Uhaini wa Mtwara ulipangwa

Uhaini wa Mtwara ulipangwa

Ulimwengu mzima, mahali ambapo panavumbulika rasilimali fulani, watu wa pale lazima wafaidike kwanza na zaidi, ndio maeneo mengine ya nchi yapate. Wenyeji wa sehemu zenye mafuta wali resist sana baada ya kuona mafuta yanaenda na wao hawafaidiki. Ni wasukuma tu wa Mwanza ndio samaki zao zilichukuliwa,madini yao yakachukuliwa wanaangalia. Serekali ya CCM isipoliona hilo, hata hiyo gas hawataifaidi, wanaweza wakajenga bomba la mafuta likahujumiwa, nani atakuwa amefaidi? Waweke wazi mikataba ya gas kwanza kama wameshachukua 10% waseme
 
Siku zote nimekuwa nikijiuliza huyu TandaleOne ni nani kumbe ni wewe! ok!
Hebu ngoja kwanza tukusanye taarifa halafu tutakujibu kwa facts maswali ambayo hujayapatia majibu mpaka sasa.
Ikiwa nitajibiwa kwa facts nitaridhika na kuona kuwa sasa JF inao washiriki ambao ni great thinkers haswa sio wale wa matusi na posho. JF hii inapaswa kuwa bora kuliko ilivyo sasa, na inaweza kuwa hivyo tu ikiwa watu wake wanafanya na kusema yale ambayo great thinkers wanatakiwa kuyasema na kuyafanya.
 
Huzuni ipo but serikali ndo imesababisha yote hayaa kwa nn isingejenga bomba la gesi mtwaraa??،na ile ni haki yaoo,
 
Wewe Tandaleone na wenzako wa buku saba mnahitaji elimu ya checkechea tu ili kujua ishu ya mtwara, lkn sababu mpo na mtaalamu mulungo/tamim najua mna vyeti vya mambo yetu yale, embu muwe mnasoma taarifa na kupata uzoefu wa nchi nyingine na sio kufikiria matumbo yenu kwa kipato mnachoingiza kwa post! ishu ya gesi kugomewa na wanamtwara haikuanza jana ni muda wabunge wa upinzani kwa muda mrefu walipigia kelele bungeni kuhusu mgawanyo wa mapato, mwaka jana wananchi wa mtwara waliandamana sana kupinga, hadi baadhi wakaja ikulu ya dar, na kama utakumbuka vizuri kuna BIBI alilaani kwamba wakichimba tu bomba litatowa maji na sio gesi........., akatumwa mn'goa kucha mmoja kwa bibi wananchi wakamshtukia nusura auwawe akakimbia gari lake likachomwa moto. wananchi wa mtwara wakaendelea kuwa na msimamo kwamba gesi haitoki..kwa hiyo yanayofanyika ni ya wanamtwara wenyewe na sio msukumo toka nje.

1. Silaha za wananchi ni mabomu ya uvuvi,mishale na mapanga ambayo yapo kila siku,miaka yote hayajaagizwa kutoka nje ya nchi.

2. Hivi wewe unataka kuniambia mwananchi akidai haki zake eti "katumwa na wachochezi'' kana kwamba yeye hana akili timamu.......unataka kutuambia hata wazee wetu wapigania uhuru waliambiwa na watu wa nje kwamba nchi zetu zilikuwa zinanyonywa na wakoloni.

3. Hata kama makosa yalifanyika nyuma kwa mikoa ya tabora,shy,mza,mara (migodi ya dhahabu na almasi) sio lazima turudie mtwara.

4. Ingekuwa Mza,A-town,Dar,Moshi serikali ya CCM ingekuja na jibu rahisi kwamba CDM inachochea, ingekuwa Zenj CUF wangetuhumiwa, Sasa mtwara tunadanganya ''mkono wa nje"

5. Wewe kama Mtz em pita vijiwe vya watu wa kawaida Kariakoo,manzese,tandale,Tmk,Kndoni,Mza,Arusha,Musoma,Bk jaribu kuuliza au kusikiliza maoni ya wananchi ndio uende kuwaambia wakuu wako pale lumumba.

