UGONJWA WA KUHARA DAMU (COCCIDIOSIS) KWA KUKU, UTAMBUE NA NAMNA YA KUTIBU & KUKINGA

  • Thread starter Helicobacter pylori
  • Start date

Helicobacter pylori

Helicobacter pylori

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Messages
403
Points
250
Helicobacter pylori

Helicobacter pylori

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2013
403 250
img_5770-jpg.1090770

Ugonjwa huu hushambulia kuku wa Umri wote, lakini Vifaranga na walioko chini ya miezi mitano wapo kwenye hatari zaidi. Husababisha vifo mpaka 50% ya kuku wote waliougua.

Coccidia ndio wadudu wanaosababisha ugonjwa wa kuhara damu, wapo kwenye kundi la Protozoa, jamii ya Eimeria spp, wadudu hawa huathiri wanyama karibia wote.

Wadudu hawa wamegawanyika kulingana na Sehemu wanayoshambulia kwenye utumbo.
1. Ceacal coccidia(appendix/ceca/kidole tumbo) kuku ana vidole tumbo viwili, basi wadudu hawa wa coccidia (Eimeria tenelle) hushambulia na ndio chanzo cha kuhara damu.
img_5769-jpg.1090773

img_5773-jpg.1090776


2. Intestinal coccidia (Utumbo mwembamba) Eimeria necatrix ndio pamoja na wengine ndio hushambulia utumbo mwembana, damu huchanganyikana na chakula ndio maana choo huonekana cha Kahawia/ugoro.
img_5772-jpg.1090774

img_5775-jpg.1090777


MAMBO HATARISHI
1. Msongamano wa kuku wengi ndani ya banda.
2. Uchafu(unyevu nyevu wa matandiko, vyombo vya chakula na maji)
3. Kuingia na kutoka bandani pasipo Utaratibu (Biosecurity).
4. Lishe duni

MAAMBUKIZI/KUENEA

Kuku hupata maambukizi kwa kula vimelea vya wadudu hawa iwe kwenye maji, chakula, kinyesi, chini kwenye matandiko.
Ugonjwa unaweza kutokea pasipo dalili kuonekana na hii Husababisha hatari ya magonjwa nyemelezi.

DALILI ZA UGONJWA.
1. Kuzubaa/kusinzia
2. Kujikunyata na kushusha mabawa
3. Kukosa hamu ya kula
4. Kupungua uzito/utagaji/kudumaa
5. Manyoya kusimama/rafu
6. Kuharisha choo cha kahawia/ugoro
7. Kuharisha choo chenye rangi nyekundu(damu)/nyeusi
8. Kuku kufa(Vifo).
img_5771-jpg.1090778


UTAMBUZI
1. Kwa kutazama dalili na Mazingira pia (Choo chenye damu au rangi ya ugoro)
2. Utambuzi wa Maabara (sampuli ya choo)
img_5773-jpg.1090779


KINGA/KUZUIA
1. Usafi wa vyombo vya maji na chakula
2. Kuhakikisha Matandiko/banda ni kavu muda wote na safi.
3. Kuweka dawa mlangoni, kukanyaga dawa kabla ya kuingia bandani.
4. Kuepusha Msongamano.
5. Kutunza kuku kulingana na rika.
6. Chanjo

Chanjo Hutolewa kiwandani (Hatchary) au Shambani kwa vifaranga wa siku moja(DOC-1~3), Chanjo hii hutolewa kwa kunywa au kupulizia (spray).
Chanjo hii hutolewa mara moja tu kwa maisha yote ya kuku/bata mzinga.
Hutakiwi kutumia dawa yeyote (Antiboitics eg, Amprolium, Tetracycline or Sulpha’s) kwa muda wa siku 30 baada ya chanjo.


MATIBABU
Ugonjwa huu unatibika kwa kutumia dawa mfano. Toltrazuril 25mg, Amprolium (200mg, 250mg), Potentieted sulphonamide (Sulfaclozine SMH 30%, Sulphadimidine-sulphaquinoxaline, Trimethoprim & Sulphadiazine; etc.) kwa muda wa siku 3-5/7 au kilingana na Maelekezo ya Daktari.

MUHIMU: Dawa hizi lazima zitolewe kwa kufuata ushauri wa Daktari maana kuna baadhi ya dawa zimekuwa na athari hasa kwa kuku wanaotaga (hupunguza utagaji).

Imeandaliwa na
Dr. Godwin Mkami, DVM
SipyVet.centre
Kinyerezi-Mbuyuni DSM
+255 764 667 503
 
Helicobacter pylori

Helicobacter pylori

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Messages
403
Points
250
Helicobacter pylori

Helicobacter pylori

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2013
403 250
Vipi kuhusu tetracycline mbona naona wafugaji wengi sana wanazinunua zinatitu magonjwa gani
Tetracycline ni Moja ya Dawa zenye wigo mpana (Broad spectrum) wa kutibu maradhi tofauti tofauti, kiufupi maradhi yanayosababishwa na Bacteria na kwa uchache Protozoa Inafanya vizuri sana.

Ingawa matumizi ya “Tatracycline kama Tetracycline” hairusiwi kwa mifugo maana ni maalumu kwa matumizi ya binadamu, kuitumia kwa mifugo hasa kuku ni inawaweka watumiaji katika hatari ya kupata Usugu wa Tetracycline.

Kuna Tetracycline ambazo ni maalumu kwa matumizi Kwa mifugo mfano CTC-Chlorotetracyclin, Oxytetracyclin n.k na ni vyema Upate Ushauri na maelekezo ya Daktari ama Afisa Mifugo kabla ya kutumia dawa kwa Mifugo yako.
 

Forum statistics

Threads 1,293,761
Members 497,728
Posts 31,152,646
Top