Alejandroz
JF-Expert Member
- Feb 14, 2017
- 327
- 376
Naomba kujifunza yafuatayo kabla sijaingia kwenye ufugaji;
Nafikiria kufuga kuku chotara (Sasso au Kroiler) kisha niwauze baada ya miezi 3 kwa bei isiyopungua 10,000/=
Lakin nimekaa nakupiga hesabu kulingana na ulishaji elekezi kwa kila wiki nikaona nikifuga kuku 100 kwa mwezi wa kwanza nitatumia mifuko 1¼ ya starter, mwezi wa 2 mifuko 2½ na mwezi wa 3 mifuko 3½
Kwa ninavyosikia mfuko mmoja wa kilo 50 bei yake ni 70,000/= hadi 80,000/= hivyo kwa ulishaji nilioutaja hapo juu kwa miezi mitatu nitatumia si chini ya laki 6 na bei yakuku (vifaranga) ni laki 2 hivyo napata jumla ya laki 8 hapo sijahesabu chanjo na madawa mengine
Nikiuza kuku wote (na-assume vifo havijatokea )
100 × 10,000/= nitapata 1000,000/= nikitoa laki 8 napata laki mbili nikitoa madawa na huduma zingine napata faida chini ya laki moja
Kwakupitia hesabu hizi hebu tupeane elimu na uzoefu,, maana naamini wengi wanachukia ufugaji kwasababu ya kukosa taarifa sahihi kama ilivyo kwangu,, kwakweli nimeona sipati faida au niwapi nakosea?
Au bei ya hio mifuko ya vyakula si sahihi?
Au kuchanganya chakula mwenyewe badala yakununua kunapunguza hizo gharama?
Je vipi nikichanganya mwenyewe nitapata matokeo mazuri?
Karibuni tuelimishane namna nzuri yakupunguza gharama za ufugaji wa kuku ili kupata faida nzuri