mareeTZ
Senior Member
- Jun 4, 2015
- 171
- 181
Kumekuwa na hadithi nyingi sana katika ulimwengu huu tunaoishi kuwa hatupo tu binadamu na wanyama pekee yetu bali pia kuna viumbe wengine wanaishi walio kama sisi maumbo mithili ya kwetu, akili kama sisi pengine kutuzidi sisi. Wengi hudai viumbe hawa wanaishi katika sayari nyingine tofauti na dunia yetu na mara kwa mara wamedaiwa kutembelea maeneo kadhaa duniani. Viumbe hawa wanatambulika kama aliens na yako mamia ya shuhuda ziliripoti na watu mbalimbali waliodai kuwaona viumbe wakiwa na chombo cha duara kinachoruka kama ndege na hukitumia katika safari zao za kutembelea duniani vyombo hivi pamoja na aliens hawa hujulikana kama (UFOS) kirefu chake ni (Unidentified flying object) maana yake ni viumbe wasioeleweka warukao pande mbalimbali za dunia yetu. Je ni kweli viumbe hawa wapo? Je Ni kweli wameonekana hapa duniani? Kuna wanaopinga na kudai ni ndege za kijeshi zinazofanya mipango ya siri na hivyo watu hudhani ni UFOs.
Moja kati ya shahidi zinazoonyesha kwamba UFOs siyo ndege au vyombo vya kawaida vitumiwavyo na wanadamu wa kawaida ni uwepo wa matukio haya ya UFOS yaliyoanza kuripotiwa zamani sana kipindi ambacho hata binadamu hajagundua ndege au chombo chochote cha moto. Tukio la kwanza kabisa kuwahi kuripotiwa ni la gavan wa koloni la Massachusetts bwana john winthrope mnamo mwaka 1639 aliyeandika kwenye kitabu chake cha kumbukumbu kuhusu tukio la msaidizi wake james evereel aliyeona chombo kikubwa chenye kutoa mwanga mkali kikipaa na kutua pembezoni mwa mto muddy kwa muda wa masaa matatu. Pia julai 1884 iliripotiwa kuonekana kwa chombo cha umbo la duara kilichozungukwa na pete kama sayari ya Saturn huko mjini norwood new York.
Katika matukio ya kushangaza kabisa ya karne hii yaliyoacha maswali mengi ulimwenguni kote ni pamoja na tukio la wanafunzi waliodai kuwaona viumbe hawa nchini Zimbabwe.
Mnamo asubuhi moja ya septemba 16 mwaka 1994 walimu na wafanyakazi wa shule ya ariel walishikwa na mshangao baada ya baadhi ya wanafunzi kuanzia miaka 7 na 12 kudai kuna ndege ya ajabu ilitua katika viwanja vya shule hiyo. Muda huo walimu walikuwa kwenye kikao hivyo wanafunzi walikuwa nje bila uangalizi wowote wakati tukio hilo linatokea, siku mbili kabla ya tukio hilo huko mjini Harare kilomita 20 kutoka mji wa ruwa kuliripotiwa kuonekana vitu vinavyopaa angani visivyoelewka.
Watoto hao walidai kwamba mwanzo waliona vitu tofauti vitatu vinazunguka angani baada na ya muda vinapotea na kutokezea tena eneo lingine halafu vyombo hivyo vikaanza kusogea kuelekea chini mwishowe vikatua katika vichaka pembezoni mwa viwanja vya shule hiyo,
Wanafunzi hao wakadai waliona kiumbe mfupi mithili ya mwanadamu mwenye urefu kama mita moja kasimama juu ya chombo hicho. Ghafla yule kiumbe alianza kuwasogelea wale wanafunzi taratibu. Kimwonekano alikuwa ana shingo kama ya mtu mzee sana, macho makubwa meusi na nywele ndefu nyeusi. Ghafla wanafunzi wale walianza kupiga mayowe wakikimbia huku na kuo kuomba msaada wakijua labda ni mashetani waliyokuwa wakihadithiwa na mababu zao katika baadhi ya hadithi. Kelele zile zilimshtua kiumbe yule alipowaona wanafunzi wale na ghafla alipotea na kutokeza tena pembeni ya kile chombo ambacho kiliondoka ghafla na kupotelea angani.
Cynthia hind mchunguzi wa matukio ya UFO barani africa aliwasili shuleni hapo kesho yake asubuhi ambapo ali kutana na mkuu wa shule hiyo, wanafunzi Zaidi ya 65 waliapa na kuripoti vitu vinavyofanana kuhusu tukio hilo. waliambiwa wachore picha za kile walichokiona jana yake. Zilichorwa picha tofauti 35 zilizokuwa na mwonekanao wa aina moja. Mmoja wa watoto hao alisema viumbe hao walikuwa wakitoa ishara kuonesha kwamba binadamu tunaharibu dunia yetu kwa uchafuzi wa mazingira hivyo tuache kabla hakujawa na madhara makubwa
Michoro ile ililingana na mamia ya matukio ya watu waliokiri kuona viumbe wa ajabu duniani
Kitabu kimoja kinachoitwa the report on identified flying object cha mwaka 1955 kilichoandikwa na Ruppelts kimeelezea mamia ya matukio ya kuonekana kwa UFOS duniani kikiandika shahidi mbalimbali za kweli kutoka kwa marubani wa jeshi pamoja na wanasayansi mbalimbali ambao walitoa ushahidi kuhusu kuwaona viumbe hao wakiwa huko angani. Shahidi nyingi zimethibitishwa lakini mpaka sasa kisa cha zimbambwe kimeacha maswali kadhaa , je ni kweli tukio hilo lilitokea? Na lipi fundisho hasa kwetu sisi wanadamu?