Ufisadi wa CHADEMA Moshi: Ofisi zote Halmashauri ilikuwa zifungwe kwa wiki nzima!!!

Hao ndio wamepewa udiwani tu, ukiwapa nchi? kwi kwi kwi teh teh teh.

Udiwani haugawiwi wala nchi haigawiwi, kama mlikuwa mmezoea kugawana, tumewaonyesha kwamba tabia hiyo hatuitaki. Hatuvumilii mpuuzi yeyote. Ukileta uzandiki na wizi ukiwa mwanachama wa CHADEMA unafukuzwa mara moja. Tunwaonyesha mfano, tumefanya, na tutaendelea kutenda kile kilicho sawa. Hatuwaombi wezi na wanafiki kujitafakari na kujivua magamba, sisi tunawafukuza mara moja.


Tabia ya kulea wezi ni tabia ya kawaida CCM.

Kama kilichhofanyika ni kweli, basi wote, haijalishi nani yupo chama gani, wote wameweka uzalendo pembeni na kuamua kuwa mchwa wa nyumba tunayojenga.
 
Mimi nasema Hakuna chama chenye matatizo Bali Watu ndo wenye matatizo yaliyotokea Mwanza kwa meya Watu tumeona na moshi tunaona nadhani sasa jibu tumepata.
 
Haya twende, moja, mbili, tatu," Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wake,............."

Kama kweli lengo la safari hiyo lilikuwa kwenda kujifunza usafi, basi hatuna budi kukubaliana nao (waliotaka kwenda safari hiyo) kutokana na uchafu dhahiri waliouonyesha kuwa nao.

Hakuna uzalendo tena! Kila mtu anataka kusafiri. Baba anasafiri, mama anasafiri na watoto nao wanataka kwenda safari kubembea na kusafisha macho. Wote wakiwa wanasafiri nani atakayelinda nyumba? Ndiyo maana wezi (mikataba mibovu, mafisadi, wala rushwa na wawekezaji uchwara) huingia kwa urahisi na kuiba. Ten percent hizi au posho a.k.a ndururu, ngawila, faranga au mpunga, zitalipeka Taifa hili pabaya mpaka lini?
 
Kama wanataka kuona usafi wa Kigali si wamtume diwani mmoja na video camera akawapigie video na picha awaletee? Shida itakuwa kama wanataka kunusa harufu ya jiji la Kigali!!!
 
Je, hizo fedha ni kutoka katika kifungu kipi, cha bajeti ipi? Je si ufisadi wa hali ya juu kukaa miezi lukuki kwa ajili ya kikao cha bajeti bungeni wakati mambo yanaendeshwa kienyeji tu?
 
Kwa miaka mingi sasa mji wa moshi umekuwa mfano wa kuigwa kwa kusimamia vema usafi. ni maajabu eti wanaenda kujifunza usafi.

halmashauri nzima wanataka kwenda kujifunza usafi, ubinafsi wa kiwango cha juu kabisa.
 

Huyu Meya mwaka 2002 alikuwa ni muuza nafaka katika maeneo ya Kiusa soko.la Juu. He was very troublesome. Hana maono ya kiuongozi wala historia ya kisiasa yenye msingi wa utu na huruma kwa binadamu wenzake.
 
Mimi nasema Hakuna chama chenye matatizo Bali Watu ndo wenye matatizo yaliyotokea Mwanza kwa meya Watu tumeona na moshi tunaona nadhani sasa jibu tumepata.

CCM ina msururu ya watu wenye matatizo lakini wanamezea hakuna hatua inacchukuliwa wezi wanafugwa ,kupandishwa vyeo kuwa mabalozi,wakuu wa bodi, au wakuu wa mikoa ndio tofauti na CDM
 

Kwanza kama kweli hii issue ni sahihi,kuna haja ya Meya,DED,DC,na DT,wote wajivue MAGAMBA.

yaani mungu tuombe atupe pumzi tu,mpaka 2015 tutaona vioja kweli nchi hii.

Kwa nini usubiri hadi 2015 wakati vioja ndiyo hivyo vinavyoendelea,kikubwa hapa ni vyema tukachukua hatua mapemba badala ya kusubiri huko,masuala ya ufisadi ndugu yangu siyo ya kunyamazia mwanawane!

Mohammed Bilal inafanya Kazi gani ... anatembea na mkasi mfukoni nchi nzima .. JK amesharudi kutoka kenya?

Acha utani kwenye maana,unamanisha nini?!

kama ni kweli hawa madiwani ni mafisadi...hongera mkuu wa mkoa ila isiwemo hila ya kisiasa

Safi sa RC wa kilimanjaro,tunahitaji wakuu wa mikoa kama hawa ambao wanatake action mapema badala ya kusubiri fedha zitafunwe kwanza ndiyo waanza kuwajibisha watu,zuia halafu tafutana naye huko mitaani mshughulikie,lakini tayari fedha ya walitanzania zimeokolewa.

Hata mimi nimeisikia.Kwakweli mabadiliko ya dhati ynahitajika.Ni suala la mfumo nadhani.