6. Tunataka masahihisho yaanzie mtwara, mji ufanane kama miji maarufu ya uchimbaji wa madini kule africa kusini tusirudie makosa ya mwanza,Shy,Tbr,Mara nk.

7. Unaposema mtwara ni mbali, unamaanisha mbali na wapi? kwasababu wanaihitaji gesi watalipia gharama za usafiri kuifuata sababu ni adimu.

8. Eti Mtwara hamna wataalamu ni uongo, Nchi yetu haina wataalamu ndio kwanza wameenda shule.......kama hiyo ni sababu bomba lingejengwa kumwaga gesi urusi ndio kuna wataalam.

9. Wasomi wote wako Dar sababu ya ajira na asilimia zaidi ya 90% si wazawa wa Dar, ni matumaini yangu kwamba hata bomba lingekuwa mtwara bado wasomi wangelifuata mtwara kupata ajira nzuri, mbona migodi ya dhahabu haijahamishwa Tbr,Shy nk lakini vijana wasomi kibao wanakimbilia huko kupata ajira nono.

Kwahiyo ni vema kukaa chini na kuja na suluhisho la juu juu, kwa sasa serikali ya CCM haiwezi kudanganya watu, sababu watu wamekufa kahama,mererani,tarime kwa manufaa ya viongozi walafi pasipo hata manufaa kwa mwananchi. Pia wananchi wakipinga usiuite uhaini, tatizo lako na CCM hamjui kwamba hata Polisi na JWTZ ni watanzania na hawafurahishwi dhuluma kwa wananchi...................
 
kaka umeandika katika hali ya huzuni hii inatokana na kusikitishwa kwako na hali ya mtwara, ila tukumbuke kuwa tatizo hili halijaanza jana, je kipindi cha nyuma viongozi wa serikali walienda kutatua tatizo gani? na muafaka upi ulipatikana? kuchomwa moto kwa ofisi za ccm na viongozi wake binafsi hapo hakuna hujuma kwa hiko chama, ila wana mtwara wanaona jinsi gani hiko chama kimewafikisha hapo, wameshatumiwa vya kutosha sasa wamechoka, wana mtwara mawefikia hatua ya LOLOTE NA LIWALO, ila nawahasa serikali wasitumie nguvu ya risasi, mabomu, na kuwakamata vijana hiyo haitasaidia bali itazidi kuchochoea. ifike mahali serikali sikivu basi isikie na ijue kuwa tanzania imebadilika si ya zamani.
 
