ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,051
- 49,736
Jeshi la Polisi nchini Uganda limepiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kiongozi wa upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, kutokana na ukiukaji wa utaratibu na kumchafua Rais Yoweri Museveni.
Polisi nchini humo wamesema mtu mmoja amefariki na wengine 10 kujeruhiwa vibaya katika mikutano yake, lakini Bob Wine ameahidi kuendelea na mikutano hiyo.
---
Afrika hii Wapinzani wanafanana tabia na ndio maana Serikali zinawashughulikia.
Watu hawawezi kujadili hoja ila kutukana Viongozi.Tabia hizi ni za kukomeshwa.
Naunga mkono Polisi wa Uganda kumshughulikia Bob Wine.Bado Chadema na Viongozi wake.

Polisi nchini Uganda wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa inayoandaliwa na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine, kutokana na ukiukaji wa utaratibu wa umma na kumchafua rais.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Tumusiime Katsigazi Jumatano alisema mtu mmoja amefariki na wengine 10 kujeruhiwa vibaya katika mikutano ya chama cha National Unity Platform (NUP).
Bw Katsigazi aliwaonya wafuasi wa NUP dhidi ya kile alichokitaja kuwa "mawazo ya kundi la watu...dhidi ya raia na wasimamizi wa usalama".
Polisi pia walimshutumu Bw. Kyagulanyi kwa kuchochea makundi katika mikutano yake iliyoanza Jumatatu.
Bw Kyagulanyi, hata hivyo, ameapa kuendelea na mikutano na kuwataka wafuasi wake "kusubiri ishara". Anatumia mikutano hiyo kuinua uungwaji mkono mashinani kabla ya uchaguzi mkuu wa 2026. Source BBC
Nilijua tu mzee hawezi vumilia mikutano ya bob wine