Tausi Mzalendo
JF-Expert Member
- May 23, 2010
- 1,471
- 722
Tuna watu wamesoma, wana madigiriii kibao!
Kazi zikitangazwa, hizo applications ukisoma,
hadi raha maana kingereza kingiiiiii!
Kinachoshangaza, "lugha" kwenye izo applications
utadhani kuna mtu mmoja anawaandikia karibu wote!
Kumbe bana, templates za kwenye internet!
Mwite mtu kwenye usaili. Tumia lugha ile ile aliyoletea maombi.
Utachoka maana ni kigugumizi kwenda mbele!Wengi huishia kukosa
fursa za kazi.
Tujikumbushe vitu vichache ili tuboreshe ushindani:
1. Ukimaliza chuo na ukaona kimombo hakipandi, jiandikishe lugha hiyo
mara moja.Nashauri British Council English course hata kama
utalipa zaidi kidogo kuliko kwenda vyuo ambapo utafundishwa
na mtu asiyekijua kimombo vizuri.
2. Ukiwa shule jitahidi kujishughulisha hasa ujue grammar
na structure ya lugha ya kiingereza,
Mapuuza tunayoyaona na kuyasikia na hata kuyasoma hapa
yakiponda lugha ya kiingereza yanawa cost watu.
3. Jiandae uwe mahiri kabla ya usahili.Epuka kudesa ma template
ya internet na kuweka mbwembwe nyiiingi kwenye application letters kama hivi:
"Excellent in analytical and writing skills, with fluency in English"
huku ukijua kabisa lugha hii ni utata mtupu kwako!Andika barua
simple ujieleze kwa lugha yako mwenyewe!Bora hata uandike kwa kiswahili fasaha!
4. Kuna watu wanaamini ati kazi kama uhasibu au udaktari hazihitaji kuwa mahiri kwenye lugha.
Huu ni upotoshaji.Hamna kazi isiyohitaji kuandika taarifa au kuwasiliana kimaandishi.
Nani ana muda kumsimamia mtu mzima kama mwalimu wa lugha na mwandiko shule ya msingi?
Umahiri ni pamoja na kuweza ufanya kazi zako zote with minimum supervision.
Tujitahidi basi ili tuweze kushindana kwenye soko la ajira.