mtoto mdogo sana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2020
- 460
- 1,337
Habari za wakati huu.
Natumai Wote wazima, mimi pia.
Kwa wenye changamoto za kiafya nawatakia nafuu ya mapema.
Bila shaka huu ni uzi wangu wa tatu, wenye maudhui haya ya kutafuta kazi. Lakini nafsi inaniambia nisichoke kue.delea kutafuta.
Mimi ni mhitimu wa Shahada ya Elimu jamii (Bachelor of Arts with Education) na nimefanya "kozi" za Linguistics na Literature hali inayonipelekea kuwa mwalimu wa Masomo ya Lugha ya Kiingereza, yaani Sarufi na Fasihi ya kiingereza.
Ninao uzoefu kufundisha japo sio sana ila pia muda mwingi tangu nilipomaliza masomo yangu ya chuo kikuu nimekuwa nikifanya shughuli nyingine tofauti na ualimu kutokana na Stadi mbali mbali nilizozipata kadiri nilivoishi.
Mbali na ualimu ambao ndio kada yangu niliyosomea na kubobea. Pia ni
Graphics Designer
(Natumia Photoshop na Illustrator)
kwa kipengele hiki pia nina uzoefu na uwezo mzuri sana. Ni Adobe Verified User na nimekuwa niki-design tangu 2018. Kwa hiyo. Najua viziri nachokifanya
Sales and Marketing
Kipengele hiki nina uzoefu nacho kwa muda pia. Nikiwa chuoni nilikuwa University Sales supervisor. Nilipata uzoefu na nikajifunza mbinu mbali mbali za kimauzo. Hata baada ya masomo. Niliporudi mtaani nilikaa duka fulani na nilifanya kazi kwa weledi mkubwa huku nikipewa mrejesho chanya juu ya uwezo wangu wa kuhudumia wateja. Pia stadi ya usanifu wa picha (graphics) hukipa kipengele hiki nguvu.
Shughuli Za "steshenari"
Ninao uzoefu wa utumiaji wa vifaa vya uchapaji uuzaji na ubunifu wa huduma za ki-steshenari. Nimefanya kwa muda. Ukizingatia pia Graphics ndio huipa thamani sana kazi hii lakini ninajua na uzoefu wa kuendesha mashine na vifaa vyake.
Huduma kwa Wateja
Nina uzoefu wa kazi hii. Nimefanya na naijua vema ambapo nilikuwa nahudumia wateja wa nchi tofauti tofauti kwa njia ya Email, mifumo ya kimtandao kupitia tovuti, Simu na kwa njia ya WhatsApp na meseji za kawaida. Uwezo wangu wa kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha na kushughulikia matini kwa muda uliniongezea sifa kipengele hiki.
Web Designing.
Waswahili husema "mtanga na jua hujuwa". Katika shughuli zangu mbali mbali nilipata nafasi ya kujifunza jambo hili japo najua lugha 3; HTML, CSS na JAVASCRIPT. Hizi angalau zinanifanya kutengeneza na kusoma mifumo ya kimtandao aghalabu kutatua changamoto zilizopo kwenye mifumo na domain mbali mbali.
Amini usiamini, pamoja na hayo yote. Leo nipo hapa sijapata ajira ya kudumu zaidi ya vibarua vya muda mfupi visivyokuwa na mkataba ambavyo hata hivo huisha baada ya muda.
Naamini ipo siku mtu atausoma uzi huu. Atagundua potential yangu na ataguswa kuniunganisha na mhitaji wa huduma au kazi nazozifanya.
Kuhusu umri wangu ni wa katikati ya miaka ya 20 na 30 na nilimaliza masomo ya chuo kikuu mwaka 2020.
Mimi ni mwaminifu na sina tamaa wala tabia za kiuharibifu. Huishi au kufanya kazi na mtu sawasawa na mfumo nilioukuta siku ninapokutana nae. Sio mjuaji wala mkosoaji.
Kama una kazi au kibarua.
Nipo hapa.