...........
Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo...
Tandaleone
Ahadi ile ya NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO IMEENDA WAPI?
Tatizo la gesi Mtwara linaletwa na vitu kadhaa ambavyo vyote vinajulikana lakini ninyi mlio na fursa ya kukaa na Mfalme mnaogopa kumwambia;
1. Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010, Ilani ya CCM ilieleza kuwa gesi ya Mtwara haitatoka kwenda Tanzania, kwa maana ya Dar es Salaam. Hili nalisema kwa kuwa Viongozi Waandamizi Serikalini wanasisitiza kuwa gesi ni ya Watanzania wote,wanasahau kuwa ikifanyia kazi Mtwara, itakuwa inawafanyia kazi Watanzania wote. Umeme unaotumika Tandahimba, Ruangwa, Nachingwea, Masasi, Lindi na Mtwara unatumiwa na Watanzania wote, hata kama haufiki Rudewa, Mpanda, Kasulu au Karagwe. Hata gesi ikienda Kinyerezi, umeme utakaozalishwa hautafika Karagwe na huko kwingineko. Umeme huo ni wa gesi ya Mtwara.
2. Aya ya Gesi ya Mtwara ilibidi iwemo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM, maana Watu wa Mtwara waliisha ona kuwa gesi ya Killwa ilipofika Tanzania (Dar es Salaam), iligeuka na kuwa ya Wamarekani na kuuzwa kwa dola za Kimarekani. Swali, kama gesi ni ya WaTanzania, kwa nini iuzwe kwa dola za Kimarekani, tena kwa bei kupangiwa huko huko Marekani, hata inaponunuliwa na Tanesco ambayo ni mali ya Watanzania?
3. Maandiko hayo kwenye Ilani yaliwafanya WanaMtwara wakipatie USHINDI WA KISHINDO katika Mkoa wa Mtwara, Chama Cha Mapinduzi. Kubadilika kwa uamuzi juu ya gesi kunakofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake kunaonekana kuwa ni USALITI WA HALI YAJUU KABISA kwa watu wa Mtwara.
4. Baada ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa taifa wa CCM alirudi Mtwara kushukuru kwa kuungwa mkono kwa KISHINDO, na siku hiyo katika mkutano wa hadhara, akasisitiza kuwa gesi ya Mtwara haitatoka, badala yake itazalisha umeme hapa hapa Mtwara, na umeme huo utatumika Tanzania nzima.
5. Ahadi hizo zilionekana kuwa mwanzo wa UKOMBOZI WA KIUCHUMI kwa Mkoa wa Mtwara maana ukweli halisi ni kuwa mkoa huu uligeuzwa kuwa jela ya kuwaadhibu wafanyakazi wa Serikali ambao ama wamekosea kazini kwao au hawapendwi na mabosi wao huko makazini.
Tandaleone,hujui kuwa mtumishi akipewa uhamisho kuja Mtwara hujiuliza mara mbili mbili kuwa ni makosa gani amefanya mpaka aadhibiwe kwa kuhamishiwa Mtwara?
6.Baada ya shamrashamra za USHINDI WA KISHINDO kwa CCM Mtwara, yakaja mabomu mazito, siyo haya ya leo na jana ya machozi, bali mabomu ya uamuzi wa Serikali juu ya gesi kupelekwa Tanzania(kwa maana ya Dar es Salaam)
7.Kilichoitwa Ukanda wa Kusini, Southern Corridor, kikageuzwa kuwa Bagamoyo Corridor maana viwanda, bandari na uzalishaji umeme umehamishiwa Bagamoyo.
Tandaleone,unaweza kusema kweli, kweli tupu na wananchi tukakusikia?
8. Balozi wa India alipoenda kumsalimia Mwenyekiti wa IPP, yapata miezi miwili iliyopita, alieleza kuwa kuna kampuni ya India inataka kuzalisha umeme, megawati 250 pale Zinga/Kerege, Bagamoyo, mara tu gesi itakapofika hapo Wilayani Bagamoyo.
10. Wataalamu wa Upimaji, Land Surveyors, wamekwisha kamilisha upimaji wa njia ya gesi toka Kinyerezi kufika eneo jipya la viwanda Zinga/Kerege Bagamoyo. Ninaamini hili unalijua.
11. Wananchi tumeshikwa na bumbuwazi kuambiwa kuwa kilichomleta Rais wa China ni kutiliana sahihi ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Bagamoyo! Tandaleone, hii inakuingia akilini? Bagamoyo hapafai kujenga bandari maana mchanga utakuwa unajaa bandarini kila wakati na gharama za kuuzoa ni kubwa mno! Bagamoyo!
12. Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Elimu Bagamoyo kwa kushirikiana na Kampuni kubwa sana ya India, atakuwa anayeyusha mawe ya Chuma cha Pua, iron ore, toka Liganga pale Bagamoyo. Kuyeyusha chuma hicho kunataka nishati ya ama gesi ama makaa ya mawe. Hivyo madini ya chuma yatatoka Ludewa kwa reli mpaka Mtwara. Yatapanda meli mpaka Bandari ya Bagamoyo na kupelekwa eneo la viwanda. Huko madini hayo, iron ore, yatakutana na gesi ya Mtwara na kugeuzwa kuwa chuma, iron ingots.
13. Yote hii ni kuinyima Mtwara fursa ya kuukuza mzunguko wa pesa, ambao haupo (na kuwa chimbuko la waajiriwa wa Serikali, Madaktari, Waalimu, na kada nyingine kuikataa Mtwara kila wanapopangiwa au kuhamishiwa huku). Serikali imeamua kuwa mzunguko wa pesa utakuzwa Bagamoyo, na kamwe siyo Mtwara!

