Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Dawa ni maombi tu. Yesu ndio dawa pekee! Amini nakuambia ukiamini ndugu yako atapona!
 
Pole sana kwa tatzo alilonalo mdogo, mi ninadawa ya asili inatibu tatzo hilo harakasana jitaidi uwasiliane nami nijue jinsi ya kumsaidia huyo kijana kabla ugonjwa haujakomaa.
 
Nenda Muhimbili kuna dawa ambazo zinatuliza, asikudanganye mtu kifafa hakina tiba ya kudumu.
 
Tatzo lenu mnapost vitu halafu hamfatiliiii.Uliambiwa na nani kifafa hakitibiki? Acha kupotoshwa wewe kifafa kinatibika kama mgonjwa atapata huduma mapema kabla ugonjwa haujakomaaa,pia ningependa ujue kwanza magonjwa kama hayo hayatibiki hospital yanatibika kwa wataramu wa tiba mbadala, hospital kuna dawa za kutulizatu, ukizubaa ndugu yako atakuwa wa hivyo maisha yake yote, na ujue wagonjwa wengi wa kifafa huishia kuwa kama vichaaa wanakuwa na uoga wa kuwapamoja na wenzao kwa hofu ya ugonjwa.pia usifuate ushauli wa huyo mkeo ukimtimua ataenda wapi ihari ni mgonjwa? Ugonjwa umemkumba yuko kwako umtimue kisa wifewako? Siku moja unaweza ukaugua na wewe akakumbia hana utu ndani yake.
 
nina mdogo ang anaumri wa miaka 19 amepatwa na kifafa miezi michache iliyopita. huwa maranyingi humtokea akiwa amelala na kama yuko macho huwakama kapigwa na bumbuwazi then akiamka anacomplain head ache na huamzito cku nzima.. tumehangaika bila mafanikio kwenye maombi ndo usiseme na kunasiku huzimia hata mara 3.. tatizo hili limemfanya kudrop hata darasan na anafikia mahali anakata tamaa ya maisha yake. je tiba yake ipo? naomba msaada
 
Naumia niimempoteza mwanangu akiwa na umri wa miaka mitatu na miezi tisa 2014 kwa homa hii ya degedege . mungu mlaze mahali pema peponi amina(RAZAKI RASHID MOHAMED) zaki sirano..jpg
 
Hivi ugonjwa wa kifafa unatibika kwelI Maana ninamdogo wangu kaugua kifafa akiwa na umri wa miaka 24.
 
Unajua kuna kifafa cha kurogwa na watu Na ambacho sio cha kurogwa, vyote vinatibika, kuna jamaa yangu amewahi pata hilo tatizo kuna mzee mmoja alimsaidia akawa fresh kabisa bahati mbaya yule mzee alishafariki pia kuna binti alikuwa na shida hiyo yeye aliniambia alipata tiba kwenye hizi clinic za tiba asilia na tatizo halijamkuta tena,
 
Nimetembea takiribani hospital 5 kubwa hapa nchini na kutumia gharama kubwa lakin haijasaidia.
 
Nimetembea takiribani hospital 5 kubwa hapa nchini na kutumia gharama kubwa lakin haijasaidia Sijui nifanyaje msaada.
 
hivi ugonjwa wa kifafa unatibika kweli? maana ninamdogo wangu kaugua kifafa akiwa na umri wa miaka 24.

Pole sana mkuu NIKIMU ... kwa kweli kifafa ni tatizo gumu sana si kwa mgonjwa tu, hata familia (ndugu na marafiki). Kifafa kipo kati ya magonjwa ya akili, kwa kuwa kina athari kwenye akili za muathirika. Labda nianze kwa kusema...kifafa mara nying ni 'dalili' ya ugonjwa, kuliko chenyewe kuwa ugonjwa. Kinapotokea kinaonyesha kuna tatizo ambalo limeathiri ubongo wa mhusika. Hivyo ukifika Hospitali lazima wachunguze kilichopelekea kifafa hicho.

Mara nyingi tatizo huwa kuathirika kwa ubongo kutokana na mambo mbali mbali (ajali, kansa, kiharusi (stroke), maambukizi (infections eg Meningitis etc), kwa watoto degedege kwa Cerebral Malaria, minyoo ya kitimoto (Tape worm Neuro-Cysticercosis hili tatizo linatokea sana siku hizi sababu ya kula kitimoto kisichopimwa), madawa au sumu, etc). Kati ya matatizo hayo, yapo yanayotibika na hivyo 'dalili' ya kifafa ikapotea kabisa...na yapo yasiyotibika. Ila mara nyingi tatizo linalosababisha kifafa linaweza lisijulikane ikaishia kuitwa tu 'kifafa (Epilepsy)'.

Matibabu ya Epilepsy mara nyingi ni dawa ambazo zinazuia au zinapunguza kupata epileptic attack i.e ile hali ya kupoteza fahamu, kuanguka, na kukakamaa, kujing'ata na kutoa haja ndogo au kubwa. Na pia kama mgonjwa ameathirika kiakili..basi kupewa dawa za magonjwa ya akili..lakini sio kwamba kinatibika kikaisha kisitokee tena..unless ni kifafa kinachosababishwa na ugonjwa Fulani na huo ugonjwa unatibika.

USHAURI: Mpeleke Muhimbili idara ya magonjwa ya akili karibu na wadi ya Sewa Haji pale atachunguzwa na kupewa huduma stahiki.
 
Muhimbili nimempeleka mara 2 kila akimaliza dozi tatizo linarudi. hata hivyo yeye humtokea usiku kuanzia saa 5-8 tu.
 
Back
Top Bottom