Ufunuo: Hatari kubwa CHADEMA

Ufunuo: Hatari kubwa CHADEMA

Nijuavyo CDM si chama cha Wakristo bali watanzania wote tena dini zote. Unabii wako siyo mbaya lakini unaweza kuwa unaelemea kwenye yanayotokea sasa.
 
Mlianza na shetani mtamaliza na shetani kumbe siku hizi hata wazinzi wanamtaja mungu kwenye maovu yao pole bwana vumilia mlianza na shetani mtamaliza na shetani.
 
Nijuavyo CDM si chama cha Wakristo bali watanzania wote tena dini zote. Unabii wako siyo mbaya lakini unaweza kuwa unaelemea kwenye yanayotokea sasa.
Kazi yetu harakati utahangaika sana lakini tamati yake ni maumivu subiri utaona omba mungu usife mapema utayaona.
 
Halafu utakuta mtu kama huyu eti na yeye anawaumini tena wanamtii kupita maelezo!Duh hawa mitume/manabii wa ki-digitali kaazi kweli kweli.
 
akomfimuje sasa?
Si kakwambia "kafunuliwa"?
Hahahah
Labda kafunuliwa na demu wake tu unadhani mungu anahangaika na wahuni kama hao make huyu juzi tu alikuwa na matatizo ja ndoa yake halafu hajatatua anatujia na ufunuo utoke wapi.
 
Labda kafunuliwa na demu wake tu unadhani mungu anahangaika na wahuni kama hao make huyu juzi tu alikuwa na matatizo ja ndoa yake halafu hajatatua anatujia na ufunuo utoke wapi.

hahaha,muogopen Mungu Simiyu Yetu,mwenzenu "kafunuliwa",hahaha,
mbavu zangu mie!
Kweli mjini kufa njaa kupenda!
 
Last edited by a moderator:
Hiki ndio kibwagizo cha makamanda "TUMEANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU "halafu mwisho utawasikia wakiimbishana peole's power. Mimi naichukulia kauli hii kama dhihaka kwa Mwenyezi Mungu alietasika na utukufu.

Kumbe mmeanza na MUNGU katika kufanya haya maovu yenu yafuatayo?

  • Mmeanza na Mungu kula ruzuku ya chama mnayopokea kutoka serikalini katika kujenga mahekalu kwa kisingizio @ katibu mkuu hawezi kuendelea kuishi katika nyumba ya kupanga ni hatari kwa usalama wake. Hivi kujimilikisha kienyeji pesa ambayo inatokana na kodi ya walalahoi ambao hata mlo mmoja wa siku kwao imekuwa ni kitendawili MUNGU anapenda?
  • Mmeanza na Mungu kuratibu mipango miovu ya kuwadhuru watanzania ili kijitengenezea mazingira ya kuonewa huruma na wananchi na mwisho kufanikiwa kwa lengo lenu la kuingia ikulu? Hivi kweli MUNGU anapenda vitendo hivyo? Kumbukeni mlichofanya pale Arusha kulipua mabomu katika mkutano wenu na kufuatiwa na mkusanyiko batili ambao ulipelekea kupotea maisha ya watu akiwamo kijana mdogo Mussa Mtoi aliekuwa anatoka kwenye mambo yake. Kumbukeni igunga, Mauaji ya daudi Mwangosi, kifo cha marehemu chacha Wange ambacho inasemekana kimeratibiwa na Mbowe, kumbukeni habari za sumu, kulegeza tairi za gari la zitto ili kumuua, n.k.
  • Mmeanza na Mungu kuwasingizia binadamu wenzenu kuwa ni mafisadi kisa tu wanataka kugombania nafasi mbalimbali za juu katika chama chenu?.
  • Mmeanza na Mungu sikuhizi kudai posho ziongezwe kwa wabunge huku mkijinadi kama watetezi wa wanyonge?.
  • Mmeanza na Mungu kwenda kujenga majumba ya kifahari ughaibuni huku mkiwashakiza walalahoi waaandamane ili kikinuka nyinyi mkimbilie nje ya nchi mkale zenu kuku kwa mirija mkiwaacha walalahoi wakiteseka?

  • Mmeanza na Mungu kueneza chuki miongoni mwenu ya kuwachukia na kuwabagua wanachama wenzenu kwa madai ya kinafiki yasio na ushahidi wa kueleweka?.
​ To mention a few.

Nakuombeni mumheshimu MUNGU na msililitaje bure jina la Mungu hata maandiko yatuonya ya kwamba "usilitaje bure jina Mungu wako".
Akhsanteni kwa kunisoma.

