Sasa Ufoo, mzazi mwenzio kaja na anakwambia atajiua na mtoto wenu pia, wewe ulichukua hatua gani kuzuia hilo? Huyo Mushi hana close friend ambaye ungempigia simu na kumweleza kuhusu jambo hilo la kutisha asemalo baba mtoto wako? Au alikua anasema hilo huku akiwa na tabasamu pana mdomoni ukaona ni utani tu? Yani hiyo kauli haikukushtua utoe taarifa polisi pia? Unless kama uliitegemea kwa kuwa kuna kitu umefanya! Na ulilala the same house na mtu aliyetoa vitisho hivyo na asubuhi makongozana kwenda kwa mama?! Ulijihisi uko salama? mie nisingelala nyumba moja na mtu aliyesema jambo la kutisha hivo! Ningekimbia usiku huo huo! Na mama yako ulimtahadharisha kwamba mnakuja na kuna neno baya limesemwa na mzazi mwenzio ili ikibidi aite hata polisi kabisa?
Na mwanao alikua wapi?!
Dada nakutakia upone salama na urudi nyumbani, lakini jaribu kutoongea kwa sasa, kwa sababu unazidi kuongeza utata.
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums