Ufoo saro aanika kila kitu juu ya sakata lake

Ufoo saro aanika kila kitu juu ya sakata lake

Busara inamtaka yeye na wenye nia ya kutaka kujua ukweli kuvuta subira, kwasasa atakuwa anaongea mambo ya ajabu na yatakayo leta utata mbele ya safari. Afunge mdomo wake na waandishi waache kumsaili mambo hayo kwa sasa.
 
Kwa taarifa za hospitali, madaktari walimkuta ufoo na risasi mbili mwilini. Lkn maelezo ya ufoo ni kuwa alipigwa risasi mbili kwa nyuma zikatokea upande wa pili. Hapo napata utata
 
Mdada huna sababu ya kuongea na mtu yeyote juu ya tukio lile zaidi ya wanafamilia tu na polisi. Hayo mambo ya wanahabari achana nao, hayo ni masuala yako binafsi wala hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kukutaka useme chanzo cha tukio lile. Kwa sasa tuliza akili, pata matibabu ili upone na kuendelea kufaidi maisha, hao waliopoteza maisha kwa tukio lile mungu awalaze pema peponi. Tunahitaji kuutumikia uhai na kuendelea na maisha. Nakuombea upate nafuu na urudi kuendelea na maisha,
 
Yani wanawake sijui wapoje. Aliwezaje kumnyima lift u4 wakati amejeruhiwa?

unadhan angefia kwenye hiyo gari nini kingejiri kwa upande wa huyo mama mwenye gari???angeembiwa kamuua yeye!!!

Sasa yanini kujitafutia kesi zisizomuhusu???....kumbuka wema sometimes huponza!!!!
 
mwandishi wa kituo cha televisheni cha itv, ufoo saro ambaye hivi karibuni alikumbwa na madhila ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mzazi mwenzie, ameanza kufunguka kidogo kidogo na kueleza kwa kina jinsi tukio zima lilivyotokea.

Akizungumza kwa sauti ndogo na taratibu na gazeti hili kando ya kitanda alicholazwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili, mwanahabari huyo alieleza kushangazwa na ujasiri na nguvu za aina yake ambazo zilimwezesha kutambaa na kujiburuza hadi eneo la karibu ya barabara ili kuomba msaada wa kukimbizwa hospitali.

Ufoo ambaye alionyesha dhahiri kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazozingira tukio lake, alisema tayari alikuwa amewahakikishia polisi waliofika kumjulia hali hospitalini hapo kwamba alikuwa akisubiri afya yake iimarike kabla hajaeleza kwa kina kila anachokijua kuhusiana na tukio hilo.

“alifika hapa kunijulia hali na kuangalia maendeleo yangu afande msangi na nikasema nitakuwa tayari kueleza kila ninachokijua baada ya afya yangu kuimarika. Nasikitika kuna watu wanasema mambo wakifikia hatua ya kutaka kuonekana wananifahamu vizuri kuliko hata ninavyojifahamu mwenyewe,” alisema akionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazoripotiwa kuhusu sakata lake.


Ufoo ambaye alifikishwa hospitalini hapo jumapili ya wiki iliyopita kutokana na kujeruhiwa kwa risasi na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja alisema anamshukuru sana mungu kwa uzima alionao sambamba na kuelezwa kupata faraja kubwa na kutiwa moyo na mwajiri wake, ndugu, jamaa na marafiki.

Mwanahabari huyo ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi mwilini mwake siku chache zilizopita, amelazwa katika chumba cha peke yake ambacho ingawa kina seti ya televisheni alisema alikuwa haruhusiwi kuiangalia kwa ushauri na maelekezo ya madaktari.

Huku akionekana wa chini ya uangalizi mwingine wa karibu na wa kudumu wa muuguzi ambaye muda wote wa mazungumzo haya alionekana kuwapo katika chumba hicho, ufoo alisema alikuwa ana mapenzi makubwa kwa mzazi mwenzake huyo ambaye alipoteza maisha katika tukio hilo.

