Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Anaweza kuwa na uvimbe kichwani, kuna ndugu yangu ilikuwa inamtokea, walipofanya kipimo cha CT Scan ikaonekana ni uvimbe, baada ya upasuaji, tatizo lilianza kupungua na sasa limepotea kabisa.
 
Ila kwa heshima tu na taadhima naomba hiyo avatar uitoe, unaweza usipate matokeo mazuri kwa ndugu yako kwa sababu ya mambo kama hayo.

I am a spiritual man, I know what I am talking about
Avatar sio tatizo wengi wana picha za ajab kama unataka kumsaidia mtu sio lazima uangalie avatar kwani walionishauli wametumia kigezo gani kama hujui kaa kimya usitafute sababu ya watu kutokunisaidia
 
Avatar sio tatizo wengi wana picha za ajab kama unataka kumsaidia mtu sio lazima uangalie avatar kwani walionishauli wametumia kigezo gani kama hujui kaa kimya usitafute sababu ya watu kutokunisaidia

Tatizo nnalijua, na nimelieleza kwa ufasaha kabisa...ni la rohoni. Kanuni ya kutatua matatizo ni lazima ujue chanzo cha tatizo. Kulala usingizi na kuanza kubehave kama ndugu yako maana yake ni kuwa huwa anapata mashambulizi katika ulimwengu wa roho.

Mtu anapolala, roho yake hailali...rohoni anaanza kukabwa, kupigwa, na kuteswa na viumbe wa rohoni ambao tunawaita mapepo, wewe mwilini utamuona anaweweseka.
Dawa ni kuyatoa hayo mapepo ndani yake na mtu anakuwa mzima kabisa...simple!!

Uponyaji huo unafanywa na Mungu aliyeumba mbingu na nchi, kupitia jina la YESU...kwa kanuni za kiMungu ni makosa kuonesha picha za uchi au nusu uchi ikiwa ni pamoja na kuonesha matiti wazi. Ndio maana nikakuonya kuwa ni vizuri uondoe hiyo avatar ili usiwe na mgogoro na Mungu, the creator of heaven and earth...don't say i didn't warn you!!
 
habari zenu wana jf. Niende kwenye mada moja kwa moja ninaomba kujua zaidi hv kifafa kinaweza kutokea tu mtu akiwa amelala? Nasema hv maana nina mdogo wangu ambye anashikwa na hali ya kifafa akiwa amelala tu, na hali hyo imeanza kutokea akiwa mtu mzima 32
 
miaka 32 tangu kuzaliwa hajawahi pata hiyo hali. Na katika ukoo wetu si wa mama au baba hamna mtu ambye anao huo ugonjwa ila yy wakati akiwa mtoto miaka kama 5 au 6 alikatwa na jembe kichwani na mwenziwe akashonwa ila lile jeraha kovu bdo liko ila kidogo
 
Pole sana ndugu, kifafa ni tatizo linalotokana na sababu kuu kubwa mbili;
1. Kurithi
Hapa mtu hulilirithi toka kwa wazazi/ukoo. Familia yenye kifafa ina uwezekano wa muendelezo wa vizazi vya wenye kifafa.

2. Kuumia ubongo.
Ubongo unaendeshwa na mfumo wa umeme ambao ukiwa disturbed mfano kupitia kujeruhiwa kichwani kunakopelekea brain injury, kiharusi au birth injury huweza kusababisha kifafa.

Hii kitu haitibiki, ila kikubwa ni kuwa karb na muathirika, pia ondoa vitu vya hatari jirani na alipoangukia. Zipo pia dawa za kutuliza hospitali.

Pole kwa changamoto hiyo, ila mtunze nduguyo kwa upendo. Inaonekana alipokatwa jembe alipata brain injury iliyopelekea kifafa!
 
Pole sana ndugu, kifafa ni tatizo linalotokana na sababu kuu kubwa mbili;
1. Kurithi
Hapa mtu hulilirithi toka kwa wazazi/ukoo. Familia yenye kifafa ina uwezekano wa muendelezo wa vizazi vya wenye kifafa.

2. Kuumia ubongo.
Ubongo unaendeshwa na mfumo wa umeme ambao ukiwa disturbed mfano kupitia kujeruhiwa kichwani kunakopelekea brain injury, kiharusi au birth injury huweza kusababisha kifafa.

Hii kitu haitibiki, ila kikubwa ni kuwa karb na muathirika, pia ondoa vitu vya hatari jirani na alipoangukia. Zipo pia dawa za kutuliza hospitali.

Pole kwa changamoto hiyo, ila mtunze nduguyo kwa upendo. Inaonekana alipokatwa jembe alipata brain injury iliyopelekea kifafa!
 
UFAHAMU UGONJWA WA KIFAFA NA TIBA YAKE

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafainayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa Waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu.

Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini?

chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mtoto huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Kuna aina mbili kubwa za kifafa

1) Primarymarygeneralized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2)Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!


Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano

• Uwezo wa kufanya kazi figo

• Uwezo wa kufanya kazi maini

• Kupima maji ya uti wa mgongo

• Kupima Kaswende

• Picha ya ubongo mfano CT SCAN.


mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..

• Kukosa usingizi kwa muda mrefu

• Mianga na miale ya disko

• Unywaji wa pombe

• Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.

• Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}yaani HUDUMA YA KWANZA

• Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.

• Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.

• Usimshike kuzuia mizunguko yake

• Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.

• Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe

• Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.

Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali..

• Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi

• Kutapika sana

• Kushindwa kuona vizuri

• Kupoteza fahamu

• Kichwa kuuma sana.


MATIBABU YA UGONJWA

Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa kwa 100% hospitali, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa basi utapewa utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.
 
Msaidien jaman ukikipata hiki ukiwa mjamzito mama na mtoto wanaweza kupoteza maisha. Pole mkuu, Allah atamsaidia.
 
Imani potofu za kishirikina juu ya ugonjwa wa kifafa zinapelekea ugonjwa huo kuenea zaidi nchini Tanzania hasa Maeneo ya Mahenge morogoro, Hayo yamesemwa leo na Professor William Matuja, aliyefanya utafiti kwa muda wa Miaka mine wiliayani Mahenge Mkoa wa morogoro. Mjadala huo ulifunguliwa na Professor Gadi Kilonzo mbobezi wa magonjwa ya akili muda Mrefu akihudumu MNH. Pia Dr. Tumaini Nangu kawakilisha utafiti wake kuhusu ugonjwa wa kifafa kwenye mkutano huo na kutunukiwa cheti. Kongamano hilo limeudhuriwa na madaktari wengi akiwemo Professor Lawrence Museru mkurugenzi mkuu wa MNH.

Hii nimeileta hapa kufuatia majadiliano marefu kuhusu magonjwa ya fahamu yanayohusishwa na imani potofu, hasa baadhi kusema ni Mapepo au mtu kurogwa. Na wengi wamekuwa wakiwapeleka wagonjwa hawa huko kwa Manabii na kuwaombea bila mafanikio na wengine kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji na kuendelea kutapeliwa bila mafanikio.

Jamii imekuwa na uwelewa mdogo kuhusu magonjwa mbali mbali, na pia baadhi ya hospitali zetu na baadhi ya madaktari wetu wamekuwa wakishindwa kugundua magonjwa hayo, hali inayopelekea wagonjwa kuamini kwamba hayatibiki hospitali na kuhamia kwa waganga wa kienyeji na manabii ambao wote wamekuwa wakiwaaminisha wagonjwa kuwa wamerogwa na kuwahusishwa na mapepo kitu ambacho ni uongo.

Niliwahi kujadili na mkuu Mshana Jr kwenye mada yake moja ihusuyo mapepo, nilieleza kwamba; Tatizo tulilonalo kwenye jamii yetu ni uelewa mdogo kuhusu magonjwa hasa yanayohusu mfumo wa fahamu,pia tunaita magonjwa ya akili. Na pia uduni wa diagnostic tools au upungufu wa hizo diagnostic tools kama CT-Scan,MRI, EEG na Topographic maping, unapelekea madaktari kushindwa kufanya diagnosis sahihi. Pia Madaktari kukosa ujuzi wa kuyang'amua magonjwa haya, kumeifanya jamii kuwa na imani eti kuna MAPEPO, au Kurogwa.

naomba wale woote wenye uelewa wa KIFAFA au Epilepsy wasaidie kuelewesha jamii. Kwa kusoma zaidi, pia niwashukuru MMG: MICHUZI BLOG:
 
Wataalamu wa afya wa kisasa wanadai kifafa (epilepsy) hakina tiba.

Huu ni uongo mkubwa,kuna watu waliwahi kuugua lakini baada ya kupata tiba mbadala mpaka leo wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kusiki hata dalili.

Mzungu kawapotosha.
 
Wataalamu wa afya wa kisasa wanadai kifafa (epilepsy) hakina tiba.

Huu ni uongo mkubwa,kuna watu waliwahi kuugua lakini baada ya kupata tiba mbadala mpaka leo wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kusiki hata dalili.

Mzungu kawapotosha.
Sio uongo wataalamu wanaongea kwa mujibu wa uwanda wa taaluma yao, kinachofanyika hata katika watu wanaotumia dawa za kisasa za kifafa kwa usahihi inawezekana mtu akakaa muda mrefu pasina kuwa au kuonyesha dalili za kifafa, nilishawahi kukutana na mtoto ana miaka 12 anatumia hizo dawa lakini hajawahi kupata kifafa wala hajui mtu wa kifafa anakuaje, kilichotokea ni kwamba shida aliipata na kugundulika alivokua bado mdogo sana akawa kwenye matibabu mpaka leo na yuko poa.
 
Back
Top Bottom