CCM TUACHE UNAFIKI.
NINAKILILIA CHAMA CHANGU CHA TANU
 
Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?

Ni kwa sababu mali za viongozi wa CCM zimepatikana kwa njia ya udanganyifu na kuhujumu rasilimali za nchi hii; hivyo kinachofanyika ni BORA TUKOSE WOTE.
CCM wanavuna walichopanda na wasitarajie kwamba nguvu ya dola inaweza kushinda nguvu ya umma. Watauawa wengi lakini watakaobaki wataendeleza mapambano hadi kieleweke.
 
We have a very serious and huge responsibilities to run the country. Maamuzi yetu yanafanywa kwa kuzingatia uhalisia wa mazingira yetu, siasa zetu na rasimali tulizonazo. Hakuna maamuzi kandamizi ama ya upendeleo ambayo CCM ama serikali yake yanaweza kuya-champion. Ni ajabu na ni muendelezo wa siasa chafu kudai serikali ya CCM inalenga kuitenga na kuionea kusini.

Katibu Mwenezi,

Kweli unataka mdanganya nani hapa baada ya miaka 50 ya utawala leo unapiga propaganda kuwa Kusini haionewi. I can not buy that, mwanafilosofias mmoja alisema huwawezi tatua tatizo ulilosababisha mwenyewe. Pesheni wengine waje kuondoa hii mess kwa taifa. Rushwa na ufisadi mlioupanda utawaangusha
 
Ndugu yangu Tandale One, naungana nawe katika kuhuzunika kwa yale ambayo yametokea Mtwara. Hata hivyo, sioni mwingine yeyote ya kumlaumu au anayepaswa kufikwa na madhila haya zaidi ya CCM na viongozi wake. Hivi madai ya msingi ya wananchi wa Mtwara ni yepi? Na serikali imeyashughulikiaje?
Pinda alipokwenda Mtwara walifikia makubaliano ya kuiacha gesi mtwara. Iweje kipengele hicho kiingizwe kwenye bajeti ya wizara ya Nishati na Madini tena kwa mbwembwe?
Wananchi wa mtwara tumewaandaaje kisaikolojia katika hili? CCM isirudi kulilia huruma ya wananchi, hili wamelitaka kwa muda mrefu hili, sina shaka linatokea sasa. Wananchi wa Mtwara leo sio wale wa miaka ya " Wreath of Father Mayer"., this is a bit new generation.. Korosho imeshindwa kuwasaidia, bandari imeshndwa kuwasaidia, na gesi pia isiwasaidie???
Noo.,
CCM imepanda kiburi, wacha ivune Kaburi..
Makubaliano ya Pinda na wanamtwara yapo bayana tena yakiwa na viongozi wa kaya, viongozi wa kisiasa na hata wa kidini wa mtwara. Makubaliano hayo yanabainisha faida na mafanikio ambayo mtwara kama mkoa utanufaika nayo kutokana na miradi ya gesi, lakini hmakubaliano hayo hayakuwa yakikataza gesi kutoka mtwara na hata neno lenyewe kutoka linatrumika vibaya kwa maana kiasi cha gesi ambacho kitaendesha shughuli zakiuchumi za mtwara ni kubwa na inayokidhi haja kuliko hata itakayosafirishwa kwa ajili ya kufua umeme kwa ajili ya gridi ya Taifa.

