Uganda, Rwanda na Kenya zinatumia mgongo wa EAC kukopa

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
495
375
Muungano usiyo na jina maalumu wa Rwanda, Uganda na kenya unakopa mkopo kwa kutumia jina la EAC, mkopo uliokopwa ni ule wa kupanua Bandari ya Mombasa na Ujenzi wa Reli itakayounganisha Uganda na Rwanda, cha ajabu hawa watu wanatumia jina la East African Community katika kukopa pasipo Tanzania kushirikishwa!!! je Urudishaji wa mkopo huo utahusisha na Tanzania au pesa ambazo Tanzania nayo huwa Inachangia jumuia hii? je wakishindwa kuulipa Tanzania nayo haitabanwa?

source: Nipashe la leo
 
Dah aisee kama hii habari ni ya kweli basi hawa jamaa wamefika mbali sana, hakuna haja ya kuwafumbia macho tena....
 
Kwa kawaida East African Community haina uwezo wa kukopa as an entity ila inaweza kutumiwa na nchi wanachama kukopa kwa miradi an shughuli za kikanda. Ninaposema kuwa inaweza kutumiwa nina maana kuwa wakopaji na wenye jukumu la kulipa ni nchi wanachama wanaohusika na mradi au mpango huo ila jina la EAC hurahisisha ukopaji. Mfano ni Barabara ya Athi River/Namanga ambayo iko katika mfumo wa barabara za kanda za EAC ambapo msimamizi wa mkopo na ujenzi wa barabara hiyo ni EAC lakini mkopo na ulipaji wa deni uko kwa Tanzania na Kenya.

Hivyo huo mkopo ni kwa Kenya, Uganda na Rwanda ila kinachotatiza ni namna ambavyo jina la
East African Community linatumika katika kufanikisha bilateral/ trilateral ya hawa mabwana nje ya mfumo wa EAC unaoongozwa na makubaliyano (Treaty) ya uanzishwaji wa East African Community. Hili limekuwa tatizo kubwa na sijui ni kwa nini serikali imelikalia kimya huku jamaa wakiendelea kuvunja Treaty. Kumekuwa na upotoshaji wa application of the Principle of variable geometry ambao unaruhusu Nchi wanachama kuendelea na utekelezaji wa vipengere vya Treaty ikiwa baadhi ya nchi au nchi moja haiko tayari. Principle hii inatakiwa kutekelezwa katika mfumo rasmi (mainstream) wa Jumuiya ukisimamiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya baada ya makubaliano rasmi ya nchi zote. Ajabu hawa jamaa watatu wameamua kutekeleza makubaliano ya Treaty nje ya mfumo rasmi na bila kumshirikisha Katibu Mkuu na Nchi wanacham wote. Kiukweli ni kwamba wanatumia Teaty ya EAC kufanikisha matakwa yako nje ya mfumo rasmi wa EAC. Sidhani kama wanaungwa mkono na wananchi wao hasa wa Kenya. Uganda na Rwanda ni rahisi kutumia mifumo yao ya kimabavu ya kiti cha Rais kuamua mambo bila ridhaa ya wananchi wao. Kwa Kenya sivyo na nina hakika si siku nyingi moto utamwakia Kenyatta ambaye kwa mtazamo wangu anasukumwa zaidi na solidarity ya hao jamaa zake wawili, PK na M7, katika kesi yake iliyoko the Hague.

Lets listen and see!
 

EAST AFRIICAN COMMUNIITY
EAC Treaty - 1999



ARTICLE 4Legal Capacity of the Community​
1. The Community shall have the capacity, within each of thePartner States, of a body corporate with perpetual succession,and shall have power to acquire, hold, manage and dispose ofland and other property, and to sue and be sued in its own​
name.


2. The Community shall have power to perform any of thefunctions conferred upon it by this Treaty and to do all things,including borrowing, that are necessary or desirable for the​
performance of those functions
 
unfortunately does not have


EAST AFRIICAN COMMUNIITY
EAC Treaty - 1999



ARTICLE 4Legal Capacity of the Community​
1. The Community shall have the capacity, within each of thePartner States, of a body corporate with perpetual succession,and shall have power to acquire, hold, manage and dispose ofland and other property, and to sue and be sued in its own​
name.


2. The Community shall have power to perform any of thefunctions conferred upon it by this Treaty and to do all things,including borrowing, that are necessary or desirable for the​
performance of those functions
 
Sidhani kama huwo mkopo utatolewa kienyeji pasipo Tz kuhusishwa kwasababu nchi zote hupaswa kuhusishwa na kuweka sine Kwa watoa mkopo..!!
 
Mkopo ni wa hao watatu tu hauihusu Tz. Siyo mkopo kwa EAC ila kwa nchi hizo tatu kwa mradi wa "EAC"!. EAC as an entity pamoja na kuwa na uwezo wa kisheria kukopa kama jamaa alivyo copy Treaty haiko credit worthiness kukopeshwa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuzalisha mapato na kulipa. Haina mapato zaidi ya michango kutoka nchi wanachama na wafadhiri ya kuendesha secretariat and other organs and organizations Za Community.
 
Back
Top Bottom