Ufuatiliaji

Kidatu

JF-Expert Member
Jun 11, 2008
1,542
307
Ndugu wana JF,
Nimepata muda wa kupitia topic karibu zote hapa JF ingawa ni nyingi na ndefu.
Nimeona wazi kwamba hiki kijiwe cha JF kina mchanganyiko wa watu wa aina tofauti, wenye vipaji na mtazamo tofauti lakini wengi wao 80% wana uchungu na Tanzania.

Topic nyingi zimelenga katika kuonesha machafu yanayotendeka ndani ya nchi yetu, nani anatenda hayo machafu na anayatenda vipi. Na kuna baadhi ya topic wana JF wamejaribu kutoa mapendekezo nini kifanyike ili kuweka sawa pale palipoharibika.

Kwa mtazamo wangu finyu ningependekeza tuwe na watu maalumu hapa JF wakufuatilia nini matokeo ya topic zinazojadiliwa katika kijiwe hiki.

Kuna topics muhimu sana hapa JF ambazo zinagusa maisha ya Watanzania wote bila kujali rangi, dini, kabila wala umri lakini zilizo nyingi zinaishia ishia tu bila kujua hitimisho la topics hizo.

Kumekuwa na tabia ya kuibua na kuchangia topic mpya huku zile za nyuma tukiziacha kabisa na kuzisahau kama vile hakukuwa na kitu kama kile. Kwa kufanya hivyo kunawapa kiburi na dharau wahusika katika makashfa yanayoibuliwa kwa kusema kwamba hata wakisema leo kesho watapata kashfa nyingine na hili langu litawekwa kapuni.

Bila shaka lengo la JF ni kumkoma nyani hadi kieleweke mwisho wake. Lakini kwa upande wangu naona tungefanikiwa zaidi kama tungekuwa na utaratibu wa kufuatilia matokeo ya topics zetu na hata ikibidi tupate hitimisho la topics hizo.

Hiki ni kijiwe kinachozungumzwa sana Tanzania hasa katika maofisi ya serikali, mashirika ya Umma na pia katika maofisi za mabalozi wa nchi za nje waliopo Tanzania. Hivyo kinacholetwa hapa kujadiliwa kinapitiwa na watu wengi sana.
Na pia kijiwe hiki kimekuwa mwiba na pilipili kwa serikali iliyopo madarakani tokana na kuanikwa kwa uchafu unaendelea ndani ya serikali. Kwa hili ningependa kuishauri serikali iliyopo madarakani kwamba ni bora kuitumia JF kama kioo chao cha kuangalia wamekosea wapi na nini kifanyike na wala hakuna sababu ya kukichukia kijiwe hiki.
 
TO BE FAIR ......! SI KWA SERIKALI PEKE YAKE BALI WATENDA MAOVU, NA USHAURI WAKO NI KWA WALE WOTE WAIFANYE JF KAMA KIOO.....!
anyway NI USHAURI MZURI.....!
 
MANAKE WAZUNGUMZWAO HUMU NI WENGI , CCM,CHADEMA,KKKT, ANGLIKANA, BAKWATA, SERIKALI, SHOPRITE, OPEN UNIVERSITY, KILI MUSIC AWARDS, ZE COMEDY, MCH. RWAKATARE, KAKOBE, ...........( the list goes on....)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom