Bei Mbaya
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 2,262
- 843
.
dokta Riwa shukrani sana, kaka yangu alipata dalili kupima Dynapharm akaelezwa vidonda vya tumbo vinamuanza utumbo mdogo. baada ya mwezi akapima damu hospitalini akaonekana hana vidonda vya tumbo. mara kadhaa anahisi dalili za gesi na kuchoma tumboni. Je ni ulcers?
hivi mara nyingi vinauma ukiwa na njaa..ukila vinapoa!
Umejuaje una vidonda vya tumbo? Mara nyingi vidonda vya tumbo huwa na dalili za maumivu ya tumbo kwenye chembe ambayo unayasikia kama yanaendelea mpaka mgongoni, maumivu yake yanakuwa ya kuchoma (kama kiungulia kikali). Kipimo cha kuthibitisha kinaitwa 'OesophagoGastroDuodenoscopy" au OGD, ambapo unaingizwa kama kampira fulani kadogo chenye kamera mdomoni, so kana piga picha kwenye koo (Oesophagus), tumbo na mwanzo wa utumbo mdogo..na vidonda vinaonekana. Pia kipimo cha damu cha kuangalia kama kuna huyo bacteria H.Pylori (serology for H.Pylori)