wewe kibe! Ishu ya kugoma gesi kugomewa na wanamtwara haikuanza jana ni muda wabunge wa upinzani kwa muda mrefu walipigia kelele bungeni kuhusu mgawanyo wa mapato, mwaka jana wananchi wa mtwara waliandamana sana kupinga, hadi baadhi wakaja ikulu ya dar, na kama utakumbuka vizuri kuna bibi alilaani kwamba wakichimba tu bomba litatowa maji na sio gesi........., akatumwa mn'goa kucha mmoja kwa bibi wananchi wakamshtukia nusura auwawe akakimbia gari lake likachomwa moto. Wananchi wa mtwara wakaendelea kuwa na msimamo kwamba gesi haitoki..kwa hiyo yanayofanyika ni ya wanamtwara wenyewe na sio msukumo toka nje.
1. Silaha za wananchi ni mabomu ya uvuvi,mishale na mapanga ambayo yapo kila siku,miaka yote hayajaagizwa kutoka nje ya nchi.
2. Hivi wewe unataka kuniambia mwananchi akidai haki zake eti "katumwa na wachochezi'' kana kwamba yeye hana akili timamu.......unataka kutuambia hata wazee wetu wapigania uhuru waliambiwa na watu wa nje kwamba nchi zetu zilikuwa zinanyonywa na wakoloni.
3. Hata kama makosa yalifanyika nyuma kwa mikoa ya tabora,shy,mza,mara (migodi ya dhahabu na almasi) sio lazima turudie mtwara.
4. Ingekuwa mza,a-town,dar,moshi serikali ya ccm ingekuja na jibu rahisi kwamba cdm inachochea, ingekuwa zenj cuf wangetuhumiwa, sasa mtwara tunadanganya ''mkono wa nje"
5. Wewe kama mtz em pita vijiwe vya watu wa kawaida kariakoo,manzese,tandale,tmk,kndoni,mza,arusha,musoma,bk jaribu kuuliza au kusikiliza maoni ya wananchi ndio uende kuwaambia wakuu wako pale lumumba.
6. Tunataka masahihisho yaanzie mtwara, mji ufanane kama miji maarufu ya uchimbaji wa madini kule africa kusini tusirudie makosa ya mwanza,shy,tbr,mara nk.
7. Unaposema mtwara ni mbali, unamaanisha mbali na wapi? Kwasababu wanaihitaji gesi watalipia gharama za usafiri kuifuata sababu ni adimu.
8. Eti mtwara hamna wataalamu ni uongo, nchi yetu haina wataalamu ndio kwanza wameenda shule.......kama hiyo ni sababu bomba lingejengwa kumwaga gesi urusi ndio kuna wataalam.
9. Wasomi wote wako dar sababu ya ajira na asilimia zaidi ya 90% si wazawa wa dar, ni matumaini yangu kwamba hata bomba lingekuwa mtwara bado wasomi wangelifuata mtwara kupata ajira nzuri, mbona migodi ya dhahabu haijahamishwa tbr,shy nk lakini vijana wasomi kibao wanakimbilia huko kupata ajira nono.
kwahiyo ni vema kukaa chini na kuja na suluhisho la juu juu, kwa sasa serikali ya ccm haiwezi kudanganya watu, sababu watu wamekufa kahama,mererani,tarime kwa manufaa ya viongozi walafi pasipo hata manufaa kwa mwananchi. Pia wananchi wakipinga usiuite uhaini, tatizo lako na ccm hamjui kwamba hata polisi na jwtz ni watanzania na hawafurahishwi dhuluma kwa wananchi...................