Hakuna suala la mfumo hapa kinachokosekana ni uzalendo kwa baadhi ya watu wanaopendelea familia na matumbo yao.

ucwe na mawazo chakavu kwan ccm ikiiba na nyie lazma muibe

Ni kweli mdau si lazima ukigundua mwenzako kapata ukimwi eti uache kufanya ngono!


Unafaa sana kwenye mambo ya msingi tuweke ushabiki pembeni na tushikamane,kwa sababu inawezekana.Ingawa bado naamini hakuna msafi hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla.


Nakuunga mkono kaka!

Habari hii kama ni ya kweli, Meya wangu Japhar unapotupeleka ni kubaya; CHADEMA chukueni hatua tunahtaj majibu

Tana hatua za haraka sana kwa sababu mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!!!!!!!!!!haya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Kila mmoja ni Mwizi even u,hebu chukua dakika tano tu zima simu,laptop yako na kila kitu unachoamini kinaweza kukusumbua halafu ujifikirie,uone je,wewe ni msafi?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!,hata hivyo wanaobainika kuchezea mali za umma washughulikiwe
nawambia ndugu zangu ,ufisadi bwana cyo chama ni m2 ona sasa hapo meya chadema anakuwa fisadi lakini mkuu wa mkoa wa ccm kakataa ufisadi ,nashauri kwene ufisadi tusikiseme chama tumseme mhusika.

Hata kwenye biblia imeandikwa hivyo,hujakosea,na kibaya zaidi wengi huzaliwa katika hali hiyo.


Sasa hao wanaofanya ni viongozi au wanachama wa chama gani?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


THUBUTUUUUUU,KUNA MZALENDO NCHI HII?????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Acha ushabiki wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ufisadi ni ufisadi tu!,hamna wa cdm au cmm,na kwa sababu tunawategemea cdm ndio wawe mbadala wa ccm katika kuleta unafuu wa maisha kwa mtanzania thts why tunaona sio fair kung'ang'ania safari iyo!

Haswaaaaaaaaaaa!!!wewe tunaweza kukaa pamoja!!!


Na ndicho kinachotakiwa kama kweli tunahitaji ukombozi kwa wote.
 

Wewe unaonesha Kiswahili si lugha mama kwako, hivi lugha mama kwako ni ipi? punguza hizo "w" za nne kutoka kulia.
 
Du, asante sana, WABHEJA SANA, Mkuu!
I could nt have done it better!
Uzalendo kwanza vysma baadaye.
 
Hivi Jaffari ndo yule aliyekuwa akiicheze ushirika ya Moshi miaka ya nyuma?
 
jamani huyu si marehemu au?

mkuu nilitaka kuuliza swali hilo hilo huyu jamaa ameshawahi kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma miaka ya 2000, na nilisikia alifariki lakini leo mdau anasema mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ni Lawrence gama
 
CCM ina msururu ya watu wenye matatizo lakini wanamezea hakuna hatua inacchukuliwa wezi wanafugwa ,kupandishwa vyeo kuwa mabalozi,wakuu wa bodi, au wakuu wa mikoa ndio tofauti na CDM

Kwahiyo Chadema nao wameona waige?
 
duu..hela zao wenyewe na si za serikali hapo sawa lakini kama ni za serikali na wanataka kwenda wote si sawa kabisa.
 
huo ni mchongo wa kula fedha za wananchi bure,sijakubaliana nao kuhusu kujifunza kufanya usafi.wangeteuliwa wachache kwa niaba ya wengine.
 
Kuna kitu kilichoanza kuzoeleka ambacho kinanisikitisha sana. Ni huu mtindo wa kufanya kazi kupitia vyombo vya habari. Inakuwaje taratibu za kazi zinapokiukwa, mkuu mhusika anaita TV, redio au gazeti kutangaza hatua za kiofisi alizochukua. Nimeiona kwa Mh. Mwakyembe akitoa vitisho huko TAZARA. Magufuli ndio kawaida yake. Kova kila wakati kututangazia kukamatwa kwa majambazi wasio na majina bila hata kutuarifu kesi ngapi za watu hao zimefanikiwa mahakamani. Juzi nikamuona Malima naye akifoka hadharani. Hata kama kuna nia nzuri ya kudhibiti uzembe kama inavyoonekana huko Moshi, wanapoyaleta haya mambo in public, je, wanatupa data zote kuhakikisha umma tunakuwa na uelewa kamili wa hayo maamuzi?

Aidha, kwa mfano, unapomtishia mtu mzima kwa jina kupitia public media kwamba utamfuta kazi si kumdhalilisha mbele ya jamii na familia yake bila sababu za msingi. Isingetosha kuchukua hatua za kiofisi kupitia taratibu zilizowekwa bila kelele za hadharani? Mimi tafsiri yangu ni kuwa unaingiza siasa kwenye kazi ya umma na kujaribu kupata mileage kirahisi ilhali utendaji wako ni wa mashaka. Inawezekana pia ukawa mkakati wa serikali baada ya kushindwa kudhibiti wizi/uzembe mkubwa ikataka kujionyesha kwa umma kwa vihatua mbuzi vilivyotakiwa kuwa mambo ya kawaida ya ndani ya ofisi. Na sisi tunapofurahia na kuchangamkia kelele hizo tujue tunapotezwa lengo kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…