Ugumu wa kuomba msamaha

bonem

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
235
55
Habari za Jumamosi ndugu wanajukwaa,

Ninaomba kwenda kwenye swala langu kama ilivyotambulishwa na kichwa cha habari hapo juu. Kwanini watu wengi ni wagumu kuomba msamaha hata baada ya kuelezwa kosa lao na kuthibitishwa kwamba wamelifanya.

Kama unabisha basi tuambie ni lini mara ya mwisho kwako kuomba msamaha. Tujuzane wakuu, kwanini kuna ugumu wa kuomba msamaha.
 
Mimi huwa ni mwepesi sana wa kuomba msamaha
Lazima uelewe maana ya Msamaha ni nini. Sio kutamka tu pasipo kutoka moyoni.

Msamaha unaotoka kwenye nafsi huwa ni dhambi kubwa sana na mara nyingi humfanya mtu kurudia kosa lile lile kila mara.

Msamaha wa kweli hutoka juu ya Hisia za mtu, sio chini ya Hisia za mtu.
 
Kumuomba mtu Msamaha sana ni Kujibebeleza ...makosa mengine sio ya kuomba msamaha hata kuuchuna pia Jibu.
 
Kuomba msamaha ni kukiri uovu uliofanya.
Kwaiyo kama kuna ugumu inategemea na kosa lenyewe.
 
Shetani Lucifer ndiye muasisi wa dhambi na suala la kutokuomba msamaha, na watu wengi wana hiyo spirit (roho) ya Lucifer a.k.a sheteni. Maana ktk maandiko, hakuna hata sehemu inayooneshwa baada ya kukosea shetani aliomba msamaha, hivyo hivyo hata Adam hatuoni sehemu aliyoomba msamaha baada ya kukosea kwenye bustani ya Eden, vile vile hata kwa mkewe Eva (a.k.a Hawa), hakuomba msamaha, japo kuwa Adam alipewa masharti ya kwenye bustani na yeye kumueleza hayo masharti mkewe ila baada ya anguko hawakuomba msamaha, ila Mungu tu aliawaonea huruma maana kuwaangamiza ingekuwa ushindi kwa shetani.

Kwa hiyo ukiona mtu anakuwa mgumu wa kuomba msamaha ujue Lucifer (shetani) spirit (roho) imemkalia kooni sana. Na ndiyo maana hizo roho kwa sehemu kubwa wanazo wanawake, wanawake huwa hawasamehi kwa sehemu kubwa ila huwa wanamezea, ila wanaume ni tofauti, wao husamehe na ni wawazi. Na ndiyo maana kwenye makanisa ya wokovu, ni nadra sana kukuta wanaume wanaanguka kwa mapepo, ni wanawake tuuuuuuuuu!
 
Hata marekani juzu Obama alishidwa kuiomba msamaha JAPAN juu ya kuipiga Hiroshima lakini ni Rais wa kwanza kwenda eneo la Tukio na kuweka Maua ya kumbu kumbu...msamaha inategemea aina ya kosa na Tukio
 
Mtu anaweza kukiri kosa ila sualala kusema NUSAMEHE likawa mzigo mkubwa kwake. Tatizo nililoligundua hao watu wa aina hiyo wana KIBURI toka KUZIMU.
 
Lazima uelewe maana ya Msamaha ni nini. Sio kutamka tu pasipo kutoka moyoni.

Msamaha unaotoka kwenye nafsi huwa ni dhambi kubwa sana na mara nyingi humfanya mtu kurudia kosa lile lile kila mara.

Msamaha wa kweli hutoka juu ya Hisia za mtu, sio chini ya Hisia za mtu.
Hakukuwa na ulazima wa kuandika yote haya
 
wewe Mudawote mimi sina roho ya huyo anaejiita lucifa ni akil zangu mwenyew nasisitiza tena sio shetan bt ni mimi sipend jishusha
 
wewe Mudawote mimi sina roho ya huyo anaejiita lucifa ni akil zangu mwenyew nasisitiza tena sio shetan bt ni mimi sipend jishusha
Eminentia shetani hushikilia akili, na Lucifa kashikilia akili zako kama wewe unahiyo tabia ya kutokuomba msamaha. Kwani hata wauaji, wezi nao akili huwatuma kama wewe inavyokutuma na hao wezi au wauaji shetani huwatumia na wao husema akili zao kama unavyosema wewe. Hata Cain alivyomuua kaka yeka Abel, naye alitumia hiyo hiyo akili unayodhani wewe ni akili ila kumbe ni ulghai wa shetani. Pia jina lako la Eminentia ukiongezea D..., yaani DEminentia na kuondoa e Dementia unapata mtu mwenye mental disorder.
 
ha ha ha! huo unaitwa uchokozi mkavu
 
sasa we Mudawote utatoaje herufi kwenye jina la mtu na uongeze herufi nyingne ili isomeke vingne hlo ni pepo chafu liko ndan yako , ata jina lako ukitoa awote ukaweka der inasomeka mudder we ni muuaji
 
Back
Top Bottom