Sir Lindege
Member
- Sep 10, 2013
- 35
- 181
Huu ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria aitwaye Corynebacterium diphtheria. Huenea kwa njia ya kumgusana au kushika vitu ambavyo mgonjwa ameshashika. Pia huenea kwa njia ya kukohoa na kupiga chafya. bacteria hawa huishi katika sehemu za Pua,Ulimi na koo la hewa.
VISABABISHI VYA DONDA KOO
- Kutokupewa chanjo ya kuzuia ugonjwa huu huitwa DTP
- Kushambuliwa na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili kama HIV, kisukari. TB
- Kuishi sehemu ambayo mazingira ni machafu
- Kuishi sehemu yenye watu wengi.
- Homa
- Kutetemeka baridi
- Kuumwa tezi za shingoni
- Vidonda vya kooni
- Ngozi kuwa na rangi ya bluu
- Kushindwa kuona vizuri
- hupewa dawa kwa ajili ya kushusha homa kama paracetamol
- hupewa dawa za antbiotics kama erythromycin na peniccilin
- Na matibabu mengine.
- Hakikisha kwamba mtoto anapata dozi kamili ya DTP akati anazaliwa ili kumwepusha na kumkinga na ugonjwa huu.
JINSI YA KUTIBU DONDA KOO ISIYO KALI (MINOR SORE THROAT PAIN) Na Beatrice Githiri-HLH
Mara nyingi hili tatizo linatupata na tunadhani ni mafua japo inaweza kuwa shida nyingine. Tunaweza kutibu au kupunguza dalili zake kwa kufuata maelekezo nitakayoyatoa. Endapo utapata dalili zifuatazo au ukiwa na hili tatizo ni muhimu umwone daktari mara moja. Homa Kichefuchefu Kutapika Tezi za shingo kuvimba Kushindwa kuhema au kumeza Tezi zenye usaa ( tonsils with pus) Maumivu makala ambayo hayapungui Jinsi ya kupunguza maumivu
1. kunywa vitu vingi vya majimaji Kuwa na maji mwilini ya kutosha kunasaidia kulainisha makamasi hivyo kuwa rahisi kutoa kikohozi au makamasi.
2. sukutua kwa maji ya vuguvugu ya chumvi Changanya kijiko kidogo cha chumvi na maji ya vuguvugu glas1 moja kisha sukutua, hii inasaidia kupunguza makamasi au kikohozi kwenye koo.
3. mumunya pipi kali au tafuna bubblish isiyo na sukari Kumumunya hivi vitu kunasaidia mate mengi kutoka au kutengenezwa hivyo kusafisha koo lako
4.Jaribu dawa za maumivu Nunua dawa za kupunguza maumivu kwa mfano brufen au paracetamol au nyingine.
5. Pumzisha sauti yako Ikiwa donda koo linahusisha njia ya hewa ,epuka kuongea sana kwa sababu itazidisha muwasho na waweza kupoteza sauti kwa mda.
6. Hakikisha hewa sio kavu Hakikisha hewa sio kavu ili kupunguza muwasho.
7. epuka hali ya hewa chafu Epuka uvutaji wa sigara au kukaa kwenye chumba chenye moshi au sehemu yenye harufu kali. Kama maumivu yataendelea nenda Hospitalini au kituo cha afya kilichokaribu