Ni upotoshaji wenye nia ile ile ya kuvuruga nchi ndio hasa unapelekea matukio na kadhia hizi zenye kuchafua taswira ya Taifa. Wananchi wa mtwara wanao wawakilishi wanaowaridhia, lakini si tu kuwa kuna wawakilishi, serikali na chama kimefanya juhudi kubwa ya kukutana na kujadili na wananchi wa kawaida kabisa juu ya manufaa yatakayopatikana mtwara. Hivyo hakuna usahihi wa aina yeyote kudai kuwa hawakuandaliwa kisaikolojia.
 
Viongozi wetu hawana uzalendo na nchi,wanajilimbikizia mali tuuuu..nakusahau hata kuleta ka nafuu kidogo kwa wananch.wanatamani sana watanzania tubaki kua wajinga.lakina kwa sasa iv wao ndo tunawaona wajinga.
Yote yanayo tokea ssiv ni mavuno yao.
 
TandaleOne
1.Kumbe na nyie manogopa kufa?
2.Hofu mliyonayo ni robo ya hofu na maumivu waliyoyapata Kubenea,Ulimboka na Kabanda
3.Mungu ni mwema sana,Kinachowasumbua ni Damu na mateso ya hawa Kubenea,Ulimboka na Kabanda
Na mungu wetu atawalipizia hapa hapa duniani,hivi mnafikiri mtakuwa salama kwenye magari yenu ya kifahari na maheaklu yenu?mtakuwa na hofu na mtalala nje kama wanavyolala maskini na ombaomba wengine,Kaeni mtubu dhambi zenu na muache michezo ya kuwahadaa watanzania,mna kila kitu Polisi na wanajeshi nk,Je watawalinda mpaka mkienda chooni?mna ndugu jamaa na marafiki nao mtawalinda?
Rudini kwenye mstari,kama hamtawatendea haki watanzania mtalala nje kama sisi maskini tunavyolala nje uswahilini kwenye madimbwi ya maji,mbu,harufu za vyoo nk
Mungu ibariki Tanzania.
Turudi kwenye maombi na mungu atatusaidia,hii nchi ni yetu sote,na sio lazima CCM mtawale daima,haiwezekani!
 
Kwanza kwa nguvu polisi walizotumia pale JK anatakiwa apelekwe the Hague au ashitakiwe kama Hosn Mubaraka, Gadafi na wanawe, Uhuru Kenyatta nk
 
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa habari naomba uniambie katika kata ya Madimba Mtwara kuja project kubwa 3 zinahusu nini? na wanachokidai watu wa Mtwara na lindi ni kipi hasa?

Km hata kwa ufafanuzi hawajakuelewa basi wamedhamilia. Hongera sana kiongozi.
 
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .

Hii ni lazima ilikuwa ndoto si dhani km ulichoandika ni suluhu,kwa nini wewe na mafisadi wenzako hamtaki kukaa na wananchi kisa ni hayo mabilioni mliyowekewa uswis? Mnatufanya watanzania wajinga kwa taarifa ni kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaid,huwezi shindana na wananchi ukashinda ,na kwa maoni ya watu wa kusini ni kwamba ccm ndio inaishia huko mtabaki kulalamika oh cuf ,chadema kumbe tatizo ni nyinyi wenyewe.
 
