Ufafanuzi wa jumla kuhusu vidonda vya tumbo

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
VIDONDA vya tumbo ni mojawapo ya ishara za mwili kuanza kuishiwa maji, ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo.

Kwanini vidonda vya tumbo ni ishara ya mwili kuishiwa maji?

Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.

Kwa sehemu kubwa miili yetu huishiwa maji kutokana na sisi kusubiri kiu ndipo tunywe maji. Ndiyo, haupaswi kusubiri kiu ndipo unywe maji, kiu ni ishara iliyochelewa ya mwili kuhitaji maji.

Akili ya kawaida inaniambia nikiwa na bustani ya mboga mboga au hata maua nitakuwa nikiimwagilia maji mapema asubuhi au jioni wakati jua tayari limezama na si mchana wakati wa jua kali, kadharika maji yakiisha ghafla kwenye injini ya gari ndani ya mwendo mrefu siwezi nikashuka tu kwenye gari na kuongeza maji kwenye injini!, ni lazima nisubiri injini ya gari ipowe ndipo niongeze maji mengine.

Tuendelee na vidonda vya tumbo …

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye alkalini katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja katika kila watu kumi anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Dalili za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na

Kuchoka choka sana bila sababu maalumKuuma mgongo au kiunoKupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsiaKizunguzunguKukosa usingiziUsingizi wa mara kwa maraMaumivu makali sehemu ya mwiliKifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kaliKichefuchefuKiunguliaTumbo kujaa gesiTumbo kuwaka motoMaumivu makali sehemu kilipo kidondaKukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuziKukosa hamu ya kulaKula kupita kiasiKusahahu sahau na hasira

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline.

1. Asidi iliyozidi mwilini

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili.

Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, n.k.

2. Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili.

Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili au mawazo yatokanayo na shida za maisha.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu waliopewa talaka na wale wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui.

Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na adui.

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.

Kadiri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi.

Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.

Dalili za mtu mwenye mfadhaiko

Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko. Dalili hizo ni:

Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote,kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi,kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoaKupoteza hamu ya chakulaKukosa usingiziWasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia kwa ujumlaKupoteza kumbukumbu au hali ya kusahausahau na kushindwa kuamuaKughadhibishwa na vitu vidogo, yaani mtu kitu kidogo tu ameshachukiaKujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.

3. Sababu ya tatu inayosababisha vidonda vya tumbo ni Haraka haraka

Maisha ya kisasa yanataka haraka katika kazi nyingi tuzifanyazo kila siku, ni lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba katika shughuli zako za kila siku pia husababisha matumbo nayo kubanana.

Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: “Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, au nasikia kiungulia baada ya kula”. Haraka haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.

Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani.

Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.

Ili kuepuka kufanya kazi zako kwa hali ya uharakaharaka unashauriwa kupanga kabla ni kazi gani na gani utaenda kuzifanya siku inayofuatia kwa kuziandika kabisa katika karatasi au kitabu maalumu kiitwacho kiingereza diary au kumbukumbu za kila siku kwa Kiswahili na mhimu ni uwe na kiasi kwa kila jambo kwani si lazima umalize kazi zote leo.

4. Sababu ya nne ya kutokea vidonda vya tumbo ni ulaji wa Vyakula vya kusisimua

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni.

Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.

5. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni.

Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

Matibabu ya vidonda vya tumbo

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.
 
majani ya mpera unayafanyaje? nimeshatumia dawa nyingi za hospital na za asili kama juice ya majani ya mashika nguo, juice ya kabichi na karoti, maji ya aloevera na asali, dawa za kimasai ila wapiiiiii
Akikujibu nitag mkuu
 
majani ya mpera unayafanyaje? nimeshatumia dawa nyingi za hospital na za asili kama juice ya majani ya mashika nguo, juice ya kabichi na karoti, maji ya aloevera na asali, dawa za kimasai ila wapiiiiii

Badilisa saikolojia yako

Niliumwa hii kitu mpaka nikawa naharisha damu

Nikapona kwa mambo matatu

Saikolojia
Diet
Na dawa ya fiterawa ya Rahabu

Mpaka leo nadunda
 
Badilisa saikolojia yako

Niliumwa hii kitu mpaka nikawa naharisha damu

Nikapona kwa mambo matatu

Saikolojia
Diet
Na dawa ya fiterawa ya Rahabu

Mpaka leo nadunda
Ulijuaje haya mambo mambo matatu yalikuponya kwa pamoja ...kwa sababu ,Saikolojia inaponya,dawa ya Feterewa ilikuwa inaponya...sijui siku hizi hata Dietting inaponya! Ungesema ulifanya /kutumia vyote kwa pamoja ila huna uhakika nini kilikuponya! au
 
Ulijuaje haya mambo mambo matatu yalikuponya kwa pamoja ...kwa sababu ,Saikolojia inaponya,dawa ya Feterewa ilikuwa inaponya...sijui siku hizi hata Dietting inaponya! Ungesema ulifanya /kutumia vyote kwa pamoja ila huna uhakika nini kilikuponya! au

Niliachana na sawa
Nikaendelea na saikolojia na diet nipo vizuri mpaka leo

Hauoni wagonjwa wengi wanapona kwa muda wa matumizi ya dawa
Wakiachana nayo wanaanza kuumwa upya?
 
Back
Top Bottom