Ugonjwa wa Vidonda vya koo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Vidonda vya koo

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,012
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Uvimbe kooni husababishwa na mambo mengi na mara nyingi huwa haisababishi shida kubwa sana.Ukifungana mapua, makamasi hupitia kooni na hivyo basi kusababisha uvimbe.Baridi kavu inaweza pia kufanya koo likauke na mtu ahisi likiwashawasha.Unaposhikwa na mafua, pia unaweza kusababisha kidonda kooni kinachoweza tu kutibiwa na dawa.


  Jinsi ya kutibu vidonda vya kooni:

  • Sukutua maji ya chumvi yaliyo vuguvugu
  • Mumunya dawa za koo, usiwape watoto inaweza kumnyonga akimeza kwa bahati mbaya.
  • Muulize mfamasia wako akuuzie kipulizo (spray) cha kutuliza uchungu kooni.
  • Ikiwa koo linawasha au limekauka, pumua mvuke wa maji moto itakusaidia.

  Muite daktari ikiwa:

  • Umefura tezi za limfu shingoni.
  • Una mabakabaka meupe huko nyuma ya koo lako.
  • Kwa gafla tu unashikwa na kuumwa na koo huku ukiwa na joto jingi.
  • Koo linavimba na kuuma zaidi ya juma moja.
  • Ukishindwa kunywa chochote umu hatarini mwa kuishiwa maji mwilini.
  • Huku mbele kwa shingo lako pia kumevimba pamoja na koo lako
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,012
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Tiba ya vidonda vya koo

  chukua Vitunguu maji kiasi kumi au vinane, uviponde halafu Uchanganye na maji kiasi kikombe cha chai kimoja Ukoroge viziru Uvichuje halafu Unywe vijiko vitatu kila siku asubuhi, mchana na jioni vijiko vitatu.
   
 3. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  • Ikiwa koo linawasha au limekauka, pumua mvuke wa maji moto itakusaidia.
  • koo langu linawasha ngoja nikajaribu nauhakika nitapona maelezo yako ni full tiba
   
 4. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mahali pasipokuwa na doctor. Where there is no doctor.
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huwa unaingia kunako chumvini?
   
 6. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2013
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,550
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  mimi huu ugonjwa unajirudia kila muda kukiwa na baridi, mafua kooni hua napata kweli
   
 7. Bintiwangara

  Bintiwangara JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2014
  Joined: Jun 30, 2013
  Messages: 525
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  dah,nashukuru sana,maana hata ndugu yangu tangia juzi analalamika kuhusu maumivu ya koo,akisema anahisi kama anakidonda kooni,ngoja nimwambie atumie vitunguu saumu,
   
 8. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2014
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,404
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kazi kwenu wazamiaji
  MziziMkavu anazidi kuwatafutia tiba ya koo zenu zilizoambush dhid ya wadudu wakali
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. The Intelligent

  The Intelligent JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2014
  Joined: Dec 27, 2013
  Messages: 2,501
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Ni vitunguu maji, sio saumu.
   
 10. Bintiwangara

  Bintiwangara JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2014
  Joined: Jun 30, 2013
  Messages: 525
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ok nashukuru kwa kunisahihisha The intelligent
   
Loading...