Ulimwengu mzima, mahali ambapo panavumbulika rasilimali fulani, watu wa pale lazima wafaidike kwanza na zaidi, ndio maeneo mengine ya nchi yapate. Wenyeji wa sehemu zenye mafuta wali resist sana baada ya kuona mafuta yanaenda na wao hawafaidiki. Ni wasukuma tu wa Mwanza ndio samaki zao zilichukuliwa,madini yao yakachukuliwa wanaangalia. Serekali ya CCM isipoliona hilo, hata hiyo gas hawataifaidi, wanaweza wakajenga bomba la mafuta likahujumiwa, nani atakuwa amefaidi? Waweke wazi mikataba ya gas kwanza kama wameshachukua 10% waseme

Katika kila jambo tunategemea mazuri zaidi ya mabaya, hawa walioamua kupigana naweza sema hawajatumia njia sahihi ya kutatua matatizo, kuna njia nyingi , sio kuchoma nyumba ambayo ni mali ya binadamu mwenzako, sio kupigana na polisi bali, vyombo vya habari, maongezi yakinifu na wataalam, pamoja ka kufuta sheria za nchi kama sheria ya kupigana ipo, watu wa MWANZA na MUSOMA wangeshapigania madini yao na samaki wao mguga za wanyama na ardhi lakini watu wa mtwara wamejengwa kisiasa hasa siasa chafu ya ukanda na kusahau TANZANIA NI TAIFA MOJA. watu hawa maadili zero

UNETHICAL PERSON IS HUMANLY WEAK AND PSYCHOLOGICAL UNHEALTHY <SOCTRATES>
 
Ni lazima tukubali kwamba kupitia njia mbalimbali za kitechnologia wananchi wa sasa sio sawa na waleeee wa enzi za zidumu fikra... Tatizo la Mtwara linazaliwa na hoja kwamba rasilimali za asili zinaondolewa na kupelekwa sehemu nyingine(bagamoyo) ambako gesi itatumika kuzalishia umeme na mambo mengine. Hoja hii inapewa nguvu na wazo kwamba badala ya kujenga mitambo ya kuzalishia umeme Mtwara mitambo hii inaenda kujengewa sehemu nyingine baada ya kusafirishwa kwa bomba lililogarimu matrilioni ya dola za marekani. Kuna mawazo kwamba mipango ya awali ya matumizi ya gesi iliyokuwepo imegeuzwa kwa faida ya watawala wa sasa.
Hoja hizi ni muhimu zikajibiwa na serikali kwa kutoa maelezo yanayoeleweka na yenye uhalisia kwani raia hawa wanaochoma matairi hawataukubali uongo na puruzai za kisiasa.
Binafsi naumizwa na yanayoendelea Mtwara na natamani busara ambayo sioni kwa watawala wetu itumike kuepusha maafa yatakayo tuzidishia umaskini wetu.
N:B NIMESIKIA KUPITIA REDIO MBAO KWAMBA KWA MUDA MREFU SASA MELI KUBWA ZA GESI ZIMEKUA ZIKISAFIRISHA RASILIMALI HII KUTOKA MTWARA. WAKUU KUNA AJUAE KUHUSU HILI? KIPATIKANACHO KUFUATIA USAFIRISHAJI HUU NI KWA FAIDA YA NANI?
 
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...

Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..

Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
Akili yako fyatu na walio ku like ni fyatu
 
Ingekuwa njama TISS wangeisha inote mapema au ndo una assume hawapo?
Kama Democrasia ni power in the hands of people sasa why serikali sikivu ya CCM isikae na hawa watu kujua tatizo nini?
KUMBUKA NI HAWA HAWA NDO WAPIGA KURA WA 2015
 
Leo asubuhi ya saa mbili na dakika 56 (08:56:16am) nimepokea ujumbe wa simu kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, ambae kwa cheo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Ujumbe wenyewe ni huu ufuatao:


Ujumbe huu uliniongezea simanzi na majonzi niliyonayo juu ya maafa mbalimbali yaliyojitokeza katika vurugu za Mtwara jana. Simanzi hii ilitokana na kuona hali ya unyonge, woga na wasiwasi mkubwa walionao viongozi wenzangu wa Chama, wasiwasi huo hautokani na woga wa kitoto bali kutokana na hatari wanayoiona mbele yao ya kuwindwa, kushambuliwa na kufanyiwa hujuma na matendo mengine ya kudhuru mwili.

Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo.

