maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,345
- 15,851
Hahahaaa...si lazima,aseme tu nini kilipelekeaUlitaka amtaje nanilii?
Hahahaaa...si lazima,aseme tu nini kilipelekeaUlitaka amtaje nanilii?
wakati watu wengi wakimuona muuaji wa mama yake ufo Saro ni mnyama,ni mkatiri,ni muuaji,hafai MIMI nipo tofauti sana na wengi.
1.mume wake ufo saro hakuwa mwehu na uamuzi aliochukua hautokani na uwehu na kama angekuwa mwehu hakupaswa kuwa na ufo saro
2.nani anajua makosa ya ufo saro na mama yake ufo saro kwa huyu muuaji?Je ufo saro si mkatiri?Si mnyama?Je ana ubinadamu?
3.ni nani anaeamini kuwa Ufo saro anaweza kueleza waziwazi mabaya yake yote yaliyopelekea balaa?Hakika naamini Ufo saro hawezi kuelezea makosa,manyanyaso,usaliti na ukatiri wake kwa mume wake,zaidi atavutia kwake tu kama utamaduni wa kila muwamba ngoma.
4.mliomhukumu aliyempiga risasi ufo saro bila maelezo ya upande wa pili wa muuaji hamuwezi kuwa sahihi kwa kuwa hukumu yenu ina maelezo ya ufo saro peke yake.
MTU ANAWEZA KUPIGA MTU HADI AKAZIRAI alafu yeye akiwa na majeraha kidogo akawahi kufungua jalada polisi,lakini polisi wakimuona mshitakiwa watashangaa maana haihitaji utalamu kubaini kuwa mshitakiwa ndo [/qoate]
Kichwa cha habari yako kina mvuto lakini maelezo uliyoyatoa hayajitoshelezi kabisa.
Nilitegemea unatoa taarifa sahihi za upande wa pili kwamba ni kwanini marehemu Mushi asilaumiwe; kumbe porojo!!!!!!!!
Toa ushahidi thabiti; kwanini jamii iaimlaumu muuaji; muuaji alitendewa nini hata uamuzi aliouchukuwa uonekane sahihi!!!
Acha bla bla kaka!
Asante.
Ila taarifa ya polisi imetoka, Mushi aliuliwa, na nani...kaa chonjo.
Upo hapo?
Sasa hapa naona Asprin unachanganya na ile stori ya Westgate kule Kenya, au?Na kuna ile hadithi ya kuwafuata vijana chumbani, wakapanda juu ya dari then wakatokea kwenye paa. kuna hadithi ya kulipua mitungi ya gesi na kuchoma magodoro.
Kuna hadithi nyingi sana hapa.
kweli ni utata na kuna kauli niliisikia kuwa u4 alimueleza yule muuza samani kwamba muuaji nimemuacha ndani cjui kama familia yangu ipo salama..sasa kama muuaji alimuacha ndani alimuonaje tena akijiua?Thibitisha haya kama unayosema nikweli. 1. Mushi alikuwa ni mume wake halali kwa mujibu wa sheria au ni hawala. 2. je, alipofika nyumbani nini kilimsukuma aseme leo atajiua yeye na mtoto? chanzo cha kupelekea kusema hayo. 3. mtoto kwa wakati huo alikuwa wapi kule KIBAMBA au nyumbani kwa UFOO. 4. Kwa mama walienda kufanya nini? 5. UFOO baada ya kupata taarifa ya MUSHI kutaka kumwua mtoto kisha yeye ajiue, alichukua hatua gani kama kuzuia tukio hilo? 6. kabla ya kuamua kwenda KIBAMBA, Ufoo alitoa taarifa kwa mama yake juu ya ujio wao hapo? 7. walitumia usafiri gani kwenda KIBAMBA? kama ni binafsi walikuwa wangapi na nani alikuwa dereva? 8. kama MUSHI alikuwa na nia ya kumwua mtoto wake na yeye kujiua, nini kilichosababisha amwue mama UFOO, na kisha kumjeruhi UFOO wakati hawakuwa kusudio lake kwa mujibu wa hayo maelezo hapo juu? 9. kama UFOO alipigwa risasi 2 na akafanikiwa kutoka nje kwa kujiburuza, aliwezaje kugeuka na kumwona MUSHI akijipiga risasi kidevuni?, alijuaje kuwa pale ni kidevuni wakati yeye alikuwa kwenye mwendo tena nje? 10. kwani MUSHI alijipiga risasi akiwa ndani ya nyumba au nje? yapo mengi ila kama anaweza ajibu maswali hayo 10 ili kupata uthibitisho wa taarifa hiyo. Pia nampa pole kwa maumivu, ni hayo tu kwa leo
Acha ujinga wewe. Unaquote habari yote hiyo na kutoa hoja fupi namna hii! Wengine tunatumia mchina bhana!
Watu mnashangaza sana. Mnamlaumu sana ufoo ataje sababu. Ili iweje? Hayo ni maisha yake na matatizo yake binafsi si lazima aitangazie dunia. Akipona atahojiwa na km anakosa atachukuliwa hatua vile vile.
Haijalishi source ya mushi kuchuchukua maamuzi km hayo ni nini. Mushi hakupaswa kuchukua uamuzi aliochukua no matter ufoo amemfanyia nini. Atakuwa ni chizi tu upstairs. Mwanaume unatakiwa ukabiliane na tatizo na ujue jinsi ya kukitatua. Lakini si kuua.
Mushi alikuwa na matatizo ya akili tu. Km alishachoka maisha angejifyatua yeye mwenyewe peke yake.
mawazo ni mazuri, ila yanakufaa wewe na vilaza wenzio: kuna roho za binadamu zimepotea xo tunahitaji interlligencia sio kupotezea penye hamna
Halafu, anasema alipita dada mmoja akamwomba kanga akajifunika.
Ina maana eneo hilo lina watu makatili sana...mtu amepigwa risasi 2, na anajiburuza na damu zinamtoka, bado huyo mdada aliishia kumpa kanga tu, na akaendelea zake na safari bila kufuatilia kulikoni mtu ana hali hiyo ya kutisha!!
Halafu, kama pale Tumbi aliweza kucommand daktari apigiwe simu, ilikuwaje asitoe taarifa za mkasa aliouacha nyumbani wa vifo vya watu 2 wakiwa wamelala sakafuni?
Mbona inaonyesha alikuwa na roho ngumu ya kutomwambia hata yule mdada aliyekutana naye, kwamba nyumbani kwao kuna msala?...hii imekaaje?
Mbaya zaidi inaonyesha huyu dada akiwa kwenye matibabu aidha anasoma magazeti au kubofya mitandao, maana anaonyesha kureact kwa watu anaodai wanataka kupotosha habari, kazi ambayo ni ngumu sana na kwavile hajapona sawa anaweza akajiongezea maradhi.
Ila movie nyingi huwa zinaanzaga hivi wakuu msiwe na hofu