“nilimpenda sana antheri. Alikuwa kijana mtaratibu na mpole sana. Najua kile kilichotokea ni shetani tu na binafsi nilishasamehe alfajiri ile ile baada ya tukio lile,” alieleza ufoo ambaye pia alimpoteza mama yake mzazi katika mkasa huo.

Tukio zima lilivyotokea

ufoo ambaye mara kadhaa katika mazungumzo na gazeti hili alionekana kukunja uso akiashiria kupata maumivu, alionyesha eneo la chini ya bega katika mkono wake wa kulia lililofungwa na bandeji ambalo alisema ndipo alipopigwa risasi ya kwanza wakati akigeuka na kujaribu kuepuka mauti muda mfupi baada ya antheri kumfyatulia risasi zilizomkuta mama yake mzazi.

Akijaribu kuvuta kumbukumbu ya tukio lilivyoanza, ufoo alisema mzazi mwenzake huyo alifika nyumbani kwake akitokea sudan alikokuwa akifanya kazi usiku huo huo wa tukio na akamtaka kwenda kwa mama yake (ufoo) eneo la kibamba, nje kidogo ya jiji la dar es salaam.

Kabla ya kufika kibamba na kwa sababu ambazo ufoo hakuzieleza, alimkariri mzazi mwenzake huyo akisema alikuwa amefikia uamuzi wa kujiua yeye na mtoto wao.

“hata sijui ni nini kilitokea. Wakati tukitoka nyumbani antheri alianza kwa kuniambia kwamba alikuwa amepanga kujiua yeye na mtoto wetu,” alisema ufoo kabla ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa na kuendelea na simulizi yake ya kusikitisha.

Akiwa na sura ya ujasiri, ufoo anasema pamoja na kumwambia maneno hayo bado mushi alimsisitiza kwamba waende kwa mama yake (ufoo) baadae warudi kumchukua mtoto wao japo ufoo hakusema walitaka kwenda wapi baada ya hapo.

Alisema walipofika nyumbani kwa mama yake walikwenda moja kwa moja sebuleni na wakiwa wamekaa kwenye makochi baada ya salamu za hapa na pale ghafla mushi akasimama akamwambia mama yake ufoo kwamba; “mama nimeishafanya maamuzi”

kwa mujibu wa maelezo ya ufoo, baada ya mushi kutamka maneno hayo ghafla akaingiza mkono nyuma ya suruali alikokuwa ameweka bastola yake na kisha akaichomoa.

Katika maelezo yake ufoo alisema baada ya kuichomoa bastola hiyo mama yake naye alisimama na kwenda kujaribu kumpokonya, kitendo hicho kilimfanya amiminiwe risasi mfululizo.

Alisema kuona hivyo aliamua kukimbia kuelekea jikoni ambapo mushi alimuona na kuanza kumiminia risasi ambayo moja ilimpata eneo la mkono wa kulia ambayo ilitokezea mbele na kuchana titi la kulia.

Kwa mujibu wa ufoo jeraha hilo halikumfanya akate tamaa ya kunusuru maisha yake kwani alijaribu kukimbia ingawa antheri alifyatua risasi nyingine kadhaa ambazo zilimpata juu kidogo ya mgongo na kutokea tumboni ambazo zilisababisha aanguke chini

akiendelea kusimulia, anasema ingawa alikuwa akivuja damu nyingi, na huku akijiburuza ardhini, ufoo alisema wakati akitambaa aligeuka nyuma na akamuona antheri akijielekeza bastola eneo la kidevu na alipofyatua risasi alianguka chini.

“nikiwa chini nilimuona antheri akijipiga risasi kidevuni na akaanguka chini, sikujua kilichofuata baada ya hapo kwani niliendelea kujiburuza ili kuokoa maisha yangu,” alisema ufoo

alivyojiokoa

“nyumbani kwetu, pale kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.

Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.

“nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.

“si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,” alisema ufoo.

