chonde chonde nafikiri mkuu unataka kuongelea fiterawa!! acha kabisa hiyo mambo huo ni utapeli tu. bora aende hospitali akapate vipimo sahiikumuone Dr.Rahabu buguruni.
Vidonda vya tumbo vya sumbua kinoma, H.pylori Kit mara 2 hakuna matokeo, kikombe cha Babu Lolio kimepita hakuna matokeo chanya, kasi ni ile ile tu, vinatulia na kukamata tena, pengine vinasabisha kichwa kiwe na mawenge, mwili kuuma hovyo, kukosa stamina, moyo kwenda mbio, kuhisi hasira zisizo na msingi...... Maoni na Ushauri Tafadhali!!!
Dah huo ni uchoyo kwani dawa ina siri bana we mwaga hapa tusikie wote au unatumia maruhaniWasiliana na mimi dawa ipo utapona kabisa! Nilikuwa na vidonda serious hujapata kuona! Siku hizi natwanga maharage kama kawa! Tafadhali niandikie private email nitakupa contact zangu
Hii ya mkojo naweza kujaribu. Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nikiumwa macho nilikuwa natumia mkojo kunawa, mara moja tu napona. Yaani mimi vidonda vya tumbo vimeweka kambi. Dawa ya feterawa nimetumia lakini wapi. Kuna kipindi nilitumia cimetidine nikapona na nikawa nagonga bia, harage n.k. Vilikuja kurudi kwa kasi, nikatumia cimetidine but wapi, dawa za kienyeji nimebadilisha kama tano hivi. Maumivu makali kweli tumboni na kifuani kama vinawaka moto. Kuna daktari kaniambia nikapime next week ila nisile nyama siku tatu kabla. Nikikuta bado ni ulcers nitatumia mkojo na hope nitapona.
Kuna dawa nilitumia mimi na nikapona!
Kwa kikurya inaitwa "matotonia maiso",...ni kama majani flan hivi,waswahili wanaita vinasa nguo,..ukitembea kwenye nyasi kama yapo basi yanatoa vidude flani hivi vina nasa nguo kwa wingi!
Sasa basi,unachuma najani yake,unayatwanga kisha una loweka kwa masaa kama ma2 hivi!
Kunywa kama unakunywa maji,hata ukihisi kiu tumia kama maji ya kunywa tu!
Kila dawa unayo andaa itumike ndani ya siku hiyo pekee,ndani ya week1 kama vidonda sio vikali sana vitaisha,au kama ni vikali ongeza hata week2 au tatu!
Onyo:
1.ni majani na sio mizizi,mizizi yake ni tiba ya kitu kingine na sio vidonda vya tumbo!
2.usi chemshe,(ukichemsha ni dawa ya kitu kingine),..loweka tu