Maana ya maneno mawili ya mwanzo ya yaani hujuma na uhaini yanafuatana kwa maana hujuma inaweza kutumika kama mkakati wa uhaini. Uhaini ni tendo la kusaliti nchi, serikali au mfadhili; uasi. Hujuma ni shambulio ama vamio: fisidi, kuvuruga ama kuharibu.

Maana ya kipengele cha tatu ambacho kimebeba maneno mawili harakati na siasa, ama siasa ina maana ni mfumo wa mawazo yaongozayo utawala wa serikali ya nchi tafsir nyingine ni utaratibu wa utekelezaji au uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo linalotarajiwa.,na maana ya neno la mwisho yaani harakati ni juhudi zinazoafanywa na watu kwa ajili ya kufikia lengo fulani, bidii, jitihada.

Katika tafsir hizo tatu, kinachoendelea mtwara hivi sasa tunakitoa kabisa katika maana halisi ya harakati za kisiasa, kwa kuwa maana ya harakati za kisiasa ni juhudi za kupanga utaratibu wa mfumo wa mawazo yaongozayo (ama yanayolenga kuongoza) utawala wa serikali ya nchi.

Kwa maana ya Hujuma kuwa ni shambulio, kuvuruga ama kuharibu ni sahihi kwa upande mmoja kuwa hiki ndicho kinachoendelea mtwara lakini kwa tafsir ya uhaini ndiyo hasa inayoelezea kinachoendelea Mtwara.

Ndio ni uhaini uliopangwa na kutekelezwa na watu wenye nia mbaya na nchi hii, wasio wazalendo na waliokosa utaifa. Wanaoendesha mkakati wa nchi kutotawalika, kwa kuibua hujuma mbalimbali dhidi ya serikali na chama kiendeshacho serikali hiyo yaani CCM.

Sio ajenda na hoja ya gesi, bali hoja hii imetumika kimbinu kuendesha mkakati huu wa kihaini ambao unawawinda wanaCCM, ofisi zao, mali zao pamoja na serikali yao. CCM ni chama cha siasa kinafanya siasa ya kuendesha nchi hii, vipo vyama vya upinzani navyo vinalenga kuelekea katika mlengwa huu wa kisiasa, lakini wakati mwingine vinapotoka na kuacha Siasa ama harakati za kisiasa na kujikuta wakifanya hujuma na vitendo vingine vya kihaini. Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?

Mkuu, sitaki mung'unya maneno.

Adui mkubwa wa chama chetu na serikali yetu sikivu ya CCM ni UFISADI. Usitafute mchawi wala kuzingizia vyama vya upinzani. CCM itapotambua kuwa nchi hii inaendeswa na siasa ya vyama vingi (demokrasia) , na kwamba ule wakati wa kufanya mambo kwa siri hukupo tena, ule wakati wa kutopenda ambiwa ukweli na hasa kama ukweli wenyewe ni mgumu kwa maana kwamba kukosolewa haupo tena. Wananchi wa Mtwara wanataka uwazi katika mikataba ya Gesi asilia, hawataki kuwa kama wananchi wa Kakola ua North Mara ambao miaka ya nyuma waliishi wakiendesha maisha yao kwa kutegea uchimbaji wa dhahabu, leo wanaishi katika umaskini mkubwa, wanaishi kwa kuombaomba, wanaishi wakiwahudimia ndugu zao waliozurika na maradhi yatokanayo na madhala ya kuwepo kwa migodi ya dhahabu kama silicoss, Tb, Ukimwi, magonjwa mengi yasababishwayo na sumu, majeruhi waliopata wakati wakifanya kazi katika migodi hiyo, mifigo yao kufa kwa kunywa maji ya sumu.

CCM wake up, kuwa chama tawala haina maana munaweza kutuamulia kila mlitaklo nyie. Demokrasi ni pamoja na kuwasikiliza minority. Mtwara is simple NGUVU YA UMMA.
 
Back
Top Bottom