Ugomvi wangu na Ali Kiba ni "personal"

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,432
7,055
Hivi karibuni, kuna rafiki yangu mmoja alipewa invitation sehemu. Akanicheck nimpe kampani. Tukaenda wote.

Ilikuwa ni house party ya familia fulani ya kiarabu. Naweza kusema ni wale waarabu waliopinda na kunyongorota kabisa maana wanatafuna mirungi, gomba na kukata kilaji kama hawana akili nzuri.

Kitu kimoja ambacho kiliniboa ni playlist yao ambayo ilikuwa inasindikizia ile party. Walijaza nyimbo za Ali Kiba za kiarabu na Marekani kiasi.. Tatizo langu lilikuwa hapo kwa Ally.

Kuna binti ambaye alikuwa ndio anacontrol muziki tulikuwa close na tunapiga story sana vile ni mchangamfu. Uvumilivu uliponishinda, nikamwambia naomba hizo nyimbo za Kiba uzipotezee bhana. Akanishangaa!

Akasema wewe unataka zipi maana humu ndani kila mtu hampendi Diamond/WCB, wote ni team Kiba. Ikawa zamu yangu kushangaa!

Ikabidi tu nimwambie ukweli. Ugomvi wangu na Ali Kiba sio ushabiki wa u-team. Ni binafsi sana. Nikamsimulia kilichotokea kati yangu na msanii huyo takribani miaka 10 iliyopita.

Ni mapenzi. Alitembea na msichana wangu ambaye alikuwa shabiki wake namba moja. Kiukweli ule ushabiki wake hata mimi ulikuwa unanitia wivu sana ila sikujua kama zingefanyika jitihada za kutokea yaliyotokea. Nilirahisisha mno nikajisahau kuwa sote tupo ndani ya Jiji moja na chochote kinawezekana.

Ili ombi langu lifanyiwe kazi, nikamtania kidogo kwa kumsifia kuwa msichana mwenyewe alikuwa shombe shombe kama wewe japo umemzidi uzuri na akili kidogo. Tukacheka na nyimbo za Ali Kiba hazikupigwa tena mpaka tulipoondoka.

NB: Ali Kiba ni msanii mzuri na ana kipaji cha kweli. Sidhani kama kuna msanii anamfikia hasa kwa vocals. Sina tatizo nae kimuziki، ila siwezi kumshabikia kwa sababu nitakuwa natakatisha kile alichonifanyia miaka ile.

Kwa ujumla, nashauri wasanii na watu maarufu wawe na nidhamu. Mitaani kuna visasi vingi.
 
Back
Top Bottom