Ufisadi wa Unaofanywa katika Jumuiya ya Wanyamapori ya Burunge, Manyara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Unaofanywa katika Jumuiya ya Wanyamapori ya Burunge, Manyara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wambugani, Apr 23, 2012.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kama inavyofahamika Serikali yetu tukufu ilianzisha jumuiya za hifadhi ya wanyama pori ili kudumisha uhifadhi wa maliasili na kunufaisha wakazi waliopo katika maeneo hayo lakini mimi kama mwanakijiji wa Kakoi nimesikitishwa na hujuma zinazofanywa na viongozi wa wanyama pori wa Wilaya ya Babati na Kamati Tendaji.
  Masikitiko ni kwamba kuna ukiukwaji na hujuma katika mambo mbalimbali kama ifuatavyo:-

  1. Mwaka jana gari chakavu lilinunuliwa kinyemela kwa Shs. Milioni 40 pasipo kufuata sheria ya ununuzi ya umma na kisha jumuiya ikatoa tena zaidi ya Shs. Milioni 16 kwa ajili ya matengenezo ya gari hilo na hadi leo halijaingia barabarani na wala halijulikani ilipo. Kwa kiasi hich cha Shs. Milioni 56 zilizotolewa ingewezekana kununuliwa magari kama Toyota Prado matatu mapya au zaidi.

  2. Kuna hoteli ya watalii iliyopo Kijijini Kakoi inayomilikiwa na Bwana Sheni a.k.a Muhsin Abdallah, Mjumbe wa NEC – CCM (M) Kigoma inalaza wageni pasipo lulipa ushuru kwa jumuiya hiyo. Ninahisi huyo mmiliki wa hoteli analindwa na viongozi wa wilaya au wa jumuiya kama siyo ngazi ya taifa. Tunafahamu Bwana Sheni aliwapeleka viongozi wa vijiji vyetu kwa ndege hadi katika hoteli yake iliyopo Kigoma. Je, hiyo siyo rushwa ya wazi?

  3. Kumekuwa na matumizi makubwa ya viongozi kwa kujilipia posho mbalimbali na kuwalipa Mawakili kwa kesi ambazo zingeendeshwa na Wakili wa Serikali.

  4. Afisa WanyamaPori wa Wilaya kuchukua fedha kutoka Jumuiya pasipo utaratibu wo wote na kufanya uchaguzi ili Kamati ya Utendaji iliyoidhinisha ufisadi ichukue uongozi.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wilaya ambaye ni DC, Dk. Ian Langiboli na Idara ya Wanyamapori wamekaa kimya bila kuchukua hatua yo yote dhidi ya ufisadi huo.

  CHANZO: Burunge WMA
   
 2. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kaka unapatikanaje maana huko kwetu
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ufike huko Burunge utashuhudia hayo madudu.
   
 4. m

  massai JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dawa ya haya majizi iko inachemka na mpaka ifikapo '15 itakua imeshaiva.tutataifisha na kuwatoza kodi zote walizo kwepa na jela wataenda
   
 5. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huu ufisadi Kagasheki unaujua?
   
 6. M

  Mtoto wa tembo Senior Member

  #6
  Nov 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimegundua kagasheki ni mropokaji tu na wala sio mfuatiliaji.amekua mtu wa matamko na mikwara.kama hizo z a wakubwa zake hawezi gusa kabisa.HAKUNA MSAFI SISIEMU YOTE MAJIZI TU.
   
 7. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2016
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Ndugu nitakupataje?

  Nahitaji kufahamu zaidi kuhusu mambo uliyoandika hapa (for research purpose). Tafadhali ni PM.
   
 8. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2016
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Ndugu nitakupataje?

  Nahitaji kufahamu zaidi kuhusu mambo uliyoandika hapa (for research purpose). Tafadhali ni PM.
   
 9. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2016
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Fuatilia kutoka ofisi ya Jumuiya ipo Kijiji cha Mwada, Wilaya ya Babati.
   
 10. BAFA

  BAFA JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2016
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,333
  Likes Received: 2,880
  Trophy Points: 280
  Fitina ndio mwendo wa Siku hzii
   
 11. Lancanshire

  Lancanshire JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2016
  Joined: Sep 20, 2014
  Messages: 13,775
  Likes Received: 7,925
  Trophy Points: 280
  Umeiandika kimbeya na kimajungu Sana. Milioni 56 Prado 3 au zaidi una malaria wewe.
   
Loading...