAMBIENI.
.
ukweli mkuu mi nakubaliana na wewe mana hadi imejengeka sasa kiongozi anayehamasisha vurugu ndio kiuongozi mzuri anaonekana shujaa wa wanyonge na wanatumia hili kutokana na uelewa wetu mdogo hasa vijana ... mf.mzuri USA kwa sasa obama kaweka katiba pembeni ruksa FBI,CIA kuwapoteza wale wote ambao wanahatarisha amani ya nchi mana haiwezekana kikundi au mtu mmoja anaharibu mfumo wa amani ya nchi....
 
mkuu mimi mwenyewe nilishaanza kuvutiwa na huu mjadala, baada ya TandaleOne kuja na hoja badala ya vioja kama siku zote.

Lakini ndio hivyo tena ameingia mitini.!!
Na huu utaratibu wa CCM kukimbia mijadala na kuogopa hata hoja wanazoanzisha wao wenyewe; kwa kiasi kikubwa ndio huleta matatizo nchini.Sasa kwa stahili hii ya kukimbia kimbia halafu wanalalamika oooh! sijui nini na nini! any way mimi sina la ziada.
 
Acha kutoa hoja dhaifu kwa issue za msingi! ni nani anayeendesha serikali kama si CCM?!kwa lolote linalitokea lazima hasira za wananchi zielekezwe kwao.
 
Ikiwa nitajibiwa kwa facts nitaridhika na kuona kuwa sasa JF inao washiriki ambao ni great thinkers haswa sio wale wa matusi na posho. JF hii inapaswa kuwa bora kuliko ilivyo sasa, na inaweza kuwa hivyo tu ikiwa watu wake wanafanya na kusema yale ambayo great thinkers wanatakiwa kuyasema na kuyafanya.

Facts:
a) Mikataba kuhusiana na gesi haijuikani hata Bungeni. Ushirikishwaji umma haukuwepo kitaalamu, ulifanywa kisiasa.
b) CCM ndiyo inayoongoza nchi. Kama CCM inavotaka kuchukua sifa ya mafanikio, iwe tayari pia kuchua lawama za kushidwa. It is unacceptable failures are identified with someone else and all the praise go to CCM.
c) Civil institutions zimeonekana si chochote kwa serikali ya CCM kiasi cha kuitwa za kichochezi. Zimesajiliwa kisheria na kazi zake zinajulikana kikatiba. Serikali ya CCM imeshindwa hata kusikiliza mawazo ya asasi hizi, achilia mbali kufanya yaliyo sahihi kwa jamii. Kama kutetea misingi ya uanzishwaji wa asasi hizi ndio uhai wake, je mategemeo tofauti kutoka CCM na serikali yana msingi upi?
d) Taking the population for granted. Tumesikia viongozi wa juu kabisa wa serikali ya CCM wakisema "ni upepo wa kisiasa, utapita", wengine "kelele za chura hazizuii ..." nk. Hii imeenda kukua na kufikia kuwa dharau kwa umma usio na madaraka!! Mawazo ya wasio na madaraka yamechukuliwa kama upepo upita. Umejengeka utamaduni wa kusubiri jambo bila kulitatua kwa sababu litapita. Societies have dynamics, certain things change!! CCM just didnt track the changes, they took everything for granted.

I am not pro-violence but I agree sometimes we all learn the hard way!
 
Back
Top Bottom