Ukweli hauwezi ukafutwa kwa uwongo wenu.mtatafutiza uwongo mpaka mtachoka ukweli utabaki umesimama palepale.
 
Ukweli hauwezi ukafutwa kwa uwongo uwongo wenu mtatafutiza uwongo mpaka mtachoka ukweli utabaki umesimama palepale.
Tena la kuvunda halina ubani likivunda linavunda tu ngonja watakimbizana mpaka kona zote za nyumba wakirudi watakuta ukweli unawasubiri tu hata wafanye nini fimbo wanazo.
 
hahaha,muogopen Mungu Simiyu Yetu,mwenzenu "kafunuliwa",hahaha,
mbavu zangu mie!
Kweli mjini kufa njaa kupenda!
Mkuu Free thinker,
jamaa huyu kituko kweli ukiingia jukwaa la mapenzi jamaa kila siku analalama tu juu ya ndoa yake sasa kama mtu kwenye ndoa tu anamatatizo si lazima awe mzinifu kwa kufunuliwa na wadada mbali mbali.
 
Hahaa!
Halafu anadai Mungu kamwambia viongozi wamfukuze "msaliti" anaye jadiliwa sana!
Dah!
This is more than cheap politics baina ya kambi zilizopo cdm!
Mashabiki wa cdm&ccm mna kaz sana Simiyu Yetu!
Nasubiri tu na wewe "ufunuliwe" Dr.W.Slaa ni hatari sana kwa cdm,hahaha,lol
 
Last edited by a moderator:
Wanajukwaa,

Kwanza nianze kwa kutanabaisha mi si mwanasiasa, sina chama na sipendi siasa lakini siku kadhaa nilipata mafunuo haya, nikaamua kunyamaza cha ajabu nafsi inaniuma sana na mengi yameanza kutokea wacha niseme ukweli.

1. Kuna hatari kubwa sana inakuja CHADEMA endapo uongozi wa chama hiki hautachukulia umuhimu unabii huu. Katika mafunuo haya nimethibitishiwa kwamba Mungu anampango wa kuliokoa taifa la Tanzania kupitia chama hiki, na amesema ni lazima ataonyesha uwezo wake viongozi wa CHADEMA muondoe wasiwasi.
2. Hatari kubwa inayoweza kuwapata mtakuwa na mapigo makali sana kwa sababu ya kwenda kinyume na taratibu au njia Mungu aliyowapangia. Hamfuati lile wingu lilikuwa linaongoza wana wa Israel, mnataka kufanya kama Yona ole wenu kwani hata vifo vitawapata. Kwanini mnaogopa wakati Mungu yu nanyi? Hatari kubwa sana.

Hatua za kuchukua.
1. Zipuuzieni tuhuma zote zinazotolewa na CCM mwangalieni nyoka wa shaba, achaneni na hawa nyoka wadogo wadogo.
2. Mnatakiwa kufanya maamuzi magumu bila kupenda, njia ya wazi imewekwa machoni kwenu. Kuna kiongozi mmoja mkubwa ndani yenu si wa KWENU ni Yuda ndani ya wanafunzi wa Yesu msiogope huyu hatafanya kitu juu yenu ila mnatakiwa mumuondoe mapema
iwezekanavyo, hana madhara kwa wanachama kama mnavyodhani. Huyu anajulikana na anajadiliwa sana saivi kwa usaliti.
3. 2015 mtashinda ila kutakuwa na vita vikali sana msipofuata haya hamtaingia IKULU na kutatokea vita Tanzania. CCM wataiba sana kura, na watajitangaza washindi.
Katika hili fanyeni hivi,
Mungu anasema hamtashinda kwa kupambana nao vita au kusimamia kura, ila mnatakiwa kuwa na kikundi cha sifa na maombi, na kianze kazi sasa. Nyinyi mtamwimbia Mungu na atawapigania nyinyi mtakuwa mnamwimbia nayeye anawapigania kama taifa la mfalme
Yehoshafati.

Niko tayari kuwasaidia katika hili la timu ya maombi.

Zaidi tuwasiliane.

Braza tunakujua wewe jaman huyu nitoke vp hajaanza leo wa ck nying
 
UBOVU NA MAOVU YA CCM NDIO YATASABABISHA WANANCHI KUCHAGUA HATA JIWE KUWA RAISI, naona kifo cha ccm 2015
 
Hicho kirusi kitakua ni Dr. Slaa na kirusi kisaidizi kitakua Mbowe Freeman.

Na Aunt Virus ni Zitto

I hope ata clean hao virus waliopo kwenye CDM operating system na itabaki salama kwa matumizi pasipo tatizo aina lolote...
 
Hauko sawa kabisa wewe!

Yani chama chenye watu wajinga kama Lema na Yericko Nyerere kipate baraka Mungu?!

Hakika wewe utakuwa umevurugwa usiku si bure!
 
Wanajukwaa,

Kwanza nianze kwa kutanabaisha mi si mwanasiasa, sina chama na sipendi siasa lakini siku kadhaa nilipata mafunuo haya, nikaamua kunyamaza cha ajabu nafsi inaniuma sana na mengi yameanza kutokea wacha niseme ukweli.

1. Kuna hatari kubwa sana inakuja CHADEMA endapo uongozi wa chama hiki hautachukulia umuhimu unabii huu. Katika mafunuo haya nimethibitishiwa kwamba Mungu anampango wa kuliokoa taifa la Tanzania kupitia chama hiki, na amesema ni lazima ataonyesha uwezo wake viongozi wa CHADEMA muondoe wasiwasi.
2. Hatari kubwa inayoweza kuwapata mtakuwa na mapigo makali sana kwa sababu ya kwenda kinyume na taratibu au njia Mungu aliyowapangia. Hamfuati lile wingu lilikuwa linaongoza wana wa Israel, mnataka kufanya kama Yona ole wenu kwani hata vifo vitawapata. Kwanini mnaogopa wakati Mungu yu nanyi? Hatari kubwa sana.

Hatua za kuchukua.
1. Zipuuzieni tuhuma zote zinazotolewa na CCM mwangalieni nyoka wa shaba, achaneni na hawa nyoka wadogo wadogo.
2. Mnatakiwa kufanya maamuzi magumu bila kupenda, njia ya wazi imewekwa machoni kwenu. Kuna kiongozi mmoja mkubwa ndani yenu si wa KWENU ni Yuda ndani ya wanafunzi wa Yesu msiogope huyu hatafanya kitu juu yenu ila mnatakiwa mumuondoe mapema
iwezekanavyo, hana madhara kwa wanachama kama mnavyodhani. Huyu anajulikana na anajadiliwa sana saivi kwa usaliti.
3. 2015 mtashinda ila kutakuwa na vita vikali sana msipofuata haya hamtaingia IKULU na kutatokea vita Tanzania. CCM wataiba sana kura, na watajitangaza washindi.
Katika hili fanyeni hivi,
Mungu anasema hamtashinda kwa kupambana nao vita au kusimamia kura, ila mnatakiwa kuwa na kikundi cha sifa na maombi, na kianze kazi sasa. Nyinyi mtamwimbia Mungu na atawapigania nyinyi mtakuwa mnamwimbia nayeye anawapigania kama taifa la mfalme
Yehoshafati.

Niko tayari kuwasaidia katika hili la timu ya maombi.

Zaidi tuwasiliane.
SIASA NA DINI:
Mimi ni muumini pia na ninaamini Biblia kama wengine wafanyavyo, mbali ya hayo ni mwalimu mstaafu wa chuo cha theologia. Nina Masters ya theologia na nina Doctorate katika mambo ya serikali in general. Lakini siamini kuwa Mungu ana vyama vya siasa ila naamini kuwa ana watu ambao wana taifa lao na wote kwake ni sawa. Kwa hiyo tusiingize mambo ya imani na tafsiri binafsi za maandiko. Tukifanya hivyo tutawavuruga wengi. Kwani siasa na Dini havichanganyiki, ukilazimisha kibuyu kinapasuka.
 
Hakika umenena, chama kinahtaji dua za dini zote ispokuwa dini ya shetani
 
SIASA NA DINI:
Mimi ni muumini pia na ninaamini Biblia kama wengine wafanyavyo, mbali ya hayo ni mwalimu mstaafu wa chuo cha theologia. Nina Masters ya theologia na nina Doctorate katika mambo ya serikali in general. Lakini siamini kuwa Mungu ana vyama vya siasa ila naamini kuwa ana watu ambao wana taifa lao na wote kwake ni sawa. Kwa hiyo tusiingize mambo ya imani na tafsiri binafsi za maandiko. Tukifanya hivyo tutawavuruga wengi. Kwani siasa na Dini havichanganyiki, ukilazimisha kibuyu kinapasuka.

Haya Mkuu tumeshajua una masters ya theolojia na una doctorate..
 
Back
Top Bottom