Ufugaji wa Mbwa kwa biashara

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Miongoni mwa mambo yanayotusumbua sana wafugaji ni pamoja na suala zima la ulinzi. Mbwa ni mlinzi mwaminifu kwa karne nyingi na mahitaji ya mlinzi huyu yanaongezeka kila siku.

Mbwa wanaopatikana sokoni si wale wa kiwango cha kimataifa. Ukiwa na mtaji changamkia biashara hii. Bei ya mtoto wa mbwa aina bora haishikiki kabisa. ukiamua kuwafuga mbwa kibiashara, basi andaa ulinzi kumlinda mlinzi. Mbwa nao wanaibiwa sana siku hizi teheeeee.

Ukitaka kujua aina bora ya mbwa, nenda chuo cha polisi Kurasini.
 
Hii ni kweli nami nitahitaji ila wawe mbegu nzuri. Polisi nimesikia ukiwapelekea wakiwa wadogo wanakusaidia kuwapa mafunzo. Tupate info zaidi maana kuwafuga kama sio mbegu nzuri na hawajafunzwa hawasaidii na wanakula kuku.
 
kufuga mbwa kibiashara ni nzuri sana ila lazima uwe na vitu viwili,

1. Kwanza kuzalisha hao mbwa na kuwauza wakiwa wadogo

2. Pili kuwa na altenative kama kampuni ya ulinzi ya kutumia mbwa ili basi mbwa wasipo nunuliwa na wakiwa wakubwa watumike katika biashara hiyo
 
Ni kweli, lakini biashara hii haijavamiwa.Kila ninakouliza mbwa ili ninunue naambiwa wamekwisha. Shida iko ktk aina ya mbwa wa kufuga,sio kila mbwa ana soko. Mara ya mwisho mbwa mgodo amefikia bei ya laki moja na nusu.
 
Kuna rafiki yangu anatokea Kenya,mwaka jana alikuwa na business plan ya kufungua kernel ya mbwa.pia kuzalisha kama kitoweo,kwani siku hizi wakina HuNHA wamekuwa wengi Dar,na kila wanapoweka site/gereji ujue huo mtaa mbwa wataanza kupungua,kwani wana mbinu na mitego mingi ya kuwanasa mbwa.
 
Akina Hwang Ho wameleta balaa, wakati wanajenga uwanja wa mpira, ng`ombe wa Iringa walipotea ghafla sana.Tatizo hawa jamaa wanalamba kila kitu,hadi kinyonga.

Natafuta mbwa nimpeleke shambani akasaidie ulinzi.
 
Ha ha ha ha ha Hua ni noma hawa jamaa wamejenga majengo mawili hapa Arusha Hotel inayotazamana na Ofisi ya mkuu wa mkoa na jengo lingine la NSSF linatazamana na kanisa la Anglicana Christ Church maeneo yote mawili walikuwepo mbwa koko wengi [Mbwa wasiotunzwa,wasikuwa na mwenyewe] leo hakuna mbwa anayezuruza hovyo wote wameliwa na hua ha ha ha.

Kuna rafiki yangu anatokea Kenya,mwaka jana alikuwa na business plan ya kufungua kernel ya mbwa.pia kuzalisha kama kitoweo,kwani siku hizi wakina HuNHA wamekuwa wengi Dar,na kila wanapoweka site/gereji ujue huo mtaa mbwa wataanza kupungua,kwani wana mbinu na mitego mingi ya kuwanasa mbwa.
 
Ha ha ha ha ha Hua ni noma hawa jamaa wamejenga majengo mawili hapa Arusha Hotel inayotazamana na Ofisi ya mkuu wa mkoa na jengo lingine la NSSF linatazamana na kanisa la Anglicana Christ Church maeneo yote mawili walikuwepo mbwa koko wengi [Mbwa wasiotunzwa,wasikuwa na mwenyewe] leo hakuna mbwa anayezuruza hovyo wote wameliwa na hua ha ha ha.

Inawezekana hawa jamaa na marafiki zao Wahehe kuna kitu wanakiona/wanapata au wanafaidi kutoka kwa mnyama huyu ambacho wengine hatukioni. Nitafanya utafiti nikienda Iringa vijijini kwa wazee, huenda nakosa siri nzito teheeeeeeeeeee
 
Hivi ukienda Kurasini pale polisi ukataka kununua mbwa kwa ajili ya ulinzi aliyefunzwa vizuri wanaweza kukuuzia?:target:
 
Sina uhakika kama wanafanya biashara hiyo. Wangefanya hiyo biashara wangepiga hela vibaya sana. Sasa hivi mbwa wanatafutwa sana.
 
mkuu wale mbwa hawauzwi!kuna mdau ali post humu anao puppies anauza,ila kaingia gizani ghafla!tafuta post yake alieka mobile yake pia.
 
Kwani wale mbwa wa Polisi huwa hawazaliani? wakizaliana watoto wanaenda wapi? kwanini wasiuzwe?
 
Mimi ninauza Mbwa aina ya Belgian Shepherd Malinois, nimebakiza puppies wa 3. Majike 2, Dume 1. Wamezaliwa wana wiki 1 mpaka leo trh 21 July 2012. wamezaliwa puppies wa5 wawili wapo kwenye oda.

Nitawatoa kwa mama yao wakifikisha mwezi na nusu. Napatikana Mbeya

ukitaka kujua tabia za mbwa hawa gonga hapa Belgian Malinois Breed Information & Pictures (Malinois, Chien de Berger Belge, Belgian Shepherd Malinois)

BEI: 150,000/=

Piga simu: 0713 952 744

Mby kipande gani, nataka aende Uwanji akaaongeze ulinzi.
 
mkuu mbeya mbali sana,mm ninao germany sherphered,ila nashangaa hawatak kuzaa!sijui kwa vila nataka kuuza!ni bness nzuri sana,manake puppy wa miez 2 unauza laki 3!wakizaliwa 10!dah full faida aisee!hakuna cha tra wala nn!
 
Uko mitaa gani sasa mkuu?
 
mkuu mbeya mbali sana,mm ninao germany sherphered,ila nashangaa hawatak kuzaa!sijui kwa vila nataka kuuza!ni bness nzuri sana,manake puppy wa miez 2 unauza laki 3!wakizaliwa 10!dah full faida aisee!hakuna cha tra wala nn!

wewe uko mbeya?
 
Back
Top Bottom