Alisema muda mfupi tu baadaye alitokea kijana aliyekuwa na pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda ambaye alimuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ya tumbi na akakubali.

“yule kijana aliniuliza iwapo nilikuwa ninao uwezo wa kujishikilia vizuri na niliposema nitaweza akanisaidia kupanda katika bodaboda.

“wakati huo nilikuwa naona kama tumbo linazidi kujaa. Nikiwa kwenye pikipiki kuna wakati nilikuwa nikihisi kwamba naweza nikaishiwa nguvu na kuanguka katika barabara na kisha kupitiwa na gari na kupoteza maisha. Lakini nilipata ujasiri na kujishikilia,” alieleza kwa sauti ya chini.

Alisema anakumbuka wakati walipofika eneo la kibaha ilipo mizani ya kupima uzito wa magari makubwa walikuta barabara ikiwa imejaa magari na yeye alimuomba dereva huyo wa bodaboda kupita hata nje ya barabara eneo la nyasi ili kumwahisha hospitalini jambo ambalo kijana yule alilifanya.

“nilipofika eneo la mapokezi pale tumbi nilimueleza muuguzi niliyemkuta kwamba nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi na nikamuomba asaidie kuokoa maisha yangu. Yule nesi alisita akitaka kwanza kupata kibali cha polisi (pf3) lakini nikaumuomba apigiwe simu, kaimu mganga mkuu wa tumbi, dk. Dattan ambaye tunafahamiana”

“baada ya muda mfupi dk. Dattan alifika na nikamweleza yaliyonipata na mara moja nikaanza kuhudumiwa kwa kuniwekea dripu, na nikamsikia akiwaeleza wauguzi kwamba isingekuwa busara kwa hali niliyonayo kama wangeanza kuchukua picha za x-ray kwani hatua hizo zingeweza kusababisha kupoteza maisha,” alieleza akikumbuka yaliyojiri hapo tumbi.

Kwa mujibu wa ufoo, akiwa bado ana fahamu alimsikia daktari aliyekuwa akimhudumia akiomba msaada wa gari la kubeba wagonjwa ili limchukue na kumkimbiza katika hospitali ya taifa ya muhimbili wito ambao ulijibiwa kwa maelezo kwamba lilikuwa halina mafuta.

Majibu hayo kwa mujibu wa ufoo, yalisababisha daktari huyo aombe kuletewa gari la wagonjwa la wagonjwa maarufu (vip) ambalo lililitwa na muda mfupi baadaye akapakizwa tayari kwa safari ya kukimbizwa muhimbili.

Alisema wakati akikimbizwa muhimbili anakumbuka namna alivyokuwa akipatwa na maumivu makali wakati wote gari ile ya wagonjwa ilipokuwa ikipanda matuta ya barabarani na kuna nyakati alikuwa akihisi kupoteza pumzi na kuishiwa nguvu.
Mtanzania

ufoo mungu bado anampango na maisha na maisha yake. Tuendelee kumwombea uzima atimize kusudi lake la kupewa second chance na mungu wake salama. Subiri kuongea ukweli ukipona vizuri dada
 
Ni kweli, hajaanika yote. Chanzo cha ugomvi ni nini? Kwa nini marehemu alilazimisha waende Kibamba?
Kuna mengi msiyoyajua kuhusu huduma za afya Tz. Wengi huuawa na watu hawa wasemao hakuna mafuta, gari iliyopo ya vip, hakuna drip, dk wa dawa ya usingizi hayupo nk huku serikali ikiwa mortury
 
Ufoo hawezi sema kweli,Yaani Mushi aseme tu bila sababu eti amefikia maamuzi haya,Ufoo anapondanganya itabidi atumie akili sana ili watu wasigindue uongo wake

Mkuu Azonte, uongo wa Ufoo umeishafahamika na watu wameishajua chanzo cha mzazi mwenzie kufanya maamuzi magumu! Ufoo amshukuru Mungu hakufa na hayo ni makusudi ya Mungu ili atubu na kujutia dhambi zake!
 
Ufoo hawezi sema kweli,Yaani Mushi aseme tu bila sababu eti amefikia maamuzi haya,Ufoo anapondanganya itabidi atumie akili sana ili watu wasigindue uongo wake

hapo umenena
 
mbona hasemi kuhusu nyumba alomdhulumu mushi na vyombo kibao vya kuanzisha studio, bado hela walizomtapeli kushirikiana na mama yake? akifinywa atasema ukweli tu.
 
Inasikitisha sana lakini story haina ukweli wowote! Mzazi gani anayeamua kuua mtoto wake na kujiua yeye bila kuwepo na sababu ya msingi?
Kaeleza vizuri jinsi alivyojiokoa kituo kwa kituo lakini kwenye suala la nini hasa chanzo cha ugomvi anaa mumunya mumunya....!
 
Watu kujifanya wanaijua sana hela, haya ss wamekutana wanaoijua hela watupu
 
Ufoo hawezi sema kweli,Yaani Mushi aseme tu bila sababu eti amefikia maamuzi haya,Ufoo anapondanganya itabidi atumie akili sana ili watu wasigindue uongo wake

Ufoo umefanya ufisadi wa pesa za mushi na kisha ukaanza usaliti wa kimapenzi. Uwe mkweli usidanganye watu.
 
Hapa kafunguka au kafungika hata mtoto anaona kina kitu!mbona nasikia wamekuta matundu mawili ya risasi??anayejiua tena kaweka kidevuni ndo mipenyo ya risasi miwili?bunduki yake ilikuwa na risasi 15 ufoo kapigwa 2-15=13 mamake ufoo risasi 5-13=8 hizi nane ndo zilikutwa katika bastola je zilizo mpiga mushi zilitoka wapi?au kauliwa?
 
angalia body language ya u4 anafika mhi2 camera ilimwonyesha kama anainuka kwenye wheal bed .maana yake ni sign ya kujipongeza the mission is complete!
 
Habari hii inaonyesha ni jinsi gani alivyo na taa ya mali tena inaonekana kulikuwa naushirikiano kati ya Ufoo na mama yake katika hujuma hii kwa Mushi ndio sababu ya hawa kulazimika kukutana usiku huohuo,Ufoo ni mwanamke hatari sana onaanavyoficha chanzo cha ugomvi kwa nguvu na kwa kulazimisha.
 
Watu mnashangaza sana. Mnamlaumu sana ufoo ataje sababu. Ili iweje? Hayo ni maisha yake na matatizo yake binafsi si lazima aitangazie dunia. Akipona atahojiwa na km anakosa atachukuliwa hatua vile vile.

Haijalishi source ya mushi kuchuchukua maamuzi km hayo ni nini. Mushi hakupaswa kuchukua uamuzi aliochukua no matter ufoo amemfanyia nini. Atakuwa ni chizi tu upstairs. Mwanaume unatakiwa ukabiliane na tatizo na ujue jinsi ya kukitatua. Lakini si kuua.

Mushi alikuwa na matatizo ya akili tu. Km alishachoka maisha angejifyatua yeye mwenyewe peke yake.

Haya mmachame umesikika
 
Hapa kafunguka au kafungika hata mtoto anaona kina kitu!mbona nasikia wamekuta matundu mawili ya risasi??anayejiua tena kaweka kidevuni ndo mipenyo ya risasi miwili?bunduki yake ilikuwa na risasi 15 ufoo kapigwa 2-15=13 mamake ufoo risasi 5-13=8 hizi nane ndo zilikutwa katika bastola je zilizo mpiga mushi zilitoka wapi?au kauliwa?

U have a point mkuu.
Hapa kuna kitu kikubwa sana nyuma ya pazia ila nna huzuni coz kitaishia juu kwa juu
BTW kwa waandika script nzuri wanaweza wakatengeneza bonge la movie
 
Back
Top Bottom